Dawa ya Mba kichwani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dawa ya Mba kichwani

Discussion in 'JF Doctor' started by Mhafidhina, Jan 4, 2011.

 1. Mhafidhina

  Mhafidhina JF-Expert Member

  #1
  Jan 4, 2011
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 548
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Wanajamii natumaini hamjambo.

  Naomba mnisaidie ni dawa gani nzuri kwa ajili ya mba. NImejaribu kutumia dawa mbali mbali ikiwa ni pamoja na shampoo pamoja na kuosha nywele mara 3 kwa siku lakini bado naona mba haziiishi.

  Naomba mnisaidie ni dawa gani nzuri kwa ajili ya Mba.

  Asanteni.
   
 2. S

  Sweet Mother Member

  #2
  Jan 4, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Tumia virgin, imesaidia wengi mimi mmoja wao
   
 3. Kiraka

  Kiraka JF-Expert Member

  #3
  Jan 4, 2011
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 2,551
  Likes Received: 613
  Trophy Points: 280
  Naomba kuelewa kuna tofauti kati ya mba na haya yanayoitwa mapunye au vibarango, vishilingi?
   
 4. S

  Sweet Mother Member

  #4
  Jan 4, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Kuna tofauti
   
 5. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #5
  Jan 4, 2011
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Ni mba gani wanakusumbua vibalango, mashilingi, mapunye au mba hawa tunaopata wakati tunasuka nywele?
   
 6. Mhafidhina

  Mhafidhina JF-Expert Member

  #6
  Jan 5, 2011
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 548
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Tafadhali unaweza ukafanua hio virgin ni nini (ni dawa ya kupaka au ya kunywa) na inazwa wapi au dozi yake ikoje? Naona umekua too brief to be useful.
   
 7. Mhafidhina

  Mhafidhina JF-Expert Member

  #7
  Jan 5, 2011
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 548
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  NI kama vipele vipele hivi halafu vinauma sana. Nimejaribu shampoo mbalimbali lakini haviishi. Vinaptea kwa muda halafu vinarudi tena. Tafadhali naomba msaada wako manake vinakua kama ni mashilingi hivi na hivyo yanafanya nijisikie vibaya sana
   
 8. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #8
  Jan 5, 2011
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Mimi nakushauri bora uende uonane na daktari bingwa wa magonjwa ya ngozi. utapata ufumbuzi wa tatizo lako. Pole sana.
   
 9. f

  fimbombaya Member

  #9
  Apr 13, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 47
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  nimekuwa nikijitahidi kuwatibu bila mafanikio!naomba mnijuze tiba sahihi ya mba kichwani.
   
 10. Chipukizi

  Chipukizi JF-Expert Member

  #10
  Apr 13, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 1,972
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 180
  Inaonekana Mba ulionao wanaitaji tiba ya vidonge.Nenda Hospital Dr akupatie FULCUNAZOLE. Ukimeza 2 weeks tu utakuwa umepona
   
 11. Katibukata

  Katibukata Senior Member

  #11
  Apr 13, 2011
  Joined: Dec 27, 2007
  Messages: 183
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mimi nimetumia mafuta ya kupaka yanaitwa CONFIDENCE, yamenisaidia sana. Umeshajaribu haya?
   
 12. Mayasa

  Mayasa JF-Expert Member

  #12
  Apr 13, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 587
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nenda upatiwe vidonge Grifulvin or Fulconazole umeze mba wataisha. Mafuta ya confidence, virgin hair, sulphur pia yanasaidia.
   
 13. 124

  124 Member

  #13
  Nov 10, 2011
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wana JF naomba kama kuna yeyote anayefahamu matibabu ya mba unaotokea haswa kichwani kwa watoto wadogo. Nini chanzo chake?
   
 14. feis buku

  feis buku JF-Expert Member

  #14
  Nov 10, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 2,371
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Dawa ecxactly siijui ila jitahidi kuwaweka safi muda wote kichwa kisikue na nywele ndefu kwa kuanzia
   
 15. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #15
  Nov 10, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,975
  Likes Received: 6,613
  Trophy Points: 280
  au awanyoe ubara.kila nywele zikiota.usafi muhimu.tatizo la jamaa wa hivi watoto wao kila kitu anamuachia hg.mia
   
 16. mshihiri

  mshihiri Senior Member

  #16
  Nov 12, 2011
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 129
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  [h=2]1. MBA KICHWANI. ( DANDRUFF.) [/h][h=1]i. Ufuta. [/h] Ponda ponda majani na mizizi ya ufuta kwapamoja. Chemsha ndani ya maji halafu chuja
  Matumizi:
  Suuza nywele kwa maji hayo kilaunapomaliza kuoga jioni.
  AU

  ii. Kitunguu thaumu na siki ya tufaha (apple).
  • kitunguu thaumu 3 vikubwa
  • siki ya tufaha (apple cedar).700ml
  Ponda vizurivitunguu thaumu tia kwenye siki, koroga vizuri tia kwenye chupa ya bilauri (siplastik) weka kwenye mwanga wa jua muda wa wiki 1.
  Matumizi:
  Utajipaka kichwani hukuukisugua mara1 kila siku kwa muda wiki 1, baadae utatumia kujipaka mafuta yazeituni (olive oil), kwa muda wa wiki 1.
  iii. Ndimu au siki. Juisi ndimu au siki kijiko1cha chakula weka kwenye glasi 1 ya maji ya kawaida.
  Matumizi:
  Paka kwenye nywele baada ya saa 1 oshanywele fanya hivi wiki mara 1.
  AU HII

  [h=1]iv. Tui la nazi.[/h] Baada kuosha nywele zako vizuri,malizia kwa tui la nazi.
  AU HII

  v. Mbeguza ndimu na pilpili manga.§ mbegu za ndimu
  § pilipili manga
  Pondaponda kwa pamoja kwa kipimo sawa
  Matumizi:
  Paka dawa hii kila siku jioni.
   
 17. 124

  124 Member

  #17
  Nov 21, 2011
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu nashukuru sana kuna mabadiliko makubwa. kitunguu thaumu na siki ya tufaa imesaidia sana.
   
 18. mshihiri

  mshihiri Senior Member

  #18
  Nov 21, 2011
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 129
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  thank hii ndio faida ya jf
   
 19. bg_dg_dy

  bg_dg_dy JF-Expert Member

  #19
  Nov 21, 2011
  Joined: Feb 27, 2009
  Messages: 448
  Likes Received: 162
  Trophy Points: 60
  Tafuta mafuta yaitwayo confidence
   
 20. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #20
  Nov 22, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Maradhi ya Mba Hutokana na ngozi iliyokufa katika kichwa yaani dead cell.
  dawa zilizopo ni :

  Ndimu au limau: Kabla kwenda kukoga jisugue limau ndani ya kichwa na baadae yale maganda ya limau yatie katika maji ya kukoga yaani yawe dafi dafi halafu ukoshe kwa maji yale kwanza na baadae utumie maji yaliyo safi.

  Fenugreek kwa kiswahili inaitwa (Uwatu) lakini imekaa kama rangi yake ni ya brown imekaa kama Vijiwe jiwe vidogodogo kama kuna Hii Uwatu unachukua vijiko 2 vya chai vya fenugreek unazirowesha katika maji usiku mzima ili zipate kulainika, halafu unaziponda ponda na baadae unapakaa ndani ya kichwa na uwache kwa muda wa saa moja na baadae kuzikosha ikiwa utafanya hivi siku zote mbaa wataondoka Inshallah bila taabu yoyote.
   
Loading...