Dawa za kuondoa sumu mwilini zilivyoondoa uhai wa rafiki yangu

ngulukizi

JF-Expert Member
Oct 10, 2018
239
1,000
Ni miaka 3 sasa tangu rafiki ambaye kwa namna moja au nyingine tulishibana sana aliponitoka kimasihara tu.

Nakumbuka ilikuwa Kariakoo siku hiyo tulipokutana na wale jamaa wanaouza dawa za kuondoa sumu mwilini ndipo nasi tukaona kuna umuhimu wa kuzinunua na kuzitumia ili tuondoe mafuta mwilini.

Kweli tukanunua mimi na mwenzangu tukatumia baada ya muda tulikuwa tunaenda chooni kila mara kiasi kwamba tukaona ni mchezo tu kidogo chooni tunatoa haja kubwa kisha tunarudi kupiga story huku tukiambiana leo sumu na takataka zote zinaondoka mwilini.

Kumbe ile dawa ilienda kufanya figo za rafiki yangu zifeli ghafla akaanza kutapika na kuharisha mfululizo ikabidi tumuhamishe Muhimbili pale hapo muda huo mimi niilikuwa na afueni sijui kwangu nini kilitokea maana ile kuharisha ilikata ghafla baada ya kuona hali ya mwenzangu tulipofika Muhimbili wakasema twende Mloganzila tukaenda na hapo hapo baada ya kuangalia vipimo madaktari wakasema figo zimefeli hivyo acha wahangaike ili apate nafuu.

Nakumbuka usiku wa tarehe 23 kuamkia 24 December jamaa yangu alifariki.

Bado ninakukumbuka ndugu yangu na rafiki yangu RIP.
 

h120

JF-Expert Member
Jan 10, 2012
2,415
2,000
Mloganzila imefunguliwa rasmi 2017 November, sasa tukirudi miaka mitatu nyuma ni 2016.
R.I.P
 

gasgas

JF-Expert Member
Jan 25, 2015
1,254
2,000
Ni miaka 3 sasa Tangu rafiki ambaye kwa namna moja au nyingine tulishibana sana aliponitoka kimasihara tu.

Nakumbuka ilikuwa kariakoo siku hiyo tulipokutana na wale jamaa wanaouza dawa za kuondoa sumu mwilini ndipo nasi tukaona kuna umhimu wa kuzinunua na kuzitumia ili tuondoe mafuta mwilini.Kweli tukanunua mimi na mwenzangu tukatumia baada ya mda tukwa tunaenda chooni kila mara kiasi kwamba tukaona ni mchezo tu kidogo chooni tunatoa haja kubwa kisha tunarudi kupiga story huku tukiambiana leo sumu na takataka zote zinaondoka mwilini

Dah kumbe ile dawa ilienda kufanya figo za rafiki yangu zifeli ghafla akaanza kutapika na kuhalisha mfululizo ikabidi tumwahishe Mhimbili pale hapo mda huo mi nilikua na afueni sjui kwangu nini kilitokea mana ile kuhalisha ilikata ghafla baada ya kuona hali ya mwenzangu tulipofika mhimbili wakasema twende mloganzila tukaenda na hapo hapo baada ya kuangalia vipimo madaktari wakasema figo zimefel hivyo acha wahangaike ili apate nafuu

Nakumbuka usiku wa tarehe 23 kuamkia 24 december jamaa yangu alifariki

Bado ninakukumbuka ndugu yangu na rafiki yangu RIP.
Pole sana.
Ndio muone faida ya kununua nunua dawa za kuondoa sumu. Wajinga ndio waliwao.

Solution rahisi, kula kwa afya, kula matunda na mboga za majani kwa wingi, maji ya kutosha na piga mazoezi ya kutosha.

Kilichotokea mmehara na kutapika mmepoteza maji mengi mwilini hivyo hata kiwango cha damu kinachofika kwenye figo kikapungua mwisho figo zikashindwa kufanya kazi yake.

Hii inaitwa Acute Kidney Injury (AKI)

Sent using Jamii Forums mobile app
 

tashwishwi

JF-Expert Member
Sep 25, 2014
2,083
2,000
Mimi huwa nashangaa sana wizara ya afya inawaona hawa wahuni wanachezea afya za watu nao wa naangalia tu. Ujinga huu unaendekezwa kwa zile nchi zenye viongozi wasio na weledi tu
 

Elkana92

Member
Feb 18, 2018
10
45
Hawa wauzaji wa hizo dawa pia uwa wanapatkana kwenye mabasi ya abiria. .kikubwa wanachofanya ni kukutajia dalili ambazo ni familiar kwa watu wengi kisha wanakutisha kutokana na izo dalili ukishaingia mkenge unanunua na auponi
Nb. Fuata ushaur wa daktari kabla yakuchukua hatua ya kutumia dawa yoyote ile.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom