Dawa za Kulevya: Dkt. Abdullah na Saboori Pharma

EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,477
15,320
Kuna habari za biashara ya dawa za kulevya zimesambaa kwenye vyombo vya habari vya India zinazomhusisha Dkt Abdullah anayedaiwa kumiliki kampuni ya Saboori Pharma iliyopo Tanzania. Yeye na kampuni hiyo wanatuhumiwa kuwa na viwanda vya kutengeneza methamphetamine nchini. Kama tuhuma hizo ni za kweli, sijui kama ina kibali cha kutengeza methamphetamine. Hata kama ina kibali uhalali wa chanzo chake cha ephedrine inayotumika kutengenezea methamphetamine kina utata.

Habari hizo kutoka India zinamlenga zaidi mcheza sinema wa zamani wa Bollywood, Bi. Manta Kulikarni ambaye anatafutwa na polisi wa India kwa kujihusisha kwenye biashara ya kusafirisha ephedrine kutengeneza dawa za kulevya. Bi. Manta Kulikarni ana uhusiano wa kimapenzi na international drug lord maarufu Bw. Vicky Goswami.

Vicky Goswami ambaye ni mtoto wa polisi kutoka India alihamia Dubai miaka ya 90 kufanya biashara ya Mandrax. Hata hivyo, alikamatwa na kupewa kifungo cha miala 25 jela huko Dubai. Alikaa miaka 16 jela kabla ya kuachiwa huru na kuamua kuslimu. Baadae alihamia Zambia lakini akakimbia ili kuepuka kukamatwa na vyombo vya dola vya huko kwa kufanya biashara ya dawa za kulevya. Baadae alihamia Afrika Kusini na kuendelea kufanya biashara yake nchini humo. Kwa sasa inadaiwa Vicky Goswami yupo nchini Kenya pamoja na mtuhumiwa mwenzake Bi. Manta Kulikarni. Polisi India wanadai kuwa Vicky Goswami tayari ana kesi mbili za madawa ya kulevya nchini Kenya na kwa sasa yupo nje kwa dhamana.

Dkt. Abdullah na kampuni ya Saboori Pharma wanaingiaje kwenye hili sakata la dawa za kulevya? Kwa mujibu polisi India, Dkt. Abdullah naye ni international drug dealer kutoka Kenya na pia ni partner wa drug dealer Vicky Goswami kwenye biashara ya dawa za kulevya nchini Tanzania. Polisi India wanaamini kuwa Dkt. Abdullah alijaribu kuanzisha kiwanda cha kutengeneza dawa za kulevya Mombasa ambacho kingetumia ephedrine kutengeneza methamphetamine. Polisi India wanadai kuwa tayari Dkt Abdula ana viwanda viwili vya kutengeneza methamphetamine Tanzania.

Kwenye hili sakata, mnamo Aprili mwaka huu Polisi India walikamata tani 18.5 za ephedrine kutoka kampuni ya Avon Lifesciences Limited ya India. Kampuni hii ya kifamasia ilikuwa na kibali cha kutengeneza Ephedrine lakini ikawa inacheza “dili” na international drug lords ambao wana-process ephedrine na kuiuza kwenye soko la kimataifa kinyume na sheria.

Kwa mujibu wa polisi India, Januari mosi mwaka huu drug lords walikuwa na kikao hapa Tanzania. Kikao hicho kilihudhuriwa na Mamta, Vicky Goswami, Dr Abdullah, Manoj Jain ambaye ni mkurugenzi wa Avon Lifesciences, Jay Mukhi na watu wengine. Kikao cha pili kilifanyika Aprili 8 mwaka huu kwenye hoteli ya Burj Khalifa huko Dubai. Waliohudhuria kikao hicho ni pamoja na Vicky Goswami, Manoj Jain, Jay Mukhi, Dr Abdullah na wengine.

Inadaiwa madhumuni ya vikao hivi ilikuwa ni kujadili jinsi ya kusafirisha dawa hizo na ku-deal na mamlaka zinazopambana na biashara ya dawa za kulevya. Avon Lifesciences Limited ilikubaliana na hawa drug lords kuwa itakuwa ina-supply karibu kilo 9,000 za ephedrine bila kubugudhiwa na mamlaka husika. Kampuni zinazotengeza controlled substances kama ephedrine zinatakiwa ku-give account of their produce. Avon Lifesciences Limited ingewadanganya mamlaka husika kuwa ina-export ephedrine kwa kampuni ya Saboori Pharma ya Tanzania kutengeneza dawa za kawaida.

Baada ya kikao cha Januari, sample ya kilo 100 za ephedrine zilitumwa kutoka Avon Lifesciences kwenda Mohammed Ali Road jijini Mumbai. Kutoka pale mzigo ulitumwa kwenda Kenya on a cargo plane. Kwa mujibu wa polisi India baada ya mzigo kutua, sehemu ya mzigo ulibakia Kenya na mwingine ukaletwa Tanzania. Polisi India wanaamini kuwa mzigo ulioletwa Tanzania ulipelekwa moja kwa moja kwenye kampuni ya kifamasia ya Saboori Pharma inayodaiwa kumilikiwa na Dkt Abdullah. Baada ya mzigo kuonekana kuwa ni “good quality” sample nyingine ya kilo 1,000 ulitumwa tena kwa air cargo lakini ukanaswa uwanjani India na mamlaka husika kabla haujaletwa Afrika Mashariki.

Baada ya mzigo wa kwanza kusambazwa Vicky Goswami alimtumia Manoj Jain kitita cha fedha. Polisi India wanadai kuwa katika vikao hivyo, wahusika pia walijadili jinsi ya kugawana faida ya dili hilo na walikubaliana 33% ingekwenda kwa Vicky Goswami and Dr Abdullah, 33% kwa Manoj Jain and Punit Shringi na 33% kwa Kishoresingh Rathod na Jay Mukhi. Pia walijadili kuuza dawa hizo kwa rupee 50,000 kwa kilo moja.

Ephedrine ni controlled substance inayotumika kutengeneza dawa za kawaida lakini pia inatumika kinyume na sheria za nchi husika kutengenezea dawa za kulevya. Medically, methamphetamine inayotengenezwa na ephedrine inaweza kutumiwa kutibu ADHD na obesity. Lakini methamphetamine inatumika sana kwa ajili ya kufanya starehe. Ni maarufu kwenye kumbi za starehe kama “ice”, "meth" au “crystal”. Inawafanya watumiaji wajisikie wako “high” pindi “ice” inavyotinga ubongoni.

Pia inadaiwa kutumiwa kwa wingi na gays, waoga wa kutongoza (inaondoa aibu), wenye tatizo la kufika kileleni mapema wakati wa tendo la ndoa. Inadaiwa pia kuwa methamphetamine inaongeza “sex drive”, uwezo wa kufanya “sex marathon” kutokana na dawa hiyo kusaidia kumchelewesha mtumiaji kufika kileleni wakati wa tendo la ndoa. Methamphetamine ni maarufu kwenye porn industry kwa sababu inasaidia kuongeza muda wa erection na ejaculation.

Hata hivyo, methamphetamine ina madhara makubwa sana kwa watumiaji kiubongo na kimwili. Unaweza ku-google au pitia "Methamphetamine." DrugFacts. National Institute of Drug Abuse, Jan. 2014. Web. 14 May 2016. Tanzania, Kenya na Uganda zimeanza kusifika duniani kwa kutengeneza methamphetamine ila sijui ni kwa matumizi ya kutibu ADHD, obesity au starehe, though hapo nyuma kuna Watanzania walikamtwa na kilo 150 za methamphetamine walizokuwa wanazipeleka Afrika Kusini.

INDIAN DRUG TRAFFICKERS SYNDICATE IN TANZANIA

... Vicky Goswani a Gujarat based in Mumbai has network in Dar Es Salaam , Nairobi and Johnesburg he is international drug baron former Bollywood acter himself has connection in film industries concerning his drug supply..... his network in Tanzania are Indians based in Dar this include One Rajendra Sedashiv addressed in Upanga.....one Virat Akhtar, Rajan Nehhu aka Bada Rajan (big Rajan) addressed at Seaview/Mkocheni.

...Dawood Ibrahim Kaskar... He is an international INDIAN drug baron.....is based in India and Dubai his network in Tanzania is extensive with various addresses in Dar which are operated by INDIANS by the following names.
Chhiota Shakeel.....Area in between Uhuru/Nkrumah/Libya street.
Varadajan Mudaliar....Muhimbili-Fire and undiclosed area.
Abu Salem and one Rajit Goshni.

NB: let the Gov't go after INDIANS also not not limit this operation wthin Local folks only.

Source: Fresh details emerge on drugs saga as Makonda names 10 more suspects
 
[QUOTE=".[/QUOTE]

Asante kwa somo la phamasia.
"Do one good thing in a day".
Wahusika bilshaka watakusoma na ku-take ACTION !
 
Kazi ipo, hii biashara hii! Hawa drug lords huwa na mtandao mkubwa sana toka vyombo vya ulinzi na usalama hadi viongozi wa Serikali.
 
Nikiwakumbuka hawa wahanga wa madawa ya kulevya
Albert mangwea RIP
Whitney Houston RIP
Rehema Chalamila
Chid benz
Mateja wa mwananyamala na kinondoni
Na kila mwathirika wa madawa ya kulevya

Na Nikikumbuka mitandao na nguvu na utajiri walivyo navyo hawa ma drug dealers ... Nabaki kimya na kutafakari mengi bila majibu
 
MWENYE ENZI MUNGU atulinde na kutuepusha na balaa hili...alinde watoto wetu, maana vinatisha jamani...
 
Nikiwakumbuka hawa wahanga wa madawa ya kulevya
Albert mangwea RIP
Whitney Houston RIP
Rehema Chalamila
Chid benz
Mateja wa mwananyamala na kinondoni
Na kila mwathirika wa madawa ya kulevya

Na Nikikumbuka mitandao na nguvu na utajiri walivyo navyo hawa ma drug dealers ... Nabaki kimya na kutafakari mengi bila majibu


hii biashara inamaliza generation ya vijana... MUNGU wangu
 
Good to see you back. Umepotea sana. Kuhusu huyo drug king, hii itakuwa kipimo kingine cha utendaji wa Magufuli akisaidiwa na Mwigulu
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Ndıo maana teja akıkushıkıa mkeo we anza kutafta mke mwıngıne tu!mateja wanakojoza bana!
madawa yana madhara makubwa kulıko unavyodhanı!kuna wengıne wanaanzıa ktk kusafırısha(punda)baadae anaanza kutumıa hıyo nımeona sana kwa vıjana wengı wa kıtanga. wengıne wamekuwa mateja kwa ajılı ya kutafta sex drıve au kutoa nıshaı ılı kotongoza hatımaye unajıkuta teja tayarı!mbalı na hapo mapunda wengı wamekuwa mashoga sbb kutıwa mavıfaa huko nyuma wakatı wa kushusha mzıgo!usıombee umeze afu pıpı moja ılale kıubavu haıtokı hadı uchokolewe.hıvyo unakuta huko nyuma panakuwa dısturbed na kupelekea kutekenya.ndugu zangu nawaasa na kujıasa usıje kujııngıza ktk haya mambo kbs
 
Mods msınıpıge ban kwa hıyo msg bıla kukemea kwa kutoa aıbu zake tutajıkuta tunazıdı kupoteza ndugu na marafıkı.me nıshapoteza 2 tayarı mwaka huu
 
  1. Saboori Pharma kipo india
  2. kuna kiwanda lab equipment cha keko mwanga kinamilikiwa na familia ya saboori
  3. mkurugenzi wake reza saboor ni balozi wa heshima wa MEXICO ( DRUG PARADISE) hapa Tanzania serikali inamtambua(an honorary consul of Mexico in Tanzania)
  4. dkt abdullah simjui wala sijawahi msikia
  5. mengine endeleeni kutiririkaa................... c.c EMT
 
  1. Saboori Pharma kipo india
  2. kuna kiwanda lab equipment cha keko mwanga kinamilikiwa na familia ya saboori
  3. mkurugenzi wake reza saboor ni balozi wa heshima wa MEXICO ( DRUG PARADISE) hapa Tanzania serikali inamtambua(an honorary consul of Mexico in Tanzania)
  4. dkt abdullah simjui wala sijawahi msikia
  5. mengine endeleeni kutiririkaa................... c.c EMT
Mungu akulinde sana .
 
  1. Saboori Pharma kipo india
  2. kuna kiwanda lab equipment cha keko mwanga kinamilikiwa na familia ya saboori
  3. mkurugenzi wake reza saboor ni balozi wa heshima wa MEXICO ( DRUG PARADISE) hapa Tanzania serikali inamtambua(an honorary consul of Mexico in Tanzania)
  4. dkt abdullah simjui wala sijawahi msikia
  5. mengine endeleeni kutiririkaa................... c.c EMT
 
Wahindi wenye maduka ya kuuza madawa ya binadamu kwa jumla ni matajiri wa kutupwa....hata nrb kuna mhindi mmoja anauza dawa za binadamu kwa jumla maisha yke ni ghali sana......nlimuuzia cutting za tanzanite 2013 hapo ofisini kwake nlikuta bundle za dola mamilioni
 
  1. Saboori Pharma kipo india
  2. kuna kiwanda lab equipment cha keko mwanga kinamilikiwa na familia ya saboori
  3. mkurugenzi wake reza saboor ni balozi wa heshima wa MEXICO ( DRUG PARADISE) hapa Tanzania serikali inamtambua(an honorary consul of Mexico in Tanzania)
  4. dkt abdullah simjui wala sijawahi msikia
  5. mengine endeleeni kutiririkaa................... c.c EMT
Huo ubalozi wa heshima wa mexico,mhindi ndio wasi wasi unapoanzia
 
Back
Top Bottom