Dawa ya tofaut ya mishahara ya umma na elimu mbovu

mchaichai

JF-Expert Member
Nov 5, 2011
648
76
ni miaka takribani 50 sasa tangu taifa limepata uhuru kamili bila kuwa na hata sekta moja iliyojoofu ili hali kuna ongezeko kubwa la wataalam wanaosomeshwa na fedha za umma walipakodi..

.Mfumo wa CCM huu...kuna kila sababu ya kulaaniwa na kila mzalendo..angalia serikali moja lakini takribani kila sekta ina kiwango chake cha mshahara...elimu isiyomwezesha kuhitimu kutumia mazingira yake kuzalisha mfano watanzania wanaohitimu elimu ya darasa la saba ambao ndiyo wengi wanaishia kukua tu na kujua kusoma na kuandika kiswahili tena kwa asilimia siyo wote...form 4 hadi 6 kujua kingereza kidogo hasa cha kukariri hakuna ujuzi katika ngazi hii..hii ina maana kwamba mtu wa form 4 na 6 bila kwenda chuo ni as good as standard seven leaver kwa Tanzania....

Wakitokea kwenda chuo asilimia 80 wanaandaliwa kuwa managers(wasimamizi) na siyo wazalishaji...wale wasio na ujunzi hata kidogo ndiyo wanategemewa kulisha nchi hii yenye sifa ya kila aina ya maliasili....hii inafanya nchi hii kuonekana masikini na ombaomba wa kila kona...

Je tufanyeje kupata suluhu ya maswala haya? Je maoni ya katiba yatasaidia?je kubadilisha mfumo na kuendelea kuendesha nchi kwa propaganda za kisiasa kama ilivyo kwa miaka 50 iliyopita italeta tija? na je kustandardise mishahara kwa watumishi wote wa UMMA na viongozi wa kisiasa itasaidia kupunguza migomo ya mara kwa mara ikiwemo hii ya madaktari nayoendelea?ushauri kwa serikali ifanyeje katika kuboresha mazingira ya kazi?

NAOMBA KUWASILISHA AHSANTENI
 
Back
Top Bottom