Yajue haya majani ni dawa ya vidonda vya tumbo

M2baki

Senior Member
Feb 25, 2013
174
309
Habarini za jioni ya pasaka ndugu wana jamvi.

Si mwandishi sana humu jamvini japo ni msomaji wa muda kidogo. Leo nimependa ku share jambo lilionipa msaada baada ya kuona watu wengi wamekuwa wakisumbuliwa na shida ya vidonda vya tumbo.

Binafsi niliumwa na vidonda vya tumbo kwa miaka mitatu Lakini nilielekezwa na jamaa niliyekutana naye. NILIEKEZWA BURE NAMI NATOA UFAHAMU HUO BURE.

Tafuta majani flani ntaatach hapa ya aina mbili nayo ambayo utayachuma na kuyatwanga yakiwa mabichi na kisha kuandaa maji ya uvuguvugu na kisha kuyachanganya na hiyo rojo na kisha chuja. Kikombe kimoja cha robo lita kwa siku 3. Nawe utapona kama nilivyopona.

Jani la kwanza scientific name ni 'Biden pilosa' na Jani la pili ni 'lippia javanica' .
Matumizi.
Chukua majani ya kwanza (Biden pilosa) ujazo wa kiganja kimoja, na majani ya pili (lippia javanica) yajae kiganja kimoja, Kisha twanga pamoja upate rojo, Kisha Chukua maji ya uvuguvugu ujazo wa kikombe cha Chai, changanya na rojo uliyobrend au kutwanga Kisha chuja mchanganyiko huo ili kupata mchanganyo. Kunywa asubuhi au jioni Mara moja kwa siku, dozi ni ya siku 3.ila kila siku tengeneza mchanganyiko huo usilaze kwajili ya Kunywa kesho yake. Tumia fresh kila siku

Enjoy the remedy.

IMG_20161215_154658_1555858127415.jpeg
 
Mkuu, naomba kufahamu kila siku unaandaa kikombe upya au utakayo andaa siku ya kwanza ndio unatumia kwa hizo siku 3 zote?
Ukiandaa kila siku ili kupata matokeo mazuri itapendeza. Hata pia nilipotumia pia niliandaa kila siku.
 
Yatafutwe,wahanga wa huo ugonjwa ni wengi,vilevile inaweza kuwa ni fursa maana mahospitalini hakuna dawa,kwahiyo ukifanikiwa kupata ukauza kwa bei nzuri utabarikiwa na Mungu...
 
Yatafutwe,wahanga wa huo ugonjwa ni wengi,vilevile inaweza kuwa ni fursa maana mahospitalini hakuna dawa,kwahiyo ukifanikiwa kupata ukauza kwa bei nzuri utabarikiwa na Mungu...
Ndio maana nimekuwa nahukumiwa nafsini, kuona nimepona gonjwa ambalo watu wanapoteza pesa nyingi na kuwa nimekaa kimya miaka inaenda na sijasaidia mtu yeyote. Atleast kwa sasa nimejaribu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom