DAWA ZA KUPUNGUZA MAUMIVU YA MWILI HUSABABISHA MTU KUPATWA NA MARADHI YA MOYO MUJIHADHARI

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,319
33,125
DAWA  ZA KUPUNGUZA MAUMIVU HUSABABISHA MARADHI YA MOYO.jpg
DAWA YA KUPUNGUZA MAUMIVU IBUPROFEN.jpg
MTU MWENYE UMRI WAMAKAMO.jpg


DAWA ZA KUPUNGUZA MAUMIVU HUSABABISHA MARADHI YA MOYO...

Matumizi ya dawa za kupunguza maumivu na uvimbe huchangia ongezeko la hatari ya kupata maradhi ya moyo, utafiti umebaini.
Dawa kama vile Ibruprofen, Naproxen na Diclofenac ndizo dawa hutumiwa sana kupunguza maumivu na kuvimba.
Jarida la Uingereza la madaktari, linasema watafiti waliwachunguza watu milioni 10 , wenye umri wa miaka 77 ambao walitumia dawa hizo.
Wataalam wa Uingereza wamesema utafiti huo haukuwa na umuhimu sana kwa wagonjwa wenye umri wa chini ya miaka 65 lakini muhimu zaidi ilikuwa kwa wagonjwa wenye umri wa makamo.
Utafiti huo ulifanyiwa watu milioni 10 wanatumia dawa hizo kutoka Uingereza, Uholanzi, Italia na Ujerumani na kulinganishwa na watu wasiotumia dawa hizo.

Watafiti kutoka chuo kikuu cha Milano- Bicocca nchini Italia, walibaini kwamba kati ya wale wanaotumia dawa hizo za kupunguza maumivu, asilimia 19 hupelekwa hospitali kwa matatizo ya moyo.

'TAHADHARI'

Shirika la Uingereza la masuala ya moyo (BHF) limesema wagonjwa wanaougua maradhi ya shinikizo la damu, kisukari na shida za figo wanastahili kutumia dawa hizo kwa kiwago kidogo na kwa muda mfupi.

Mkurugenzi wa shirika la BHF, Profesa Peter Weissberg amesema utafiti huo umesisitiza uchambuzi wa hapo awali kwamba wagonjwa ambao wenye shida za maungio, wamo katika hali ya hatari ya kupata shida za moyo.
'Haswa kwa wale ambao hutumia dawa hizo za kupunguza mauamivu kila mara.'
 
Back
Top Bottom