Dawa za Kichina kuongeza makalio, bikira, matiti, hips, kukuza uume zateketezwaw Dodoma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dawa za Kichina kuongeza makalio, bikira, matiti, hips, kukuza uume zateketezwaw Dodoma

Discussion in 'Jamii Photos' started by Candid Scope, Jan 16, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Jan 16, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Kanda ya Kati, Florent Kyomo
  akimwaga bidhaa ambazo hazifai kwa matumizi ya binadamu kabla ya kuchomwa
  katika dampo la Mbwanga katika Manispaa ya Dodoma mwishoni mwa wiki.

  MAMLAKA ya Chakula na Dawa (TFDA) Mkoa wa Dodoma mwishoni mwa wiki iliteketeza bidhaa mbalimbali zenye thamani ya Sh milioni 26 ambazo hazifai kwa matumizi ya binadamu. Miongoni mwa bidhaa hizi ni dawa za Kichina za kuongeza ‘heshima kwenye ndoa’. Kaimu Meneja wa TFDA, Florent Kyombo alisema bidhaa hizo zina uzito wa tani sita na zilikamatwa
  wakati wa ukaguzi uliofanyika Novemba 14 hadi 28, mwaka huu. Ukaguzi huo ulihusu maduka 104 ambapo kati yake, maduka 33 yalikutwa na bidhaa mbalimbali ambazo hazifai kwa matumizi ya binadamu.

  Kabla ya kuteketezwa kwa bidhaa hizo eneo la Mbwanga, wakazi wanaokaa karibu na dampo hilo, walifika kushuhudia huku wengine wakiomba wapewe bidhaa hizo. “Mimi naomba mafuta hayo hata kama yameharibika nitayachemsha sana,” alisema mama moja wa makamo ambayo hata hivyo alibakia kushuhudia bidhaa hizo zikiteketea na kuamua kuondoka huku watoto wengi wakiomba kupewa juisi zilizolundikwa kabla ya kuteketezwa.

  Bidhaa zilizoteketezwa ni dawa za Kichina za kuongeza makalio, kurudisha bikira, kukuza matiti, kuongeza hips, kukuza uume na kahawa ambayo hutumika kuongeza hamasa kwa wanawake.

  Pia, vipodozi vya aina mbalimbali, dawa za binadamu, mipira ya kiume, dawa za meno, sabuni na vifaa vya maabara ambavyo havina taarifa za utengenezaji wake pamoja na vyakula mbalimbali ikiwemo mafuta ya kupikia, juisi na soda za kopo. Kyombo alisema bidhaa hizo zinateketezwa kwa gharama za mmiliki wa bidhaa ambaye husaini
  fomu za kuteketeza bidhaa hizo na kuongeza kuwa bidhaa nyingi zinatoka nje ya nchi na ni vigumu kuwakamata watengenezaji.

  Alisema jambo la msingi ni kuwasisitiza wadau kufanya biashara kwa misingi ya utaratibu na kanuni za vyakula dawa na vipozi. “Watanzania wakitilia shaka bidhaa zozote watoe taarifa ili hatua zichukuliwe,” alisema na kuongeza kuwa dawa za Kichina zinazouzwa kila kona zimekuwa na athari kubwa kwa maisha ya binadamu na baadhi zimekuwa zikiongeza shinikizo la damu.
   
 2. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #2
  Jan 16, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Yaani hapo hayo makemikali yanachomwa moto tunaachiwa ma-fumes yanaenea tu bila mpangilio.
   
 3. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #3
  Jan 16, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Duh! sasa sijui itakuwaje......
   
 4. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #4
  Jan 16, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Dawa hata za kurudisha ubikira, huu ni ufirauni sasa, hii imekaaje?
   
 5. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #5
  Jan 16, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Siku zote nilikuwa nafikiria hawa dada zetu wako natural kumbe ni artificial?
   
 6. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #6
  Jan 16, 2012
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  :hat::hat::hat: :A S 465::A S 465::A S 465: :nerd::nerd::nerd: :poa:poa:poa..........................
   
 7. Geraldo DaVinci

  Geraldo DaVinci JF-Expert Member

  #7
  Jan 16, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 277
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  duh! Kumbe kuna bikira za kichina ckuizi
   
 8. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #8
  Jan 16, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  hapo sasa kazi kwenu vidume
   
 9. chapaa

  chapaa JF-Expert Member

  #9
  Jan 17, 2012
  Joined: Feb 19, 2008
  Messages: 2,355
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  sku hizi kila mdada umuonae anariverse minikawaga nawapa sifa mabinti wa kibongo kumbe hamna lolote
   
 10. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #10
  Jan 17, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Matatizo hatuna quality check when these things are brought into TZ soil. Kuchoma moto sio preventive measure, it should be at the time of clearing these items at our borders or ports.
   
 11. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #11
  Jan 17, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Madawa mengi yamezagaa kila kona na watu wanaumusha makalio miili inaonekana mizuri kwa sura lakini ukiishika imekakamaa kama mpira wa kucheza uwanjani, hawajui ladha ya uzuri aliotuwekea Muumba wetu.
   
 12. MGAWARIZIKI

  MGAWARIZIKI JF-Expert Member

  #12
  Jan 17, 2012
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 306
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ndio maana siku hizi kuna magonjwa ya ajabu
   
 13. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #13
  Jan 17, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  dawa ya kuongeza heshima kwenye ndoa. heheheheheehehe
   
 14. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #14
  Jan 17, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Ulishaingizwa mjini nini?
   
 15. Mnyamwezi wa Urambo

  Mnyamwezi wa Urambo JF-Expert Member

  #15
  Jan 17, 2012
  Joined: Dec 7, 2011
  Messages: 932
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Kumbe wachina hadi kwenye matiti na ubikira wamo?duh hii sasa hatali!!
   
Loading...