Dawa ya makundi ndani ya CCM, ni Upatanishi au Hongo ? Nani amfunge paka kengele ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dawa ya makundi ndani ya CCM, ni Upatanishi au Hongo ? Nani amfunge paka kengele ?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mag3, Sep 29, 2010.

 1. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #1
  Sep 29, 2010
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Kikundi cha kigaidi cha Mafia kina njia moja ya kunyamazisha upinzani wowote ule uwe wa ndani au wa nje kwa kutoa kinachojulikana kama an offer one cannot refuse ! Kwa tafsiri nyepesi ni kuwa ukikubaliana na masharti wanayokupa utanufaika na kubaki salama lakini ukikataa umejimaliza na hutakuwa salama wewe pamoja na familia yako.

  Hivi sasa tunasikia ndani ya CCM wako watu watatu wanazunguka wakipatanisha makundi ndani ya CCM kwa kuwapa masharti wahusika - offers they cannot refuse. Watu hao ni mgombea Uraisi kupitia CCM Jakaya Mrisho Kikwete, Mkewe Mama Salma Kikwete na mwanaye Ridhwani Kikwete.

  Kwa bahati mbaya hawa watu wana nguvu kubwa kwani hakuna wa kuwahoji hata kama matendo yao yanatia shaka, ni nje ya taratibu ama yanapingana na sheria. Si Hosea wa TAKUKURU, Tendwa wa Usajili wala Makame wa NEC ana ubavu wa kuwahoji kwa vitendo vyao wakati huu tunapoelekea Uchaguzi Mkuu.

  Matendo haya yanafanyika waziwazi na sheria zinavunjwa tukishuhudia kwa macho yetu lakini vinafumbiwa macho na mamlaka zote husika kwa sababu tu wahusika ni CCM. Je hali hii inaashiria nini kama wanaofanya hivi tutawapa tena miaka mitano ya kuendeleza huu UMAFIA - hapana mwaka huu lazima uwe wa ukombozi !
   
Loading...