Ndugu wana JF,
Nimekuwa nikisumbuliwa na mba (dandruff) za kichwani (scalp) kwa muda mrefu sasa na nimetumia dawa kila aina bila mafanikio. Nilianza kwa kupaka mafuta ya Whitefield lakini sikuona mabadiliko. Kisha nikameza vidonge aina ya grasiofulvin bado sikuona ahueni yoyote. Baadaye nikashauriwa kumeza vidonge aina ya ketokenazole, baada ya kushauriwa na daktari kwamba hivi vidonge ni vikali kuliko grasiofulvin nilivyotumia mwanzo. Bado tatizo liliendelea kuwepo, tena safari hii likazidi kuwa sugu zaidihata ukiwa mbali ukinitazama kichwani utadhani nimepaka ungahii ni kwa sababu ya ukoko wa mba unaochomoza kutoka kwenye ngozi ya kichwa (scalp).
Baada ya kuona tatizo limezidi ikabidi nimuone daktari wa magonjwa ya ngozi, ambapo huyu daktari alinitengenezea dawa kali kwa kuchanganya alcohol na dawa fulani ya mba. Sambamba na hii dawa aliniandikia dawa ya ketakonazole shampoo ambayo niliipaka kwa muda usiopungua mwaka mmoja. Nilitumia hadi dawa ikasiha laki bado tatizo liko palepale.
Hivi karibuni nimerudi tena hospitali daktari akaniandikia vidonge. Nilipogundua kwamba vidonge alivyoniandikia ni glusiofulvin (vidonge ambavyo vilishindwa kunitibu awali), nilivitupa vidonge hivyo jalalani. Sasa hivi nanyoa nywele kila baada ya wiki moja, tofauti na awali ambavyo nilikuwa nanyoa kila baada ya wiki mbili. Hii hali imenichanganya sana. Sijui nifanyeje. Niliwahi kwenda hadi hospitali ya St Benard kule Kariakoo nikachomwa dawa yenye mchangayiko wa salicylic acid lakini sikupata ahueni yoyote.
Wandugu, naomba mnisaidie. Anyefahamu tatizo hili naweza kuliondoaje au daktari anayeweza kulitibu naomba anielekeze. Natanguliza shukrani.
Piga namba hii nikupe ufumbuzi wa tatizo lako halafu utakuja kutoa ushuhuda 0718 754694
Hiyo movt nimeitafuta madukani sijaipata hapa Iringa!
Si umeona wahanga ni wengi mkuu? Ungeitoa tu hiyo dawa hapa maana watu wanakwambia wamepaka Sulphur mpaka wakanuka ila mba umo tu!
Pole sana ndugu yangu tumia diproson jipake kichwa kizima muda wa wiki tatu utanijulisha
Badili vinyoleo au saloon unayonyolea pia vifaa vya bafuni kama chana, vikopo vya sabuni, na vikorokoro vingine tupa; hao wadudu watakuwa wapo maeneo hayo hata dawa ikianza kuuwa wanaingia wapya utadunda mpaka utajiachia ila siku ukihamishiwa mkoa mwingine utajiona ghafla unapona
Ukiona hyo dawa uliyoelekezwa nayo inadunda,tumia mafuta ya nazi yanayoitwa
'MINARA',yanapatikana ktk maduka ya kawaida,yamenisaidia sana na mimi nilikuwa kama wewe mkuu,sasa hv nikinyoa kichwa ni kisafiiii,yanauzwa buku tu
View attachment 117852
cc tpaul Amavubi
Hayo mimi yamenisaidia sana kwani mara ya kwanza kugundua nina mba ilikuwa 1999 wamenisumbua hadi mwaka baada ya kubadilisha mafuta ya kupaka kichwani na kuanza kupaka MOVT.
Hilo kopo dogo huwa nanunua tsh1000 tu. Sasa hata nina amani kabla ya hapo nilkuwa naona aibu kwenda saloon kunyoa.
Shukrani zangu zimwendee dada mmoja mmiliki wa saloon ya kiume dar, ndio alienishauri hayo mafuta
hayo hapo Preta
asanteni, leo nimeingia chaka kdg niliuliza movt nikapewa sabuni, kumbe ni mafuta...nitayatafuta
Kweli hii movit imeonesha ndio tiba ya Mba sugu ya kichwa. Naanza kuamini nimeteseka kama mtoa mada.
Kuna movit ya njano kutoka Uganda ina sulphur, hakuna kitu pale Utapata harufu tu.
Ni pm namba ya huyo dada wa saloon aliyeshauri hii Dawa nimtumie hata BUKU kwa kweli.
Asante sana mkuu, ila mafuta ya nazi nilipaka sana hadi yakadunda. Labda hizi dandruff za kwangu ni chronic sana. Nimeenda hadi kwa dr bingwa wa ngozi kule Hindu Mandal akanitengenezea dawa maabara, nikapaka weeeee, wapi!!!!!!!!!!!! Nimeanza kupaka RADIANT, naona maendeleo yanatia moyo. Ngoja niendelee na dozi hii tuone itamifikisha wapi. Nashukuru sana kwa ushauri mujarabu.
Wewe nenda kwenye madukA ya yavipodozi utayapata ni ya blue na yana picha ya msichAna badae kidogo nitakuwekea picha
Jina lake la biashara ni RADIANT. Movt ni kampuni inayotengeneza hayo mafuta---jina la mafuta ni RADIANT, kampuni inayotengeneza mafuta hayo ipo Kampala, Uganda. Mafuta hayo ni very common, huwezi kuyakosa kwenye duka la vipodozi. Tangu nianze kuyatumia nimeona great improvement. Kama una tatizo kama langu, yatafute yatakusaidia sana. Bado muda kidogo nije kutoa ushuhuda hapa.