Dawa za Asili za kuingiza Ukeni zinasababisha Cervical Cancer?

Quetzal

JF-Expert Member
Dec 9, 2018
6,330
10,750
Kuna hi Hali ya Madoctor na wanasayansi kukataza wanawake kuweka vitu vya kiasili ukeni. Huku kwenye mitandao ya kijamii kumekuwa na Matangazo Mengi sana.

Kuna mengine ya kusteam uke tukumia herbs, mengine ya kuweka unga wa mbegu za maembe kubana uke na mfanowe..na wengine wadai wanarudisha Bikra..

Mimi niliwafuata Hawa wauzaji na kuwauliza mbona haya Mambo wanasansi wanapingana nayo. Wakasema mbona wanasayansi hua wanatoa dawa za kupaka kwenye uke...na nyingine Zina vitu maalumu vya kuingizia ukeni hizo dawa.

Mbona Hawa wanasayansi Wanatoa dawa ambazo LAZIMA udumpukize kwenye uke..kwa vidole?..

Naomba kujua Je hizi Dawa za asili ninkweli Zinasababisha Cervical Cancer?

Na hizi za hospitali mfano ukiwa unawashwa uke kuna dawa unaiingiza kwa kifaa...Au pia na gynaecologist Kuna dawa huwa wanakuweka ndani ya uke kwa vidole...

Je, hizi hasisababishi CERVICAL CANCER?

Na douching Ni kwa kiasi gani in a madhara...Mimi douching huwa nafanyaga Mara Moja mpaka 3 kwa mwezi.

Nawasilisha
 
Kuna hi Hali ya madaktari na wanasayansi kukataza kuweka vitu vya kiasili ukeni.

Huku kwenye mitandao ya kijamii kumekuwa na matangazo mengi sana.

Kuna mengine ya kusteam uke, kutumia herbs; mengine ya kuweka unga wa mbegu za maembe kubana uke na mfanowe na wengine wadai wanarudisha Bikra.

Mimi niliwafuata hawa wauzaji na kuwauliza. Mbona haya Mambo wanasansi wanapingana nayo. Wakasema mbona wanasayansi hua wanatoa dawa za kupaka kwenye uke na nyingine zina vitu maalumu vya kuingizia ukeni hizo dawa.

Mbona hawa wanasayansi Wanatoa dawa ambazo lazima udumpukize kwenye uke kwa vidole?

Naomba kujua, je hizi dawa za asili ninkweli Zinasababisha Cervical Cancer?

Na hizi za hospitali mfano ukiwa unawashwa uke kuna dawa unaiingiza kwa kifaa. Au pia na gynaecologist kuna dawa wanakuwekea ndani ya uke for matibabu purposes.

Je, hii haiwezi sababaisha Cervical cancer?
 
Unaeka nyama na kushinda nayo hadi jioni, kisha unampikia mpenzioo...limbwata tosha
 
Kuweka makorokocho ukeni kunaweza kuwa kunaondoa wale bacteria wa asili na kusababisha uke kuwa mkavu sana, ama kutoa harufu mbaya, au vitu vingine, kuhusu cervical cancer sijajua.

Ila njia salama ya kubana uke ni mazoezi ya kegel

Huko mtandoni mambo mengi ya hovyo sana.

Cervical cancer huchangiwa na vitu kama magonjwa ya zinaa (HPV na HIV) kuvuta sigara, kuanza mapenzi umri mdogo n.k
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom