Dawa ya Sagamba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dawa ya Sagamba

Discussion in 'JF Doctor' started by Kichankuli, May 7, 2009.

 1. Kichankuli

  Kichankuli JF-Expert Member

  #1
  May 7, 2009
  Joined: Dec 18, 2008
  Messages: 847
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  JF DR. au mdau mwingine yeyote wa JF tafadhali nieleze iwapo kuna dawa inayoweza kutibu Sagamba (mipasuko ya kwenye visigino)
   
 2. Kichankuli

  Kichankuli JF-Expert Member

  #2
  May 8, 2009
  Joined: Dec 18, 2008
  Messages: 847
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  Wadau mbona kimya, hakuna mwenye kujua habari za tiba ya sagamba?
   
 3. I

  Ikena JF-Expert Member

  #3
  May 8, 2009
  Joined: Oct 24, 2007
  Messages: 479
  Likes Received: 246
  Trophy Points: 60
  Kuna dawa ya cream inaitwa Fungnil ni nzuri sana, ni maalum kwa fungasi na hayo magaga/sagamba.
   
 4. Kichankuli

  Kichankuli JF-Expert Member

  #4
  May 8, 2009
  Joined: Dec 18, 2008
  Messages: 847
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  Ikena nashukuru ngoja nikaisakanye madukani
   
 5. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #5
  May 8, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,466
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 0
  unaongelea sagamba kama ugonjwa au sagamba kama hali inayoweza kumpata mtu asiyeangalia miguu yake?
  Ili kuzuia sagamba nakushauri uwe na kawaida ya kuiloweka miguu yako kwenye maji ya uvuguvugu na sabuni kisha uisugue na jiwe au brashi ( pumice stone).Kisha kausha na upake mafuta.Pia pendelea kulala na soksi baada ya kupaka mafuta hadi hali iwe ya kuridhisha.Endelea kuwa unaisugua unapooga.Miguu yako itabaki soft bila mipasuko.
   
 6. D

  Dina JF-Expert Member

  #6
  May 8, 2009
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 2,779
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Pia upunguze 'rate' ya kuvaa viatu vya wazi...tatizo linakuja kama pia una matatizo ya fungus za vidoleni, manake nazo zinachachamaa ukikazana kuzifunika!
   
 7. I

  Ikena JF-Expert Member

  #7
  May 8, 2009
  Joined: Oct 24, 2007
  Messages: 479
  Likes Received: 246
  Trophy Points: 60
  Mafanikio mema,, ila uhakikishe unaipata dawa yenyewe kwani maduka mengi wakikosa dawa hiyo wanakutafutia substute.

  Boksi la dawa hiyo ni kama la zambarau na picha ya mtu mwenye sagamba nyayoni imeonyeshwa hali kadhalika mtu mwenye fungus/ukurutu pia imeonyeshwa.
   
 8. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #8
  May 8, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,235
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Mi nijuavyo hali ile inatokana na mara nyingi kutoijali sana miguu.

  Mimi nikiwa nimekulia vijijini, nilishambuliwa sana na hayo makenya, lakini ilikuwa inatokana na kutovaa viatu almost muda wote, na ile hali ya baridi sana. Mara baada ya kuhamia mijini na kuanza kuvaa viatu fully, hali hiyo ilipotea na haijarudi tena.

  Unless kama hiyo hali ni special ambayo kwa mimi sijaizowea. Fuata ushauri wa hiyo cream kama ulivyoshauriwa na dada WoS.
   
 9. Kichankuli

  Kichankuli JF-Expert Member

  #9
  May 8, 2009
  Joined: Dec 18, 2008
  Messages: 847
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  Hili tatizo analo mai waifu, na sidhani kuwa linasababishwa na kutoijali miguu/visigino, kwani mwenyewe huwa anaviosha na kuvisugua kwelikwweli. Labda kwa suala la kutovaa viatu vya kufunika visigino hilo naweza kubaliana nalo kwani mara nyingi huvaa viatu vya wazi.

  Lakini kitu kingine ambacho kinanitatiza ni kuwa, hata mimi nimekulia kijijini na nakumbuka kutovaa viatu vya kufunika nadhani hadi nilipojiunga na kidato cha kwanza lakini sijawahi kupasuka visigino. Katika familia yetu Mama na dada zangu wawili walikuwa na tatizo la kupasuka visigino. Lakini nakumbuka pia kuna dada mmoja tulikuwa tunasomo shule moja ya msingi, yeye visigino vyake vilikuwa vinatoka unyevunyevu mwingi kiasi kwamba tulikuwa tunamshangaa kweli. Je kuna uwezekano wa upasukaji wa visigino kuwa ni suala la kibayolojia kama ilivyo kuota ndevu, sharafa au gadern love?
   
 10. Kichankuli

  Kichankuli JF-Expert Member

  #10
  May 8, 2009
  Joined: Dec 18, 2008
  Messages: 847
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  Nimejaribu kupitapita kwenye maduka ya hapa Dodoma nimekosa, na kuna duka moja walitaka kunichomekea kunipa mbadala kwa mantiki kuwa zote ni anti-fungus. Unaweza kunieleda jina la duka (Dar) ambalo naweza kwenda straight nikapata hiyo dawa tafadhal
   
 11. Himawari

  Himawari JF-Expert Member

  #11
  May 8, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 2,075
  Likes Received: 566
  Trophy Points: 280
  Mafuta ya vaselini ni dawa tosha. Safisha miguu vuzuri paka mafuta ya vaselini. Tumia mafuta ya vaselini kila wakati na tatizo la sagamba halitajirudia tena.
   
 12. I

  Ikena JF-Expert Member

  #12
  May 11, 2009
  Joined: Oct 24, 2007
  Messages: 479
  Likes Received: 246
  Trophy Points: 60

  Mkuu hilo ni swala la kurithi na wakati mwingine ni la mazingira.
  Mi ni wa huko dom, ila kwasasa sipo dom. Nami nilikuanayo hayo masagamba kabla ya kutoka dom.Miezi ya kwanza baada ya kutoka dom ni nilianza kuona mabadiliko katika nyayo zangu na hasa baada ya kutumia fungnil.
  Siku hizi situmii kabisa na visigino vimekua kama vya mtoto mchanga.
  Nikienda maeneo flan flan na hasa huko dom sagamba zinarudi upya.
  So actually ni hali ya hewa au tuseme mazingira yanachangia sana. Nauhakika kuna mazingira ambayo favourable kwa waifu wako.

  Endelea kumshauri kuosha miguu, kupaka mafuta na kuvaa viatu vya kufunika kama ulivyoshauriwa na wanajamii.
   
Loading...