Dawa Ya Mchungaji Ambilikile Mwasapile a.k.a Babu. Je Ni Ulaghai? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dawa Ya Mchungaji Ambilikile Mwasapile a.k.a Babu. Je Ni Ulaghai?

Discussion in 'JF Doctor' started by X-PASTER, Apr 7, 2011.

 1. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #1
  Apr 7, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Dawa Ya Mchungaji Ambilikile Mwasapile a.k.a Babu. Je Ni Ulaghai?  Asalaam Aleikum, Aman iwe nanyi...!

  Wana JF, habari za miangaiko ya kila siku... Poleni na majukumu na miangaiko ya hapa na pale.

  Leo nami nimeonelea kwa mara ya kwanza kutoa mchango wangu, kuhusiana na kadhia hii inayo endelea uko Loliondo. Japokuwa baadhi ya haya yaliyomo humu, nimesha yaeleza kwenye thread nyingine, lakini nimeonelea kuyaunganisha hapa, ili niweze kueleweka kwa watakao penda kuelewa.

  Hizi habari za Mchungaji Mstaafu Ambilikile Mwasapile wa kijiji cha Samunge wilayani Loliondo, ambaye anajulikana kwa jina la umaarufu kama babu, zimechukuwa nafasi kubwa sana kwenye vichwa vya Watanzania wengi.

  Mimi ni mmoja wa wengi ambao wanafuatilia habari zake kwa kina na ukaribu...! Huyu babu kwenye mahojiano yake... ameelezea kuwa yeye amepata mahono kutokwa kwa Mwenyezi Mungu na dawa yake inaponyesha baada ya siku zisizo pungua saba.

  Kusema ukweli tumesikia mengi sana, kutoka kwa wadau mbali mbali...! Lakini kitu cha ajabu ni kwamba, wengi ambao wamekunywa hiyo dawa, hatuwasikii tena kwenda hospitalini au zahanati ya karibu, ili kupima na kujua afya zao zinaendeleaje? Yaani zimekuwa simulizi za mdomoni tu, kuwa fulani kapona na wengine wamediliki hata kujitaja wao binafsi kuwa wamepona na hali hawana uthibitisho wa kitabibu kuonyesha kuwa wamepona.

  Vile vile kuna wadau wanao mtete, huyu mzee, ambaye mimi namwita Kinjeketile Ngwale wa karne hii ya 22. Wale walio soma historia ya vita vya majimaji, wanajuwa kilicho wapata wale wote waliokunywa na kujipaka ile dawa ya Kinjeketile... Dawa ambayo ilikuwa ni mchanganyiko wa mbegu za Mbarika na Mtama... Matokeo yake kila mtu anajuwa kilicho wapata wazee wetu wale. Ingawa hata Kinjeketile naye kuyapa uzito madai yake alidai kuwa ameoteshwa na Mwenyezi Mungu.

  Ajabu ni kwamba, leo hii ni miaka 100 imepita tangia vita vile vipiganwe. Na hivi sasa tupo karne ya Sayansi na Technolojia, bado wapo watu wenye kuamini yale yale yalio wapata wazee wetu karne moja nyuma. Hawa wadau kila kukicha wao wanakuja sera mpya mpya za kumtete huyu mchungaji mstaafu...!

  Matokeo ya hii dawa ya huyu mchungaji, yameanza kuonekana kwa wengi, kuna ambao wamezidiwa na maradhi wakakimbizwa hospitalini na wale wasio na bahati wamepoteza maisha. Kwangu mimi naona kuwa ni uzembe na ujinga wa makusudi, ulio sababishwa na wao kuacha kula dawa za hospitalini wakitarajia miujiza ya uponyaji kutoka kwa huyu mzee.

  Licha ya watu kupoteza uhai, bado kuna ambao wanamtetea...! Utawasikia wakisema "Oooh babu hazuii kifo..!" Ndio tunajuwa kuwa hakuna mtu mwenye uwezo wa kuzuiya vifo... Hata hao mitume tunao waamini kwenye dini zetu, ziwe za jadi au hizi ambazo tuna ziita za kimapokeo, hawakuwa na uwezo wa kuzuiya watu wasife... Lakini kama vifo vinatokana na uzembe na ujinga wa makusudi kwa kuacha kula dawa zenye kukuongezea uhai, mnataka tuwaeleweje?

  Sasa tunasikia tena kuwa watu wasiache kula dawa zao, japokuwa wamepata kunywa dawa za Kinjeketile Ngwale wa karne hii ya ishirini na mbili... Kulikoni tena?

  Hao waliokwisha kunywa dawa mpaka leo hatusikii wakisema kuwa wamekwenda kupima... Wanaogopa kitu gani...!? Utawasikia wakijisifia kuwa wamepona kwa kujiangalia kwenye kioo...! Na hali maradhi yanawatafuna ndani kwa ndani...!

  Mwisho hao watetezi watakuja na utetezi mpya kuwa wale wote ambao hawakupona hawana imani ndio maana dawa ya babu Kinjeketile haikufanyakazi...!

  Hivi hao waathirika waliozidiwa baada ya kuto endelea na dawa zao za mahospitalini, watajisikiaje watakapo simangwa kwa kushutumiwa kuwa hawakupona kwa kuwa hawana imani...! Je hamuoni ni kuwazidishia maradhi zaidi?

  Hivi anayetakiwa kuwa na imani hapa ni nani mgonjwa au babu kinje...! Yeye si ndiye aliye dai kuwa kaoteshwa na mungu na dawa yake inaponyesha maradhi yote...!? Hivi Mwenyezi Mungu anapoleta Neema huwa anachaguwa wa kumpa? Au huwa anawapa hata wale wasio muamini?

  Hivi ni kweli uwezi kupona mpaka huwe na imani ...!? Inaingia akilini kweli?

  Mbona tunasoma kwenye maandiko ya biblia kuwa kuna watu waliponywa na wala hawakuwa na hiyo imani...! Na wengine walifufuliwa...! Je wale walioponywa na kufufuliwa na Nabii Elisha...! Walikuwa na imani? tena wengine walifufuka kwa kugusa mifupa ya manabii tu.

  Jamani tuwache kushabikia vitu ambavyo haviwezekani kwenye karne hii... karne ambayo mwenyezi Mungu ametujaalia utaalam wa kutengeneza madawa ya kutibu maradhi mbali mbali...! Kinacho wafanya watu wasitumie hiyo miujiza ya kunywa dawa mahospitalini ni kitu gani kama si ulimbukeni na kutafuta njia za mkato ni nini...!? Kwani hizo dawa za mahospitalini hazina baraka za Mwenyezi Mungu!?

  Hivi tunamwambia nini Mwenyezi Mungu siku ya hukumu... Na hali ametupa akili na tunashindwa kuitumia... Hivi ni neema gani zaidi ya kutumia akili zako na kutambua kuwa hapo Lolly hakuna uponyaji zaidi ya kuwapumbaza watu kwa kivuli cha imani!?

  Mara nyingi ni vigumu sana kushindana na wajinga, watakushinda tu...! Watakusumbua na hoja zao za kijinga na kukushusha mpaka ufikie level yao...!
  Kisha watajiona kuwa wao ni mahodari na kuanza kujisifia na hali wanaona kuwa ujinga wao umepelekea maangamizi ya ndugu, marafiki na jamaa zao wenyewe...!

  Ukiwauliza haya mambo yamekuwaje... Hawakosi hoja hata siku moja...! Utawasikia wakisema "Aaah wale, wale wamekosa imani ndio maana hawakupona, unatakiwa umkiri bwana kwanza..."

  Jamani hivi hakuna viongozi wa dini ambao wamefariki kwa maradhi ya kutibika, lakini wakafariki? Je hawakuwa na imani!?

  Msije sema kuwa hatukuwaonya na kuwatahadharisha na hatari iliyoko mbele yenu...! Sisi tunawapenda zaidi ya hao ambao wanao wapeleka kwenye mdomo wa mauti, uko mnakoenda hakuna uponyaji, bali kuna mauwaji...!

  Nawapa pole sana ndugu, jamaa na marafiki wote walio athirika kwa njia moja au nyingine, nawataka wasikate tamaa na kujiona kuwa imani zao ni haba, bali wanapaswa kurejea kutumia dawa zao za mahospitali, na kufuata masharti ya madaktari na wauguzi wao...!

  Namuomba Mwenyezi Mungu awarejeshee afya na siha njema wale wote walio taabika kwenda uko Lolly, ili waweze kurejea kwenye furaha kama zamani... Na wale wenye kutumia dawa za HIV na kisukari basi wasiwache kutumia dawa zao kwa matumaini hewa na ya kilaghai, waswahili tuna msemo wetu mmoja kuwa "Kupotea njia ndio kujua njia", basi msikate tamaa, rejeeni dawa zenu ili muendelee na maisha, sisi wote tunawapenda.

  Nawatakia siku njema.

  Amani ya Mwenyezi Mungu hiwe nanyi.
   
 2. E

  ELLET Senior Member

  #2
  Apr 8, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 111
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watu wengi walienda kwa Babu kwa imani kwamba ametumwa na Mungu wa mbinguni muumba wa mbingu na inchi, labda ungetusaidia kweli alitumwa na Mungu? otherwise, ata shetani(mungu wa dunia hi) naye anaponya!
   
 3. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #3
  Apr 8, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Mhhh...................

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. cartura

  cartura JF-Expert Member

  #4
  Apr 8, 2011
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 3,049
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Yatazungumzwa mengi sana kuhusu Babu wa Loliondo, but at the end of the day uamuzi wa nini cha kufanya unabaki kuwa wa mnywa kikombe mwenyewe na matatizo aliyonayo...
   
 5. N

  Ngambili Ngenja Member

  #5
  Apr 8, 2011
  Joined: Mar 1, 2008
  Messages: 44
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 15
  'but at the end of the day uamuzi wa nini cha kufanya unabaki kuwa wa mnywa kikombe mwenyewe na matatizo aliyonayo...'

  Nadhani hii ndo final conclusion!
   
 6. Baba Mtu

  Baba Mtu JF-Expert Member

  #6
  Apr 8, 2011
  Joined: Aug 28, 2008
  Messages: 881
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Mtani sikonge naona sasa ushakuwa mwenyeji hapa dar/pwani, maana nawe unaiujuwa mipasho. Haya nambie ni nani huyo atakayekufa na hicho kijiba cha roho??!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. L

  LAT JF-Expert Member

  #7
  Apr 8, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  naunga mkono
   
 8. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #8
  Apr 8, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,869
  Likes Received: 6,608
  Trophy Points: 280
  wengi waliotoka Loliondo ndo kwanza wamenyongea.....Babu msanii tu!
   
 9. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #9
  Apr 8, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  mkuu inawezekana aliambiwa na Mungu kweli amponye mtu mmoja tu yule wa kwanza na si vinginevyo. Alipewa kama ufunuo kwa ajili ya mtu mmoja na si kwa style anayoendelea kuifanya. anachofanya ni ulangai na kujitafutia pensheni, inasikitisha baadhi ya maaskofu wa KKKT ni kama wameigeuza kuwa doctrine ya kanisa.
   
 10. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #10
  Apr 8, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Hee mkuu una uswazi furani?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. g

  guta Senior Member

  #11
  Apr 8, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 179
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mimi ningependa sana kama kuna mtu hapa JF alikwenda kwa babu na akapata kikombe, alikuwa anaumwa na vyeti vya hospital anavyo na sasa amepima tena kaonekana kapona kabisa atuletee. Pia kama mtu hajapona afanye vivyo hivyo. Tukipata watu kumi hivi tutajua ukweli uko wapi.
   
 12. s

  seniorita JF-Expert Member

  #12
  Apr 8, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 674
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mungu ataweka kila kazi nuruni.....
   
 13. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #13
  Apr 8, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Je, pia inawezekana aliambiwe atoe bure na kwa sababu ya hali ngumu ya maisha akaanza kutoza pesa na kudai Mungu alimwamuru na bei ya dawa zake?

  tusijidangaye wapendwa, Mungu wa kweli haponyi namna hiyo ya samunge


  hakuna aliyepona, sasa utapata wapi vyeti vinavyothibitisha uponyaji?

  kweli jeshi lote lililoenda samunge hadi leo wakiwemo wanaJf wote hawa, tumekosa hata ushuhuda mmoja tu wa kuaminika? mbali na hadithi tu za fulani kapona?
   
 14. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #14
  Apr 8, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  mi nlchoshuhudia ni wa2 kuzdiwa na nmeshuhudia kati ya hao waliozdiwa wa 5 kat yao walipoteza maisha( RIP WOTE) kuna k2 bdo knanchanganya na cjakielewa vzr. Kwa nini waliopata dawa ya babu wanaona nafuu wk2 za mwanzo then baada ya 2wks wanazdiwa mara 10 ya mwanzo? Nna ushahd cz nmewashuhudia wengi. Mungu wabariki waTZ.
   
 15. Pawaga

  Pawaga JF-Expert Member

  #15
  Apr 8, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 1,247
  Likes Received: 686
  Trophy Points: 280
  ndugu,kuna m2 mmoja cmkumbuki ni nani alikuja na ku2eleza kuwa alienda na hajapona pia aka2pa na ushahidi wa baadhi ya ndugu na jamaa zake ambao hawakupona pia,. Labda 2pate ambae amepona...
   
 16. WAKUNJOMBE

  WAKUNJOMBE JF-Expert Member

  #16
  Apr 8, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 251
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  nikweli.........mimi kama mimi...sitetei upande wowote ila naamini anaye mpinga babu waloliondo huyo ni mzima yaani haumwi......

  pia kwahapa kiwandani kwetu watu kama saba wemeenda kati ya hao mmoja alifariki baada tu ya kupata kikombe ila wngine wote wazima kabisa (according to doctor frola wahapa kiwandani) nawanendelea na kazi nzito...tufauti na mwanzo walikuwa wamepewa kazi simple simple tokana na matatizo yao...
   
 17. Mahai

  Mahai JF-Expert Member

  #17
  Apr 8, 2011
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 351
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Watu wanashindwa kuelewa kuwa siku dawa ya UKIMWI ikipatikana dunia yote itageuka upside down. Itakuwa ni habari moja kubwa sana kati ya habari zilizowahi kuvunja rekodi humu duniani. Si Tanzania tu peke yake bali the whole world will be in shock.
   
 18. Mahai

  Mahai JF-Expert Member

  #18
  Apr 8, 2011
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 351
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Halafu mnasema mnatakiwa kuwa na imani ya kwenda kupona kwa kinjekitile ngwale...
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. howard

  howard Senior Member

  #19
  Apr 8, 2011
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 188
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  jamani sikilizeni clouds fm jumapili kipindi njia panda kuna dada anashuhudia tena alikwenda kupima kwa hiyo atakuwa na cheti atahojiwa jumapili hiyo alikuwa na ngoma
   
 20. khayanda

  khayanda JF-Expert Member

  #20
  Apr 9, 2011
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 248
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kuna mangapi tumeyapokea bila kuuliza???? Mwenzetu unaonekana una gonjwa ila unasita, kanywe kikombe halafu upinge kuwa haifanyi kazi. :love::love:
   
Loading...