Dawa ya Punda Mvivu

X-PASTER

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
11,607
1,818
Nakumbuka mwaka mmoja nilitembelea kule Pangani. Nikashuhudia kisa kimoja cha jamaa na Punda wake, ambaye inasemekana Punda wake alikuwa mvivu sana. Jamaa alikuwa anamtumia Punda wake katika kubebea nazi kutoka shamba kwenda Nyumbani kwake, tatizo la yule punda ni kuwa alikuwa mvivu sana akibeba mzigo anaenda taratibu mno.

Jamaa akawa anachukia sana kwa tabia ya Punda yule, akaamua kumtafutia dawa, sasa katika kuulizia ulizia kwa watu, akakutana na Baniani, baada ya kumwelezea matatizo ya Punda wake, yule Baniani akampa pilipili za aina mbili tofauti akamwabiwa hii fupi ni speed 40 na hii ndefu ni mara mbili yake yaani ni speed 80. Ukiona Punda wako anakwenda kivivu, usipate tabu wewe mpake Punda matakoni uone.

Jamaa akafurahi sana akaona dawa si ndio hii. Akaenda akambebesha mizigo kibao kuliko kawaida, Punda kama kawaida yake akawa anakwenda tartiiiiibu.... Yule jamaa akaamua kumpaka yule Punda pilipili ya speed 40. Punda akaongeza mwendo, yaani ni mbio, jamaa kila akimfukuza hampati, akajisemea moyoni ahaa.... hisiwe tabu ngoja na mimi nijipake hii speed 80. Kweli bwana jamaa kwa ukali wa pilipili alikimbia akampita hadi punda. Watu walimkuta nyumbani amefika kabla ya punda anajipepea na feni m4t4koni...!!!
 
Back
Top Bottom