Dawa ya kweli ya mwizi ni kutokuwa na kitu: mwizi wa kura, usijiandikishe wala kupiga kura

Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
11,342
6,468
Kumekuwa na malalamiko ya wizi wa kura kwenye chaguzi nyingi nchini na kwingineko duniani.

Kupiga kura kwenye uchaguzi wa viongozi wa kisiasa ni haki ya msingi ya kidemokrasia, lakini hata kutokupiga kura ni haki ya kimsingi ya kidemokrasia.

Kuna ushauri utolewa kuwa usipopiga kura hautakuwa na nafasi ya kumchagua unayemtaka ila kupiga kura sio lazima ashinde uliyempigia kura. Ushauri huu niliufuata lakini naona sio mzuri kwani katiba ipo tenge, sheria zipo tenge, hivyo ni ngumu kufahamu kama kuna 'goli la mkono' au la.

Kama kweli kuna wizi wa kura, basi ni vyema kutumia haki ya msingi ya kutokupiga kura ili kukomesha wizi wa kura. Na endapo unaamua mapema kutokupiga kura basi ni vyema kutojiandikisha kabisa hata kama kitambulisho cha kupigia kura kitakufanya upate huduma nyingine.

Kwanza sio sahihi, kwani kazi ya kadi ya kupigia kura ni utambulisho wakati wa kupigia kura.

Wakijiandikisha wachache, wakaenda kupiga kura wachache, wezi hawatapata cha kuiba.

Na huo uchache tutauona kwenye kampeni na siku ya kupiga kura ambao ni kiboko ya mwizi wa kura.

Hatutaki tena kuona akina "Akwilina" wakiondoka hapa duniani. Hatutaki tena kuona mauaji ya wanasiasa.

Hatutaki tena kuona utekaji na utesaji wa wananchi. Hatutaki kuona wanasiasa wakimiminiwa risasi kwa kutumia silaha za kivita.

Kama kweli wewe hutaki maisha haya ya kutokutendewa haki, basi tumia haki yako ya msingi ya kidemokrasia ya kutokupia kura ikiwemo kutokujiandikisha kabisa.
 
Back
Top Bottom