Dawa za kulevya zasambaratisha vigogo wa polisi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dawa za kulevya zasambaratisha vigogo wa polisi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Dec 25, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Dec 25, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  SAKATA la upotevu wa kilo kadhaa za dawa za kulevya zilizokamatwa Novemba 18 mwaka huu mkoani Mbeya, limechukua sura mpya baada ya vigogo watatu wa Jeshi la Polisi mkoani humo kung’olewa na wengine kuvuliwa vyeo.

  Taarifa za uchunguzi na zilizothibitishwa na baadhi ya mamlaka na baadhi ya askari polisi, zimetanabaisha kuwa kati ya vigogo wa jeshi hilo waliosambaratishwa na kutarajiwa kuondolewa mkoani Mbeya hivi karibuni ni pamoja na kamanda wa polisi wa mkoa wa Mbeya, Advocate Nyombi.

  Vyanzo hivyo vya habari vimelieleza gazeti hili kuwa mbali na kamanda huyo wa polisi wa mkoa wa Mbeya pia inadaiwa mkuu wa upelelezi wa polisi wa mkoa huo (RCO) Malindisa na Staff One nao wanatarajia kuondolewa mkoani Mbeya kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kutokana na tukio hilo la upotevu wa dawa za kulevya.

  “Baada ya vyombo vya habari kufichua upotevu wa dawa za kulevya zilizokamatwa hivi karibuni mjini Tunduma na makao makuu kutuma kikosi cha uchunguzi sasa tayari kuna taarifa za uhakika za kuondolewa wakubwa hapa mkoani Mbeya huku baadhi wakihusishwa moja kwa moja na tukio hilo,’’ walisema baadhi ya maafisa wa polisi wanaofahamu kwa kina suala hilo.

  Aidha vyanzo vingine vya ndani kutoka ndani ya jeshi hilo vimeeleza kuwa kamanda Advocate Nyombi anatarajiwa kuhamishiwa makao makuu ya polisi na kupangiwa kazi nyingine huku Malindisa akitarajiwa kuwa makamu wa RPC katika mkoa mwingine na Staff One akitarajia kuukwaa ukamanda wa polisi.

  Hali hiyo haijawashtua askari wengi mkoani hapa kwa kile walichodai kuwa walitarajia tukio hilo kwani baadhi yao historia zao za kazi siyo nzuri sana.

  Dawa zinazodaiwa kupotezwa kwa makusudi na kubadilishwa kuwa majivu kutoka mkoani Mbeya kwenda jijini Dar es Salaam ni zile zilizokamatwa Novemba 18, mwaka huu mjini Tunduma zikiwa njiani kupelekwa nchini Afrika Kusini na watu wawili:

  Vuyo Jack (29) na mwanamke mwenye asili ya Kiasia Anastacia Cloete (25).

  Dawa hizo miongoni mwake kulikuwa kilo 1200 za heroine, Cocaine na Morphine zilizoingizwa nchini kupitia mpaka huo wa Tunduma kati ya Oktoba 27 – 30 mwaka huu.
   
 2. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #2
  Dec 25, 2010
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Muhusika wa wizi wa dawa za kulevya ni rpc nyombi na wenzake kwa nini wasikamatwe ???
  Kitendo cha kuwahamishia makao makuu ya polisi kinaongeza mtandao wa madawa ya kulevya makao makuu polisi na wanaweza kuharibu upelelezi wa kesi za dawa za kulevya
   
 3. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #3
  Dec 25, 2010
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Tatizo ni kuruhusu polisi wakajipeleleza wenyewe. Katika hali kama hii ilitakiwa awepo mpelelezi binafsi hasiye polisi kushughulikia jambo hili. Hivi sasa tunayarudia yale yale ya Zombe.
   
Loading...