Mba kichwani (Dandruff): Fahamu Chanzo, tiba na jinsi ya kuepukana nazo

Nyoa nywele zote yaani fresh ya unga, au para! Au dongo, au lami. Then nenda Pharmacy nunua dawa inaitwa Sonaderm. Paka 1x2 kila baada ya kuoga asbh na jioni. Hakikisha unakausha kichwa vzr na usipake mafuta kichwa kabla au baada ya kupaka dawa.
 
Hbr za majukumu wadau,nimekuwa nikisumbuliwa sana na mba kichwani hata nywele zinapokuwa fupi nimehangaika kutafuta tiba bila mafanikio,naombeni Msaada na ushauri wenu
wewe huwa unapona ila tu unaajiambukiza tena.
Kuchangia kofia, kitana/chanuo, provers, na kupitia saluni zisizozingatia usafi.

Dawa, kuna mdau kashauri utumie sonaderm hapo juu, tumia hiyo ioa ongeza na vidonge vya griseofulvin kidonge cha 500mg kunywa mara 2 kwa siku kwa mwezi mzima.
 
naomba mtu anayejua mafuta yanayoondoa mba za kichwani
mba wa kichwani ni matokeo ya uchafu tuanzie hapo kama una mba wewe ni mchafu. ikubali kwanza iyo hali kisha anza upya nyoa nywele zote kisha usioge kichwani na sabuni ya kipande mfano; imperial ,protex, mo-soaps na sabuni zote zinazoacha mabaki kwenye matundu ya ngozi ya kichwa bali uoshe nywele na sabuni za maji alimahalufu shampoo hutajutia kwakufwata nilichokwambia nina miaka 3 sijawai pata mba wala kujikuna kichwani
 
Tafuta castor oil na tee tree essential oil
Castor oil 3teaspoon na 2-3 drops tea tree essential oil

Utafurahia result
 
RICH MK,
Mba kichwani au kuwashwa kichwa si uchafu kwa kila mtu. Kuna watu wanaosha kila siku na bado kichwani hakueleweki. Wakati mwingine matatizo ya mba au kuwashwa ni kutokana kuwa na ngozi kavu kichwani. Try to moisturise your scalp regularly inaondoa hizo shida.
 
Mkuu na mba za ngozi unaweza kutumia dawa gani?
Mkuu kama hizo mba zimekuwa kubwa/sugu sana unaweza kutumia dawa ya vidonge inaitwa Gresiofulvin sambamba na dawa ya kupaka inayoitwa Whitefield. Lakini ningkushauri uonane na daktari kwanza ili akushauri kwanza kabla ya kuanza matibabu.
 
Dah hakika. Nimefuatilia uzi mwanzo mwisho. Ngoja nikajaribu hizi tiba maana nilishakata tamaa ya kupona MBA nilihisi labda ni inheritance.
 
Mimi too 2012 Dandruff inaniadhibu ..natumia sulphur 8 mpaka nimekua mtumwa was hayo mafuta.

Nikiikosa kichwa kinakauka na kuwasha kichizi......

Dah.
 
Wakuu, dawa za ukweli za mba ni hizo nilizoweka hapo juu: Terbifin na Beprosalic ointment. Baada ya kusumbuka kwa miaka mingi, dawa hizo zilinipa suluhisho.
Tunashukuru chief kwa mrejesho huu, maana si mchezo uzi tangu 2013 suruhisho umepata 2018 lakini hukuchoka kutupa mrejesho kwasababu ni kweli tunasumbuliwa wengi na tatizo hilo

Na vipi hizi dawa lazima zitumiwe kwa pamoja au unaweza tumia mojawapo? Natanguliza shukrani zangu
 
Tunashukuru chief kwa mrejesho huu, maana si mchezo uzi tangu 2013 suruhisho umepata 2018 lakini hukuchoka kutupa mrejesho kwasababu ni kweli tunasumbuliwa wengi na tatizo hilo

Na vipi hizi dawa lazima zitumiwe kwa pamoja au unaweza tumia mojawapo? Natanguliza shukrani zangu
Asante kwa shukrani mkuu. Dawa hizi lazima ziende sambamba maana moja inadhibiti ndani na nyingine inadhibiti nje ya mwili.
 
Mkuu kama hizo mba zimekuwa kubwa/sugu sana unaweza kutumia dawa ya vidonge inaitwa Gresiofulvin sambamba na dawa ya kupaka inayoitwa Whitefield. Lakini ningkushauri uonane na daktari kwanza ili akushauri kwanza kabla ya kuanza matibabu.
Ndugu yangu hiyo dozi ulitumia kwa muda gani? Mie nimetumia siku 20 lakini hakuna nafuu. Naomba muungozo ndugu yangu japo kuwa dawa zenyewe bei kweli kweli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo sasa itakubidi umuone daktari bingwa wa ngozi mkuu. Kama upo Dar nenda pale Aghakan Hospital ukamuone Profesa Mgonda atakusaidia mkuu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom