Dawa ya mba sugu za kichwani (Dandruff)

Uzzi

Uzzi

Member
Joined
Dec 5, 2016
Messages
21
Points
45
Uzzi

Uzzi

Member
Joined Dec 5, 2016
21 45
yanapatikana wapi mkuu? unaweza ukatupa picha yake? kuna mafuta ya sulphur yapo kwenye lichupa fulani hivi nilipaka hadi yakadunda. ukiyapaka mafuta yale kisha ukaoga kichwa unahisi kinakuwa kikavuuu...si ndio hayo mkuu?
Brother tatizo bongo hatuna dawa. Kuna shampoo iliyosaidia watu wengi duniani inaitwa Nizoral a-d. Ni nzuri Sana ILA Tanzania haipatikani
 
ZAGANZA

ZAGANZA

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2014
Messages
515
Points
500
ZAGANZA

ZAGANZA

JF-Expert Member
Joined Jul 15, 2014
515 500
Mba ni maeneo yenye mabaka yanayoletwa na fangasi ,ambao hushambulia ngozi, hivyo ngozi hubadilika rangi yake na kuwa na rangi hafifu au inayoonekana zaidi (kama ni mtu mwenye rangi ya maji ya kunde basi ngozi iliyoathiriwa hubadilika na kuwa nyeupe au nyeusi sana.
Kuna Natura clay, watu wengi imewaponya. Kwa kuwa wengi mshatumia gharama kujitibu, mi ntawapa nusu dozi BURE, ukiona progress utakuja malizia dozi na kulipia.Dozi yote haizidi tzs 5,000/-.
Mussa
Mtaalam wa Afya ya ngozi
0713-039875
 
Mwanga Lutila

Mwanga Lutila

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2016
Messages
2,953
Points
2,000
Mwanga Lutila

Mwanga Lutila

JF-Expert Member
Joined Nov 10, 2016
2,953 2,000
Ndugu wana JF,

Nimekuwa nikisumbuliwa na mba (dandruff) za kichwani (scalp) kwa muda mrefu sasa na nimetumia dawa kila aina bila mafanikio. Nilianza kwa kupaka mafuta ya Whitefield lakini sikuona mabadiliko. Kisha nikameza vidonge aina ya grasiofulvin bado sikuona ahueni yoyote. Baadaye nikashauriwa kumeza vidonge aina ya ketoconazole, baada ya kushauriwa na daktari kwamba hivi vidonge ni vikali kuliko grasiofulvin nilivyotumia mwanzo. Bado tatizo liliendelea kuwepo, tena safari hii likazidi kuwa sugu zaidi—hata ukiwa mbali ukinitazama kichwani utadhani nimepaka unga—hii ni kwa sababu ya ukoko wa mba unaochomoza kutoka kwenye ngozi ya kichwa (scalp).

Baada ya kuona tatizo limezidi ikabidi nimuone daktari wa magonjwa ya ngozi, ambapo huyu daktari alinitengenezea dawa kali kwa kuchanganya alcohol na dawa fulani ya mba. Sambamba na hii dawa aliniandikia dawa ya ketoconazole shampoo ambayo niliipaka kwa muda usiopungua mwaka mmoja. Nilitumia hadi dawa ikasiha laki bado tatizo liko palepale.

Hivi karibuni nimerudi tena hospitali daktari akaniandikia vidonge. Nilipogundua kwamba vidonge alivyoniandikia ni glusiofulvin (vidonge ambavyo vilishindwa kunitibu awali), nilivitupa vidonge hivyo jalalani. Sasa hivi nanyoa nywele kila baada ya wiki moja, tofauti na awali ambavyo nilikuwa nanyoa kila baada ya wiki mbili. Hii hali imenichanganya sana. Sijui nifanyeje. Niliwahi kwenda hadi hospitali ya St Benard kule Kariakoo nikachomwa dawa yenye mchangayiko wa salicylic acid lakini sikupata ahueni yoyote.

Wandugu, naomba mnisaidie. Anayefahamu tatizo hili naweza kuliondoaje au daktari anayeweza kulitibu naomba anielekeze. Natanguliza shukrani.
Vipi mkuu tpaul ulipona hili tatizo baada ya kutumia hayo mafuta uliyoambiwa na Remote maana hata mimi nina tatizo hili mwaka wa 10 sasa na nimejaribu kila mafuta lakini bado. Ila hayo ya Movt sijajaribu, mtupe mrejesho mlioyatumia.
 
B

balyambalola

Member
Joined
Dec 12, 2016
Messages
5
Points
45
B

balyambalola

Member
Joined Dec 12, 2016
5 45
Kama plan A imeshindikana ingia plan B dawa za kienyeji za kunywa huku ukiendelea kupaka hiyo movit sulphur ya njano
 
B

balyambalola

Member
Joined
Dec 12, 2016
Messages
5
Points
45
B

balyambalola

Member
Joined Dec 12, 2016
5 45
View attachment 117852
cc tpaul Amavubi
Hayo mimi yamenisaidia sana kwani mara ya kwanza kugundua nina mba ilikuwa 1999 wamenisumbua hadi mwaka baada ya kubadilisha mafuta ya kupaka kichwani na kuanza kupaka MOVT.
Hilo kopo dogo huwa nanunua tsh1000 tu. Sasa hata nina amani kabla ya hapo nilkuwa naona aibu kwenda saloon kunyoa.

Shukrani zangu zimwendee dada mmoja mmiliki wa saloon ya kiume dar, ndio alienishauri hayo mafuta

hayo hapo Preta
Mbona hiyo ni jelly!!!! Movit tunayoisemea ni ya njano ina na sulphur
 
tpaul

tpaul

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2008
Messages
15,585
Points
2,000
tpaul

tpaul

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2008
15,585 2,000
Vipi mkuu tpaul ulipona hili tatizo baada ya kutumia hayo mafuta uliyoambiwa na Remote maana hata mimi nina tatizo hili mwaka wa 10 sasa na nimejaribu kila mafuta lakini bado. Ila hayo ya Movt sijajaribu, mtupe mrejesho mlioyatumia.
Pole sana mkuu. Hili tatizo hata mm limenisumbua kwa muda mrefu sana pamoja na kupaka kila aina ya mafuta yakiwamo hayo ya MOVIT. Mafuta ya movit sio kwa ajili ya tiba bali ni kwa ajili ya kinga na urembo kwa akina mama (yame-contain a little amount of sulphur ambayo haiwezi kutibu mba). Ukiona mtu amepaka haya mafuta amepona, basi huyo hakuwa na mba ila harara tu.

Baada ya kuteseka na mba za kichwani (dandruff) kwa muda mrefu, hatimaye nimepata tiba kutoka Hospitali/Clinic ya Doctor's Plaza iliyopo Kinondoni Morocco, jirani na makao makuu ya Airtel. Ukifika Airtel, elekea upande wa Mashariki sambamba na barabara ya kuelekea Posta, vuka Furaha Medical Centre, kisha vuka hilo ghorofa jipya unaloliona hapo mbele, kwa mbele kidogo utaona ghorofa fupi ina maandishi yameandikwa LANCET LABORATORIES...ndani ya jengo hili (Second Floor) ndimo ilimo Clinic ya Doctor's Plaza inayofanya kazi chini ya mwavuli wa LANCET LABORATORIES yenye makao makuu Afrika Kusini.

Siku nilipoenda pale sikumkuta daktari wa ngozi lakini niliomba kuonana na daktari wa kawaida ambaye alini-prescribe dawa ya kupaka inaitwa BEPROSALIC OINTMENT na vidonge vya kumeza vinaitwa TERBIFIN. Hizi dawa zimefanikiwa kuponya tatizo langu lililonisumbua kwa zaidi ya miaka 20!

N.B: Beprosalic ointment ni dawa muhimu sana na haipatikani kwenye maduka ya dawa ya kienyeji. Kwenye maduka ya kienyeji utauziwa Beprosalic cream ambayo haina uwezo wa kutibu kama ointment. Na wafamasia wengi hawajishughulishi kuzinagtia hilo, kwa hiyo unapaswa kuwa makini wewe mwenyewe mnunuzi.
 
Mwanga Lutila

Mwanga Lutila

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2016
Messages
2,953
Points
2,000
Mwanga Lutila

Mwanga Lutila

JF-Expert Member
Joined Nov 10, 2016
2,953 2,000
Shukrani sana mkuu tpaul ngoja nichukue maelezo yako na hayo majina ya dawa nifanyie kazi.
 
W

wengiwengi

Member
Joined
Jun 13, 2014
Messages
29
Points
45
W

wengiwengi

Member
Joined Jun 13, 2014
29 45
tpaul tupe mrejesho.. ni kweli umepona?? hiyo hali haijarejea tena maana kuna dawa nyingine unapaka zinasaidia ndan ya miezi miwili afu mziki unaanza tena
 
tpaul

tpaul

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2008
Messages
15,585
Points
2,000
tpaul

tpaul

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2008
15,585 2,000
tpaul tupe mrejesho.. ni kweli umepona?? hiyo hali haijarejea tena maana kuna dawa nyingine unapaka zinasaidia ndan ya miezi miwili afu mziki unaanza tena
Wakuu, dawa za ukweli za mba ni hizo nilizoweka hapo juu: Terbifin na Beprosalic ointment. Baada ya kusumbuka kwa miaka mingi, dawa hizo zilinipa suluhisho.
 
mbomi

mbomi

Member
Joined
Mar 6, 2015
Messages
37
Points
95
mbomi

mbomi

Member
Joined Mar 6, 2015
37 95
Saga tangawiz changanya na ndiz au parachichi paka kwenye ngozi ya kichwa kaa nayo kwa muda wa nusu saa osha kichwa chako.
NB: husipake tangawiz bila kuchanganya na tunda mojawapo hapo itakusababishia maumivu.
 
Titicomb

Titicomb

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2012
Messages
5,968
Points
2,000
Titicomb

Titicomb

JF-Expert Member
Joined Jan 27, 2012
5,968 2,000
hahaaaa mkuu jaribu hayo movt... binafsi baada ya kuanza kutumia sina tena MBA
Mkuu hauna tena mba au hauonekani ule mpauko wa mba lakini kwenye ngozi na damu wapo?
 
Y

Yuyo Ahumile Shamalendi

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2018
Messages
982
Points
1,000
Y

Yuyo Ahumile Shamalendi

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2018
982 1,000
Mkuu Tpaul hio clinick inasurport bima??
 
mkurya org.

mkurya org.

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2014
Messages
1,281
Points
2,000
mkurya org.

mkurya org.

JF-Expert Member
Joined Sep 25, 2014
1,281 2,000
Wakuu, dawa za ukweli za mba ni hizo nilizoweka hapo juu: Terbifin na Beprosalic ointment. Baada ya kusumbuka kwa miaka mingi, dawa hizo zilinipa suluhisho.
Mkuu na mba za ngozi unaweza kutumia dawa gani....???
 
tpaul

tpaul

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2008
Messages
15,585
Points
2,000
tpaul

tpaul

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2008
15,585 2,000
Mkuu na mba za ngozi unaweza kutumia dawa gani....???
Mkuu kama hizo mba zimekuwa kubwa/sugu sana unaweza kutumia dawa ya vidonge inaitwa Gresiofulvin sambamba na dawa ya kupaka inayoitwa Whitefield. Lakini ningkushauri uonane na daktari kwanza ili akushauri kwanza kabla ya kuanza matibabu.
 
Mbwa Mwitj

Mbwa Mwitj

Senior Member
Joined
Mar 9, 2019
Messages
144
Points
250
Mbwa Mwitj

Mbwa Mwitj

Senior Member
Joined Mar 9, 2019
144 250
Dah hakika.. Nimefuatilia uzi mwanzo mwisho. Ngoja nikajaribu hizi tiba maana nilishakata tamaa ya kupona MBA nilihisi labda ni inheritance.
 

Forum statistics

Threads 1,325,448
Members 509,127
Posts 32,192,776
Top