Urinary Tract Infection (UTI): Chanzo, Dalili na Kinga/Tiba yake

JamiiForums

JF Official Account
Nov 9, 2006
6,202
4,997
Wadau wengi wamekuwa wakiumizwa na maradhi haya; hebu tuyaangalie kwa mapana yake:
Asilimia kubwa ya Watanzania hawaujui vizuri ugonjwa wa UTI. Kumekwepo na maelezo kutoka kwa watu mbali mbali na wakati mwingine hata kwa wataalamu wa afya kuhusu ugonjwa huu lakini bado watu wengi wanakanganyika na ukweli halisi.Leo nitajaribu kutoa maelezo walau kwa kina ili jamii iujue ugonjwa huu kinagaubaga.

Kwanza kabisa kirefu cha cha herufi UTI ni URINARY TRACT INFECTION ikimaanisha maambukizi kwenye njia ya mkojo.

Msomaji anapaswa kujua njia ya mkojo ni ipi, inaanzia wapi na inaishia wapi. Kwa ujumla njia ya mkojo inaanzia kwenye mrija wa mkojo kwa mwanaume na mwanamke. Mrija huu unajulikana kama URETHRA na ukishapata maambukizi ugonjwa sehemu hii unaitwa URETHRITIS.Njia ya mkojo inayofuata baada ya urethra ni BLADDER yaani kibofu.

Kibofu kikipata maambukizi ugonjwa unajulikana kama CYCITITIS. Baada ya kibofu inafuata mirija miwili inayokwenda kwenye figo mbili. Mirija hii inaitwa URRETERS na ikishaambukizwa inajulikana kama URRETITIS.Na mwisho wa njia ya mkojo ni figo mbili yaani KIDNEYS na hizi figo zikishaambukizwa ugonjwa unajulikana kama NEPHRITIS.Sasa basi ni lazima tujue ni vimelea wa aina gani wanaoleta ugonjwa wa UTI.

Hapa nitajaribu kuonisha na kupanga vimelea katika makundi maalum.

Vimelea vinavyojulikana ni kama ifutavyo:
1. BACTERIA eg Streptococci, Staphylococci, E.Coli, H.Influenza, Proteus sp.Pseudomonas etc.
2. VIRUSES eg Clamydia tracomatis
3. FUNGI eg Candida albicans
4. TRICHOMONIASIS
5. SCHISTOSOMIASIS (kichocho)
6. PARASITES
7. GONORRHEA (kisonono).

Watoto wadogo mara nyingi wanapata UTI kutokana na kutobadilisha nepi kwa wakati na hivyo unyevu wa mikojo na mavi huvuta vimelea na kuleta maambukizi. Kwa watu wazima hasa wale wanaofanya ngono zembe wanapata magonjwa ya zinaaa kwa urahisi na hivyo wanakuwa tayari wana UTI. Kuna fikra kubwa imejengeka miongoni mwa jamii kuwa UTI inaletwa kwa urahisi kwenye vyoo vya kuchangia.

Dhana hii kwangu naweza kusema si sahihi hata kidogo kwa sababu wanaume wanakojoa kwa kuagiza mkojo kwa mbali kama risasi kwenye tundu la choo, sasa hao vimelea wanafuata mkondo wa mkojo kama unavyofanya umeme? Au wanaruka na kuja kuingia kwenye tundu la mkojo? Jibu ni hapana.Kwa wanawake wao wanajisaidia kwa kuchuchamaa, wakimaliza hawatoezi au hawasoteshi nyeti zao kwenye sinki au shimo la choo na wala vimelea vya magonjwa vilivyomo chooni haviambukizi kamwe kwa ya mvuke.

Dalili za UTI zinaonekana kulingana na aina ya maambukizi.Lakini dalili kuu kwa watoto na watu wazima zinafanana nazo ni maumivu wakati wa kukojoa na pengine kutoka uchafu au usaha kwenye njia ya mkojo. Kichocho dalili zake ni kukojoa damu na maumivu. Complications za UTI nazo ziko nyingi na zinategemeana na aina ya maambukizi. Matibabu nayo yako mengi na tofauti kulingana na aina ya maambukizi.

UTI= Urinary Tract Infection ni ugonjwa unaoambatana na mfumo mzima wa njia ya mkojo kutokea kwenye mafigo, mirija ya mkojo (ureter), kibofu, tunda (prostate gland ) na njia ya kupitia mkojo kwenye uume (urethra)

Hivyo sababu huambatana na chanzo cha tatizo katika mojawapo ya sehemu husika, Mfano:

1. Ugonjwa wa sukari hufanya kiwango cha sukari kuwa kikubwa kwenye damu kwa vile mafigo kazi yake ni kuchuja damu hivyo ni kusema sukari huingia kwa wingi kiasi cha kusababisha vidudu bakteria kuzaliana kwa wingi kwenye mafigo au kibofu cha mkojo.

2. Madawa /sumu huchubua utando wa njia ya mkojo na kusababisha bacteria kuzaliana

3. Matatizo ya vijiwe kwenye figo/ mirija ya mkojo, kibofu, hufanya msongomano wa mkojo na Vijidudu huzaliana.

4. Maradhi ya Tunda Prostate gland huvimba na kufunga njia ya mkojo matokeo yake kuuzuia na kuuweka mkojo mda mrefu kwenye kibofu mpaka bacteria kuzaliana.
5. Tendo la ndoa, sexual intercouse unapata vijidudu moja kwa moja kutoka kwa mwanamke mwenye uambukizo

6. Kujichua, tendo hili mara nyingi watu hutumia mafuta au sabuni ambazo huwa zina kemikali zinazopenya kwenye mrija wa mkojo huwasha na kusababisha vidonda ambayo bacteria hukua na kazaliana

7. Usafi, aidha kwa kujikamua sana baada kukojoa, kutawaza maji machafu kutokuwa na hali ya unadhifu, huko chini kuna vijidudu ambavyo huishi baina ya njia ya haja kubwa na makorodani kutokana na hali ya ujoto humea vizuri na hupata nafasi ya kukuingia kwenye mirija kama utakuwa huna tabia ya kuwapunguza kwa usafi.

Natumai nimejaribu kukutajia sababu kuu muhimu katika mazingira ya kawaida huenda zikakusaidia kukata kiu yako.

Asante

UTI ni ugonjwa unaowasumbua sana watu wengi, hasa wanawake na watoto wadogo. Leo nitazungumzia UTI kwa wanawake na tiba yake.

Ugonjwa huu huambukizwa kwa njia ya maji maji, choo kichafu au kujamiiana na mtu mwenye UTI, pia kwa wanaopenda kufanya mapenzi kinyume na maumbile.

TIBA ASILI
Chuma majani ya mpera, uyachemshe kwa dk15, kisha chuja kwenye chombo kisafi, subiri yapoe kisha kunywa kikombe kimoja mara mbili; asubuhi na jioni kwa siku 7

au

Oshea ukeni asubuhi na jionikwa siku 7. Wakati unaanza utahisi maumivu ukeni, lakini kadri unavyoosha maumivu yatapungua na yakiisha ujue umepona. Hakuna madhara wala haiwaangamizi walinzi/ bacteria wanaolinda uke.

TAHADHARI: Usinywe ukiwa mjamzito.

Maelezo zaidi niPM





urinary-tract-infections-s1-photo-of-uti-illustration.jpg


What Is a Urinary Tract Infection?

About half of women will get a urinary tract infection or UTI at some point in life. It happens when germs infect the system that carries urine out of your body -- the kidneys, bladder, and the tubes that connect them. Bladder infections are common and usually not serious if treated promptly. But if the infection spreads to the kidneys, it can cause more serious illness.

urinary-tract-infections-s2-photo-of-hand-reaching-for-toilet-paper.jpg


UTI Symptoms: Bladder Infection
Most UTIs are bladder infections. Symptoms include:
Pain or burning during urination
The urge to urinate often
Pain in the lower abdomen
Urine that is cloudy or foul-smelling
Some people may have no symptoms

urinary-tract-infections-s3-photo-of-woman-with-kidney-pain.jpg


UTI Symptoms: Kidney Infection
An untreated bladder infection can spread to the kidneys. Signs of this include:
Pain on either side of the lower back
Fever and chills
Nausea and vomiting

urinary-tract-infections-s4-photo-of-suffering-from-uti.jpg


When to See Your Doctor
See your doctor right away if you have signs of a urinary tract infection. A bladder infection is generally not a medical emergency -- but some people have a higher risk for complications. This includes pregnant women, the elderly, and men, as well as people with diabetes, kidney problems, or a weakened immune system.

urinary-tract-infections-s5-photo-of-obgyn.jpg


UTI or Something Else?
Although burning during urination is a telltale sign of a UTI, it can also be a symptom of certain sexually transmitted diseases (STDs.) These include chlamydia, gonorrhea, and trichomoniasis. Simple lab tests are available to distinguish a UTI from an STD.

urinary-tract-infections-s8-photo-of-uti-problems.jpg


UTI Complications
The main danger associated with untreated UTIs is that the infection may spread from the bladder to one or both kidneys. When bacteria attack the kidneys, they can cause damage that will permanently reduce kidney function. In people who already have kidney problems, this can raise the risk of kidney failure. There's also a small chance that the infection may enter the bloodstream and spread to other organs.


=============
Case Studies:
Habarini waungwana mbalimbali

Mimi ni kijana wa kiume nina miaka 24 nasumbuliwa sana na u.t.i mpaka sasa toka mwaka jana. Mwezi wa 4 mwaka huu nimefanya urine culture na nikapewa dawa lakini bado tatizo lipo.

Nimechoma sindano pamoja na vidonge lakini nimalizapo tu dozi basi tatizo huanza tena. Na huwa mapumbu yanakua kama yanatekenya hivi tumbo lina choma usawa wa kibofo na vichomi vichomi katika tumbo mpaka sehemu ya kupitishia mkojo kwa chini inakua kama inawasha lakini hakuna uchafu wowote unaotoka wakati wa kukojoa. Mkojo mda mwingine ni mweupe sana mda mwingine kahawia.

Wataalam mbalimbali naomba msaada wenu tafadhari wa haraka nini nifanye nahambatanisha na majibu ya vipimo.
Wana JF naombeni msaada juu ya hili.

Mke wangu anasumbuliwa na kuumwa tumbo na mgongo mara kwa mara.

Mara ya kwanza tulienda hospitali wakasema ana U.T.I, akapewa dawa baada ya kumaliza ile dose alikaa kama miezi miwili bila hayo matatizo then akaanza tena kulalamika.

Tukaenda hospital nyingine akapewa dawa na kushauriwa aache kutumia vidonge vya uzazi wa mpango(akasitisha matumizi yake), tangu mwezi 9, mwaka jana mpaka juzi 14/01/2012 ameanza tena kulalamika tumbo na mgongo.

Kabla na nikiwa nafikiria nini cha kufanya naombeni mawazo yenu kwa uzoefu, ufahamu na ushauri wa kitaalamu juu ya hili.

Nina tatizo hili la UTI kujirudia mara kwa mara naombeni msaada wa matibabu kwa kina kwani nimetibiwa huu mwaka unaisha lakini kila nikipima tena inaonekana ipo japokuwa dalili zake hupungua.

Kwa mara ya kwanza nilikua nakojoa mara kwa mara, maumiv wakat wa kukojoa, maumivu chini ya kitovu, homa lakini kadri muda unavozidi kwenda dalili hizo zimepotea ila ugonjwa haujaisha.

Nini tatizo wajameni, ukizingatia kipindi hichi ni mjamzito; je, ugonjwa huu utaniletea matatizo kwa mtoto atakayezaliwa?
Wandugu,

Mpenzi wangu amekuwa na tatizo ambalo sasa limefikia mahala linaninyima raha kabisa....anasumbuliwa sana sana na tatizo la U.T.I na amejaribu kwenda hospitali na kupata dose....ya sindano kwa vile tatizo lilionekana kubwa na akafanikiwa kumaliza dose salama na kupona kwa wakati ule...

Sasa tatizo ni kwamba kila tunapofanya mapenzi baada ya muda kidogo lile taatizo linajirudia tena na aanapokwenda kwa daktari anakuta UTI ya kutosha sana tu!!

Mwanzoni nilidhani ni ugonjwa unaoambukizwa kwa njia ya kufanya mapenzi ndo nilipoamua kwenda nami kucheki na kukuta mkojo wangu upo okay....

Sasa hii ya juzi ndo imenishangaza mpaka sasa nipo pending......sijielewi kabisa...

Ni takribani miezi miwili hajaziona siku zake(MP),nikamshauri aende akaangalia kama ni mimba ili tupate uhakika na tukianalie mazingira ya kueleweka hicho kiumbe kijacho,

Alichokuta ni UTI tena na dokta kamwambia hakuna mimba ..... na kuna UTI nyingi sana na akapewa dose ya kutumia......

Hii kitu inatuumiza sana vichwa sote wawili na huwa maswali yaliyokosa majibu yanayojitokeza ni haya ndugu zangu....

1. Je, kuna uwezekano kweli mwanamke akapitiliza kwa miezi miwili bila MP na bila mimba vilevile?
2. Kuna uhusiano gani kati ya MP na UTI kwa wanawake?
3. Nini sasa suluhisho la kudumu la matatizo yake ya UTI? maana yanaelekea kuwa sugu sasa,na yanajitokeza mara tu baada ya kufanya mapenzi

Nahitaji sana ushauri wenu wakuu,ili tuweze nasi kuenjoy mapenzi yetu, sio siri hili tatizo linatu-disturb sana mind zetu

Thanks in Advance wakuu!!

Nakaribisha ushauri wa kujenga...

Athari kwa watoto:
Habari wana JF na wenye ufahamu na Mambo ya kitabibu.

Nimechelewa mno kugundua tatizo la mkojo mchafu kwa mwanangu wa miezi tisa.

Alianza kwa kujishikashika nyeti zake kama miezi miwili nyuma, sasa labda kwa kukosa uzoefu kwa Kuwa ndiye mtoto wangu wa kwanza sikugundua kuwa linaweza kuwa Ni tatizo, sasa mpaka tunashtuka mimi na mama yake mtoto anakojoa damu.

Tulimkimbiza haraka hospitali kariakoo kwa dk Hameer ma ametupa dawa fulani hivi ya unga ya kuchanganya ma maji ambayo anatumia siku ya pili sasa,
Ila mtoto anapata taabu sana akojoapo yaani ni kilio hatulali wala mchana hatupumziki kabisa!

Je, hii hali itakwisha kweli maana tunakosa raha kwa kweli tunapomwona mtoto wetu pekee anapata taabu namna hii.

Ana siku ya pili anatumia dawa, mtoto wetu ni wa kiume.
 
jamani wan JF naombeni msaada kwa hili! nina kaka yangu anasumbuliwa sana na UTI kama kuna mtu anafahamu dawa nzuri anielezee! ameshakunywa sana antibiotics (cipro,cephalexin,celexin etc) lakini wapi inatoka kwa muda then inarudi!

napendelea sana tiba asilia mwenye ujuzi amwage data
 
Natural Remedies for a Urinary Tract Infection (UTI)


Although natural remedies are being studied for urinary tract infection, it is important to seek medical attention and not self-medicate. If improperly treated, a urinary tract infection may spread to the kidneys. This can occur even though a person's symptoms appear to improve.
Cranberry

Cranberry juice (Vaccinium macrocarpon or Vacinnium oxycoccus) has been used for more than a century as a home remedy to prevent and treat urinary tract infection.
Although it was previously thought that cranberry worked by making the urine more acid, more recent evidence suggests that constituents in cranberry called proanthocyanins prevent bacteria from adhering to the walls of the urinary tract. This is thought to allow urine to wash away the bacteria.
A study published in the Canadian Journal of Urology in 2002 compared pure cranberry juice, cranberry extract tablets, and a placebo in 150 women at high risk for infections. Both the juice and tablets both significantly reduced UTI. Of the two, the tablets were the most effective. The National Institutes of Health and the National Center for Complementary and Alternative Health recently launched a $2.6 million dollar initiative for research into cranberries.
Cranberry juice should be unsweetened. Unsweetened juice can often be found in health food stores.
Uva Ursi

Uva ursi (Arctostaphylos uva-ursi) is a herb that is used as a folk remedy for certain types of urinary tract infection. The active component, arbutin, appears to be broken down and then excreted in the kidneys, where it appears to have antiseptic properties.
Uva ursi contains significant amounts of compounds called tannins. Tannins are not believed to be absorbed from the intestines, however, liver damage has occured with people who have taken large doses of tannins. There have been no reports of uva ursi toxicity due to the tannins.
People with kidney or liver disease or pregnant or nursing women or children should not take uva ursi.

Side effects of uva ursi can include brown or green colored urine, nausea, ringing in the ears, or indigestion. Rarely, uva ursi has been associated with retinal damage, seizures, cyanosis, cancer, or even death when taken in large amounts for long periods of time.
Other Natural Remedies

Herbs
Goldenseal (Hydrastis canadensis)
Marshmallow root (Althea officinalis)
Buchu (Barosma betulina)
Corn silk (Zea mays)
Horsetail (Equisetum arvense)

Homeopathic Remedies
Cantharis - sharp burning pain, intense urge to urinate
Staphysagria - continual burning, result of sexual intercourse

Source: Natural Remedies for Urinary Tract Infection (UTI) - Best Urinary Tract Infection Remedies
 
.UT.I ni ugonjwa sugu unaosumbua sana watu wengi hivi sasa, wakubwa kwa wadogo. U.T.I (Urinary tract Infection) ni ugonjwa unaoathiri njia ya mkojo na huweza kusababisha maumivu makali na unapojiimarisha mwilini kwa muda mrefu huathiri figo pia. Dalili za ugonjwa huu ni pamoja na mtu kusikia haja ya kukojoa kila wakati na kusisimka wakati wa kujisaidia, kusikia maumivu, kutoa mkojo mchafu na hata kutoa haja ndogo iliyochanganyika na damu.

Wataalamu wetu wa masuala ya tiba wanatueleza kuwa tatizo hili hujitokeza pale mlango wa njia ya haja ndogo inaposhambuliwa na bakteria ambao husambaa na wasipotibiwa mapema huenea hadi kwenye figo na athari zake ni mbaya.

UNAWEZA KUDHIBITI U.T.I KWA TIBA MBADALA
Kwa kawaida kila ungonjwa una tiba mbadala, siyo lazima kwenda hospitali. Unaweza kuudhibiti au kuponya ugonjwa huu kwa kunywa maji mengi pamoja na juisi itokanayo na matunda halisi, iwapo utawahi kabla tatizo halijawa sugu.

Kwa maana nyingine, unaweza kujikinga na ugonjwa huu kwa kuwa na mazoea ya kunywa maji ya kutosha kila siku. Ukinywa maji ya kutosha yatakufanya uende haja ndogo kila mara na kwa njia hiyo wale bakteria watakuwa wakitoka na hatimaye kuisha kabisa. Aidha, njia nyingine ya kuudhibitibi ugonjwa huu ni kunywa maji mengi au kwenda haja ndogo mara baada ya kufanya tendo la ndoa, kitendo hiki husaidia kuwaondoa mapema bakteria wote ulioambukizwa wakati wa kujamiiana na mwenzio.

Katika hali ya kawaida, ugonjwa wa UTI hutoweka ndani ya siku tatu mara baada ya kuanza kutumia tiba asili ya kunywa maji mengi na juisi ya matunda halisi, iwapo ugonjwa utaendelea kuwepo baada ya siku hizo, hiyo itakuwa na maana ugonjwa wako umeshakomaa na hivyo hauwezi kutibika kwa tiba hii ya nyumbani.

Katika hali kama hii, utakuwa huna njia nyingine isipokuwa kwenda hospitalini na kuonana na daktari ambaye atakufanyia uchunguzi na kukupatia dozi sahihi ambayo utatakiwa kuizingatia bila kukosa. Uamuzi huu ni muhimu hasa kama unasikia maumivu makali ambayo yanaweza kuwa yanasababishwa na kuathirika kwa figo. Kwa kawaida tiba ya kidaktari kwa ugonjwa huu huhusisha matumizi ya dawa kali za antibiotics, ambazo watu wengi wanazikimbia kutokana na athari zake za baadae (side effects). Lakini ni muhimu kufuata ushauri wa dokta na kumaliza dozi ili kuepuka uwezekano wa kurejea kwa ugonjwa, tena kwa kasi kubwa.

KUZUIA
Ili kujiepusha na ugonjwa huu, suala la usafi na kuwa na tabia ya kunywa maji ya kutosha ni jambo muhimu sana. Hakikisha unajisafisha vizuri mara baada ya kwenda haja na kubadilisha mara kwa mara nguo yako ya ndani, hasa kwa akina mama.

Vile vile usikae na haja ndogo kwa muda mrefu, nenda kajisaidie mara nyingi kadri unavyosikia kufanya hivyo. Kitu cha mwisho cha kuzingatia kwa mgonjwa wa UTI ni kupunguza unywaji wa pombe na vinywaji vingine vyenye sukari, kwa sababu sukari ni chakula cha bakteria hivyo kwa kuendelea kunywa kinywaji chenye sukari kutaifanya hali kuendelea kuwa mbaya. Ugonjwa huu ni rahisi kuepuka kwa mtu anayependa kunywa maji ya kutosha na kunywa juisi halisi kila siku.

DAYATI MUHIMU KUDHIBITI UTI
Katika kuudhibiti ugonjwa huu, pendelea kula vyakula ama vinywaji vyenye kiwango kikubwa cha vitamini C ambayo utakipata kwenye matunda ya aina mbalimbali yakiwemo machungwa, mboga za majani n.k. Jiepushe na ulaji wa vyakula vya kupaki kama vile chizi, chokoleti na bidhaa nyingine zilizotengenezwa kutokana na maziwa. Pia jiepushe na ulaji wa vyakula vyenye viungo vingi kama pilau, epuka vyinywaji vyenye caffeine, kilevi na sigara na mwisho achana na vinywaji kama soda na vinavyofanana na soda.
 
Go to the hospital for them to take a swab of your juices. Request them to culture the swab for bacteria and fungi. This will be a culture sensitivity test which will isolate the causative organisms and the best medicine to get rid of them,

Good luck!
 
jamani wan JF naombeni msaada kwa hili! nina kaka yangu anasumbuliwa sana na UTI kama kuna mtu anafahamu dawa nzuri anielezee! ameshakunywa sana antibiotics (cipro,cephalexin,celexin etc) lakini wapi inatoka kwa muda then inarudi!

napendelea sana tiba asilia mwenye ujuzi amwage data

The following are some of the antibiotic classes used most commonly to treat UTIs:
Beta-Lactams

The beta-lactam antibiotics share common chemical features and include penicillins, cephalosporins, and some newer similar drugs.
Penicillins (Amoxicillin). Until recent years, the standard treatment for a UTI was 10 days of amoxicillin, a penicillin antibiotic, but it is now ineffective against E. coli bacteria in up to 25% of cases. A combination of amoxicillin-clavulanate (Augmentin) is sometimes given for drug-resistant infections. Amoxicillin or Augmentin may be useful for UTIs caused by Gram-positive organisms, including Enterococcus species and S. saprophyticus.
Cephalosporins. Antibiotics known as cephalosporins are also alternatives for infections that do not respond to standard treatments or for special populations. They are often classed as first, second, or third generation. Cephalosporins used for treatment of UTIs include cephalexin (Keflex), cefadroxil (Duricef) cefuroxime (Ceftin),loracarbef (Lorabid), and cefixime (Suprax, among others.
Other Beta-Lactam Drugs. Other beta-lactam antibiotics have been developed. For example, pivmecillinam (a form of mecillinam), is commonly used in Europe for UTIs.
Trimethoprim-Sulfamethoxazole (TMP-SMX)

The typical treatment is a 3-day course of the combination drug trimethoprim-sulfamethoxazole, commonly called TMP-SMX (such as Bactrim, Cotrim, or Septra). A 1-day course is somewhat less effective but poses a lower risk for side effects. Longer courses (7 - 10 days) work no better than the 3-day course and have a higher rate of side effects.
TMP-SMX should not be used in patients whose infections occurred after dental work or in patients allergic to sulfa drugs. Allergic reactions can be very serious. Trimethoprim (such as Proloprim or Trimpex) is sometimes used alone in those allergic to sulfa drugs. TMP-SMX can interfere with the effectiveness of oral contraceptives. High rates of bacterial resistance to TMP-SMX exist in many parts of the United States.
Fluoroquinolones (Quinolones)

Fluoroquinolones (also simply called quinolones) are now becoming as widely used as TMP-SMX. They are the standard alternatives to TMP-SMX. Examples of quinolones include ofloxacin (Floxacin), ciprofloxacin (Cipro), norfloxacin (Noroxin), and levofloxacin (Levaquin).
Pregnant women should not take fluoroquinolone antibiotics. They also have more adverse effects in children than other antibiotics and should not be the first-line option in most situations.
Tetracyclines

Tetracyclines include doxycycline, tetracycline, and minocycline. Treatment with tetracycline or doxycycline may be used for infections that are caused by Mycoplasma or Chlamydia. Tetracyclines have unique side effects among antibiotics, including skin reactions to sunlight, possible burning in the throat, and tooth discoloration. They cannot be taken by children or pregnant women.
Aminoglycosides

Aminoglycosides (gentamicin, tobramycin, amikacin) are given by injection for very serious bacterial infections. They can be given only in combination with other antibiotics. Gentamicin is the most commonly used aminoglycoside for severe UTIs. They can have very serious side effects, including damage to hearing, sense of balance, and kidneys.
Other Antibiotics Used Specifically for UTIs

Nitrofurantoin. Nitrofurantoin (Furadantin, Macrodantin) is an antibiotic that is used specifically for urinary tract infections as an alternative to TMP-SMX or a quinolone. Unlike many of the other drugs, however, it is usually taken for 7 - 10 days, even in cases of simple cystitis. It is not useful for treating kidney infections. Nitrofurantoin frequently causes stomach upset and interacts with many drugs. Other chronic or serious medical conditions may also affect its use. It should not be used in pregnant women within 1 - 2 weeks of delivery, in nursing mothers, or in those with kidney disease.
Fosfomycin. The antibiotic fosfomycin (Monurol) may be prescribed as a 1-dose treatment for women who are pregnant.
Doripenem. Doripenem (Doribax) is a new carbapenem antibiotic, which was approved in 2007 for the treatment of complicated urinary tract infections. It is given by injection.
Medications for Treating Symptoms

Although antibiotics can cure for most urinary tract infections, severe symptoms can persist for several days until treatment effectively eliminates the bacteria. A number of options are available for relieving symptoms until the antibiotics take action.
Phenazopyridine. Phenazopyridine (such as Pyridium, Uristat, Barodium, Eridium, and AZO Standard) relieves pain and burning caused by the infection. Patients should not take this medicine for more than 2 days.
Side effects include headache and stomach distress. The drug turns urine a red or orange color, which can stain fabric and be difficult to remove. Rarely, it can cause serious side effects, including shortness of breath, a bluish skin, a sudden reduction in urine output, shortness of breath, and confusion. In such cases, patients should immediately call the doctor.
Antispasm Drugs. Methenamine (such as Atrosept, Prosed, and Urised) or flavoxate (Urispas) reduce bladder spasms, which may occur with some UTIs. These drugs can have severe side effects, however, that the patient should discuss with the doctor.


NB: Nakiete Pharmacy au JD Pharmacy wana dawa nzuri kwa ajili ya UTI
 
MziziMkavu,

Habari yako mzizi mkavu,yani nashukuru sn kwa maelezo yako marefu kuhusiana na UTI mi ni mmoja wapo ninayesumbuliwa sana na ugonjwa huo but nimejifunza zaidi kupitia haya maelezo yako asante sana ubarikiwe
 
NANASI+EPO+TIKITI MAJI
Juisi ya mchangayiko wa nanasi, epo na tikitimaji huondoa mlundikano wa chumvi mwilini, husafisha kibofu cha mkojo pamoja na figo. Hii ina maana kwamba juisii hii ni kinga tosha dhidi ya magonjwa ya kibofu cha mkojo na figo.
 
Ni vigumu kusema ipi ni dawa nzuri ya UTI kati ya antibiotiki lukuki zilizopo, kwani inategemea aina ya vimelea vilivyosababisha hiyo UTI, kwa mazingira yetu, madaktari/matabibu huchagua dawa kutokana na uzoefu wa practice zao au kutokana na upatikanaji wa dawa hizo, lakini kitaalamu na kisayansi dawa madhubuti ya UTI hupatika baada ya kuotesha vijidudu hivyo kwa kuchukua sampuli ya mkojo wa mgonjwa na kujaribisha aina nyingi za dawa nje ya mwili wa mgonjwa, yaani maabara (urine culture and sensitivity test), kisha wataalamu wa maabara wanamshauri daktari aina za antibiotiki ziliyoonyeha kuua aina ya vimelea vilivyooteshwa na zilizoshindwa.
 
Leo nimepima mkojo na choo nimekutwa nina maambukizi ya urinary tract infections (UTI). Kwa kweli mwenzenu nina maumiv makali sana ya mwili na sehemu za siri. Tatzo n kwamba: nimepima hapa Marie stopes-Mwanza na gharama ya dawa nambiwa tsh 35,000 halafu vpimo sh 12,700. Nimeomba niandikiwe dawa nkatafuta kwingine hawataki, uwezo wa kulipia hzo dawa mie sina,
naomba ushauri ndugu zangu nifanyeje au nitumie dawa gani nipone mapema kwani maumivu ni makali sana sehemu za siri na choo hamna infection. I'm MALE.
 
Mmmmm!! Pole sana! Bila shaka wana Jf waliopo hapo Mwanza wanaweza wakawa na msaada zaidi! Mi nimepita2! Ntarudi baadae.
 
uti ni ugonjwa simple sana kutibiwa.unaonaje ukaenda bugando au kituo cha afya chochote ambako nina hakika gharama ni robo ya hiyo?pole sana.meanwhile kunywa maji mengi,inasaidia ku-clear kwa kiasi fulani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom