Mba kichwani (Dandruff): Fahamu Chanzo, tiba na jinsi ya kuepukana nazo

Habari ya wakati huu, kama kichwa kinavyojieleza nasumbuliwa na hili tatizo kwa muda sasa bila kujua sababu halisi na tiba kamili ya hili tatizo mwanzoni nilihisi ni maji kwani maji tunayotumia ni yana chumvi sana na sababu nyingine kadha wa kadha kwa wale ambao mnalielewa vizuri hili tatizo na tiba yake naomba kushare nanyi ili nipate chochote,na ikiwezekana niondokane kabisa na kadhia hii.
Nawasilisha
 
Kila baada ya kutoka kuoga kama unanywele ndefu kidogo, jitahidi kuwa na utaratibu wa kupaka mafuta na kuchana nywele hata kwa kitana kidogo, itakusaidia kuondokana na tatizo hilo.

Kwa kawaida hii husababishwa sana na wanaume wengi kutokupenda kupaka mafuta ya nywele kichwani na hivyo kufanya ngozi kuwa ngumu na inapofikia ule muda wake wa kuondoa ngozi nzee na kuweka mpya inakuwa haitoki kwa wakati na unaruhusu accumulation ya dead skin kichwani kitu kinachokuwa kinaongeza uchafu na muwasho kichwani.

Thnx
 
Kibiti1,
Kwa hiyo tiba ni kupaka mafuta kichwani? Sisi tulio na aleji na mafuta ya nywele vipara vinatuhusu
 
Kwa hiyo tiba ni kupaka mafuta kichwani? Sisi tulio na aleji na mafuta ya nywele vipara vinatuhusu
Mafuta yapo ya aina nyingi, tafuta mafuta yenye ingredient zinazofit nywele zako, ila kama ishu ni kutokupenda mafuta, jitahidi usiwe na nywele ndefu na uwe unazitana kila utokapo kuoga.

Mafuta yanafanya kazi ya kuirainisha ngozi, hivyo hata ngozi iliyozeeka inatoka kirahisi na kuacha ngozi nzuri pia inalinda ngozi kutokupata muipasuko ambayo inaweza kupenyeza wadudu waharibifu tatizo likawa kubwa zaidi.
 
tpaul,
Vipi mkuu tpaul ulipona hili tatizo baada ya kutumia hayo mafuta uliyoambiwa na Remote maana hata mimi nina tatizo hili mwaka wa 10 sasa na nimejaribu kila mafuta lakini bado. Ila hayo ya Movt sijajaribu, mtupe mrejesho mlioyatumia.
 
Vipi mkuu tpaul ulipona hili tatizo baada ya kutumia hayo mafuta uliyoambiwa na Remote maana hata mimi nina tatizo hili mwaka wa 10 sasa na nimejaribu kila mafuta lakini bado. Ila hayo ya Movt sijajaribu, mtupe mrejesho mlioyatumia.
Pole sana mkuu. Hili tatizo hata mm limenisumbua kwa muda mrefu sana pamoja na kupaka kila aina ya mafuta yakiwamo hayo ya MOVIT. Mafuta ya movit sio kwa ajili ya tiba bali ni kwa ajili ya kinga na urembo kwa akina mama (yame-contain a little amount of sulphur ambayo haiwezi kutibu mba). Ukiona mtu amepaka haya mafuta amepona, basi huyo hakuwa na mba ila harara tu.

Baada ya kuteseka na mba za kichwani (dandruff) kwa muda mrefu, hatimaye nimepata tiba kutoka Hospitali/Clinic ya Doctor's Plaza iliyopo Kinondoni Morocco, jirani na makao makuu ya Airtel. Ukifika Airtel, elekea upande wa Mashariki sambamba na barabara ya kuelekea Posta, vuka Furaha Medical Centre, kisha vuka hilo ghorofa jipya unaloliona hapo mbele, kwa mbele kidogo utaona ghorofa fupi ina maandishi yameandikwa LANCET LABORATORIES...ndani ya jengo hili (Second Floor) ndimo ilimo Clinic ya Doctor's Plaza inayofanya kazi chini ya mwavuli wa LANCET LABORATORIES yenye makao makuu Afrika Kusini.

Siku nilipoenda pale sikumkuta daktari wa ngozi lakini niliomba kuonana na daktari wa kawaida ambaye alini-prescribe dawa ya kupaka inaitwa BEPROSALIC OINTMENT na vidonge vya kumeza vinaitwa TERBIFIN. Hizi dawa zimefanikiwa kuponya tatizo langu lililonisumbua kwa zaidi ya miaka 20!

N.B: Beprosalic ointment ni dawa muhimu sana na haipatikani kwenye maduka ya dawa ya kienyeji. Kwenye maduka ya kienyeji utauziwa Beprosalic cream ambayo haina uwezo wa kutibu kama ointment. Na wafamasia wengi hawajishughulishi kuzinagtia hilo, kwa hiyo unapaswa kuwa makini wewe mwenyewe mnunuzi.
 
Dawa za dandruff nilizotaja hapo juu hizi hapa:
20180316_100821.jpg
20180316_095855.jpg
20180316_095844.jpg
 
tpaul tupe mrejesho.. ni kweli umepona?? hiyo hali haijarejea tena maana kuna dawa nyingine unapaka zinasaidia ndan ya miezi miwili afu mziki unaanza tena
Wakuu, dawa za ukweli za mba ni hizo nilizoweka hapo juu: Terbifin na Beprosalic ointment. Baada ya kusumbuka kwa miaka mingi, dawa hizo zilinipa suluhisho.
 
Habari wajuvi,

Nikichana nywele kichwani hua panatoa vumbi nilizani labda ni wingi Wa nywele kichwani hivyo basi nikamua kuachana na ufugaji Wa nywele nyingi na kuanza kutumia aina mabalimbali za mafuta yakiwemo mafuta ya Nazi lakini sijaona mabadiliko yoyote.

kama kuna yeyote anayejua jinsi ya kuondoa tatizo hili msaada tafadhali
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom