Dawa ya kutozeeka yapatikana. Je, Tanzania tunaihitaji?

shige2

JF-Expert Member
Oct 11, 2016
8,106
3,967
Wana jamvi nimeona nilete hoja hii ili tuone na tujadili kama hata sisi Tanzania kama dawa hii itatufaa.

Wanasayansi wamegundua njia ya kukarabati DNA inayohusika na mambo mengi mwilini. ili kuzuia UZEE wa HARAKA na hivyo kuishi miaka mingi sana.

Chembe chembe DNA hizi zinapoanza kuchoka mtu huanza kuwa mzee KIFIKRA na kuandamwa na magonjwa mengine ambayo huja kwa sababu ya age acceleration.

Majaribio yaliyofanyiwa PANYA, Kidonge hiki KILIKARABATI DNA yao katika kipindi cha wiki moja.
Chuo kikuu cha New South Wales kilichofanya pia majaribio hayo kimesema DAWA hiyo INAWEZEKANA sana.

Uzee ambao husababishwa na kuchoka kwa DNA, Chembechembe za DAMU na pia MIALE (Radiation),
Hivyo dawa hii imeonyesha matumaini na itaanza kufanyiwa MAJARIBIO kwa BINADAMU katika kipindi cha miezi 6 ijayo.

Na kuwa kwenye SOKO katika kipindi cha miaka MITATU hivi.

Kwa sababu hiyo shirika la anga za juu la Marekani NASA, linataka kuwapa ASTRONAUTS wake wanaojiandaa kwa safari ya kwenda Sayari ya Mars.

Wanadai kuwa kidonge hicho kitawazuia KUZEEKA wakiwa safarini na pia kutokana na MIALE iitwayo COSMIC radiation ambayo HUUA asilimia 5%ya CELLS katika miili yao wakiwa safarini na hivyo kusababisha CANCER kuwa tishio kubwa.

Dawa hii NAD+ booster inayoitwa NMN imeonyesha MATUMAINI makubwa sana.
Dawa hii inategemea kuwasaidia pia watumiaji wa ndege wa mara kwa mara maana huathirika na miale ya cosmic.
Ambao nao HUZEEKA ama kuugua kutokana na exposure ya mara kwa mara ya miale hiyo.
Wakitoa mfano wa safari ya ndege ya London- Singapore- Merlbourne miale yake ni mikali kama ya CHEST X-RAYS.

Japokuwa chembechembe za damu mwilini hujikarabati DNA iliyochoka UWEZO huu HUPUNGUA wakati UMRI unapoongezeka.
Hivyo kuna dalili za watu KUISHI MIAKA MINGI sana mpaka WACHOKE!

Majaribio kwa BINADAMU yataanza mwaka huu katika Brigham and Women's Hospital huko Boston.
Chanzo: Daily mail.co.uk
 
Hii ni Kinyume na Mapenzi ya Mungu!

Ipo kanuni Moja hivi inaitwa "Kanuni ya Uchakavu",Yaani "Kitu chochote kilicho katika hali asilia hakiwezi kubaki katika hali ile ile milele,Lazima mwisho wa siku ichakae",Iwe binadamu,Mnyama,Mimea,Chuma nk.Kutumia dawa ya Kutozeeka mapema ni chukizo mbele ya Bwana.

Pia hii ni kanuni ya Maumbile "Kwa waliosoma Genetics watanielewa zaidi",Inatubidi tuzeeke na baadaye tufariki.

Kwanini uogope kuzeeka?.
 
Walete ya UKIMWI kwanza hayo mengine baadae.
Dawa ya huo ugonjwa "UKIMWI" ipo.

Ukiishaelewa Prevention measures zake hatutokaa tuusikie tena.Tusipojiadhari lazima iendelee kutuua kila uchwao.

Rudisha ile avatar ya Mwanzo banaa,Ujue sijakutambua?.Hahahahaa.
 
Mkuu hizo Prevention measures ni ngumu, mzee ruksa alisema "ugonjwa ule umeingia pahala ambapo sote tunapataka, si mzee wala si kijana. SUKARI IMEINGIA SUMU".
 
Dawa yoyote inayoenda kinyume na mpango wa Mungu itaishia kuwa side effects mbaya kuliko tatizo lililolengwa kutibiwa. Mungu anatuona.!
 
Wana jamvi nimeona nilete hoja hii ili tuone na tujadili kama hata sisi Tanzania kama dawa hii itatufaa.

Wanasayansi wamegundua njia ya kukarabati DNA inayohusika na mambo mengi mwilini. ili kuzuia UZEE wa HARAKA na hivyo kuishi miaka mingi sana.

Chembe chembe DNA hizi zinapoanza kuchoka mtu huanza kuwa mzee KIFIKRA na kuandamwa na magonjwa mengine ambayo huja kwa sababu ya age acceleration.

Majaribio yaliyofanyiwa PANYA, Kidonge hiki KILIKARABATI DNA yao katika kipindi cha wiki moja.
Chuo kikuu cha New South Wales kilichofanya pia majaribio hayo kimesema DAWA hiyo INAWEZEKANA sana.

Uzee ambao husababishwa na kuchoka kwa DNA, Chembechembe za DAMU na pia MIALE (Radiation),
Hivyo dawa hii imeonyesha matumaini na itaanza kufanyiwa MAJARIBIO kwa BINADAMU katika kipindi cha miezi 6 ijayo.

Na kuwa kwenye SOKO katika kipindi cha miaka MITATU hivi.

Kwa sababu hiyo shirika la anga za juu la Marekani NASA, linataka kuwapa ASTRONAUTS wake wanaojiandaa kwa safari ya kwenda Sayari ya Mars.

Wanadai kuwa kidonge hicho kitawazuia KUZEEKA wakiwa safarini na pia kutokana na MIALE iitwayo COSMIC radiation ambayo HUUA asilimia 5%ya CELLS katika miili yao wakiwa safarini na hivyo kusababisha CANCER kuwa tishio kubwa.

Dawa hii NAD+ booster inayoitwa NMN imeonyesha MATUMAINI makubwa sana.
Dawa hii inategemea kuwasaidia pia watumiaji wa ndege wa mara kwa mara maana huathirika na miale ya cosmic.
Ambao nao HUZEEKA ama kuugua kutokana na exposure ya mara kwa mara ya miale hiyo.
Wakitoa mfano wa safari ya ndege ya London- Singapore- Merlbourne miale yake ni mikali kama ya CHEST X-RAYS.

Japokuwa chembechembe za damu mwilini hujikarabati DNA iliyochoka UWEZO huu HUPUNGUA wakati UMRI unapoongezeka.
Hivyo kuna dalili za watu KUISHI MIAKA MINGI sana mpaka WACHOKE!

Majaribio kwa BINADAMU yataanza mwaka huu katika Brigham and Women's Hospital huko Boston.
Chanzo: Daily mail.co.uk
Nilifikiri wanasema dawa ya kuzuia kufa.
 
Hiyo dawa kampakeni Bashte wa koromije.
Wakati wenzetu wanafanya RESEARCH mbalimbali. Sisi tumebaki tukiuliza VYETI vya Bashite mchana na usiku dah!
Jamani saa ngapi UTAFIKIRIA mambo yenye tija?
 
Back
Top Bottom