Dawa ya Tanzania ni Taasisi na mifumo imara itakayozalisha Watu imara

Kilemakyaaro

JF-Expert Member
Jul 19, 2016
5,050
5,078
Nimekua mfuatiliaji mzuri sana wa siasa zetu, nimefuatilia pia mijadala mbalimbali hususan kuanzia mwaka 2015 mpaka majuzi tulipopatwa na Msiba wa kuondokewa na aliyekua Rais wetu.

Katika kufuatilia huko nimegundua kama Taifa imefika mahala tujikite kwenye Ujenzi wa Taifa kwa kuimarisha Taaasisi zetu( Bunge, Mahakama, Executive na Media). Uimarishaji huu sharti ujengewe misingi Imara kutoka katika Sheria mama, yaani KATIBA.

Hii itatusaidia kutuzalishia viongozi Imara watakaokua wanadhibitiwa na mfumo na ikitokea akapatikana kiongozi/viongozi wa hovyo basi nature (Mfumo) utapambana nao na kuwabwaga kabla hawajaaribu Taifa letu.

Nnachokiona sasa ktk uongozi wetu tumejikita sana kuangalia mtu(individual Person) ambapo kama kawaida binadamu sio malaika anakosea na kutokana na kuwa hatuna mifumo dhibiti, basi tunajikuta watu wa kulalamika kwa maumivu mpaka mwisho na hatimae kila siku tunaanza Upya kama wajinga.

Ukosefu wa Taasisi na Mifumo imara imezalisha Taasisi ndogondogo (vyama vya siasa na media) dhaifu na udhaifu huo umezalisha watu dhaifu wapigania tumbo na maslahi binafsi na sio Taifa.

Ripoti ya CAG imekuja na madudu kuanzia vyamani, vyama mbadala na chama tawala. Hii maana yake ni kwamba hata ikitokea tukabadili chama bado tutakua na watu wa kaliba ileile kwakua wametokana na taasisi dhaifu.

Kama Taifa tumekua tunaweka matumaini kwa watu badala ya Mifumo, kila anaekuja anaonekana afadhali lkn akiondoka ndio tunajua kua kumbe afadhali ya aliyekua kabla yake.

Mifumo Imara itationdolea waganga njaa, viongozi magoigoi, wanafiki na wazandiki ambao hawana uthubutu wa kukemea mabaya kisa tu aliyeyafanya ni wakwao, mifumo itatupa watu watakaokua wanawajibika kwetu sio kwa wanasiasa.

Ni ajabu mtu/ Waziri kila ripoti ikija inamtaja kwa mmabaya lkn hajiuzulu na hatuna namna ya kumuwajibisha na badala yake atatujibu majibu ya hovyo tu na kesho utamuona tena Bungeni.

Tukubali tu kua sasa bora kuanza upya kwa kujenga taasisi na mifumo Imara kwa kuwa Watu mashuhurui (Strong Men) wanakuja na kupita, ila Mifumo hudumu.

Kinyume chake tutakua watu wakusifia mtu na kikundi chake na kila akiondoka tutalaum tu na ipite ila tukumbuke tuna deni kubwa kwa kizazi kijacho.

Wasalaam.
 
Naunga hoja mkono.

Tujikumbushe maneno ya Rais Obama alipokuja hapa nchini mwaka 2014. "Africa needs strong institutions rather than strong men".
 
Kwa jinsi tabia zetu zilivyo Watanzania, kunasehemu kama Taifa tumemkosea MUNGU.
 
CCM wanaamini Katiba Mpya itakuja kuondoa ulaji wao ndio maana hawaitaki, tatizo kwangu bora wangekuwa na akili za kusimamia hizo rasilimali za taifa, badala yake hawana hizo akili kila mwaka ripoti za CAG ni madudu tu, mbaya zaidi wahusika hawachukuliwi hatua zozote za kisheria wanaachwa waendelee kubakia serikalini matokeo yake ni muendelezo wa madudu tu, sijui tutaendelea kushangaa hii trend mpaka lini.
 
Back
Top Bottom