Dawa ya kutoa uchafu kwenye pasi

renamaizo

JF-Expert Member
Oct 17, 2014
2,118
3,004
Habari za Jumatatu WanaJamiiForums hope mpo poa.

Sasa basi nisiwachoshe kuna pasi yangu hapa nyumbani naona inataka kuniharibia nguo zangu ina uchafu mweusi kwa chini ni mgumu sana kutoka umeshaniunguzia nguo zangu mara kadhaa.

Nimejaribu kununua panadol nisigue uchafu nilitumia nguvu nying lakini uchafu uliotoka ni kidogo mno nimejaribu kuchukua kisu kuutoa lakini wapi ni mgumu mno naombeni mnipe mbinu za kisasa za kuutoa uchafu huu.

Nawasilisha.

1620906868935.png
 
Chomeka kwenye socket wash mpaka mwisho huo uchaf ulainike kabsa then chomoa ukwangue kwa kiwembe au mkaa uliopikiwa tyr unaweza kwangulia pia.

Au unaweza nyooshea kwenye unga wa dona pia.
 
Hakikisha imepata joto la kutosha then chukua steel wool (ile ya kusugulia masufulia) sugua sehemu yenye uchafu...

NB:- steel wool inamaterial yanayo pitisha joto so kuwa makini kwani unaweza ukaungua.
 
Mkuu washa pasi ipate moto wastani ili uchafu ulainike afu ichomoe kwne umeme then tumia kidonge cha panadol kukwangua ule uchafu mpka uishe. then ipukute kwa kitambaa laini.

NB: Epuka sana kutumia vitu vinavyokwangua pasi kama steel wire, kisu au msasa hio pasi pale ambapo umepasugua patakua panakuunguzia nguo yako kila siku. mwishowe utatupa hiyo pasi. Thank me later!!
 
Panadol inaondoa uchafu ila ukipasi nguo nyeupe yale mabaki ya panadol yanaibadili hiyo shati rangi.

Solution ya uhakika ya kutoa uchafu kwa pasi ni Steel wool au stili waya ya kuoshea vyombo.. iweke pasi kwa umeme ikipata joto sugua nastili waya. mission accomplish.
 
Panadol inaondoa uchafu ila ukipasi nguo nyeupe yale mabaki ya panadol yanaibadili hiyo shati rangi.

Solution ya uhakika ya kutoa uchafu kwa pasi ni Steel wool au stili waya ya kuoshea vyombo.. iweke pasi kwa umeme ikipata joto sugua nastili waya. mission accomplish.
Mkuu ukishasafisha kwa panadol ikitikata ndo unapitisha kitambaa laini unaifuta vizuri.. tena inanga'aa vizuri sana. unaweza ukawet hata kitambaa ukairinse ikawa vizuri sana.

Hayo masteel wool yanaharibu pasi.. hapa hom binti wa kazi alikua akiuunguza nguo anasugulia hizo saiv hizo pasi hata uweke moto wa wastani tu inadaka nguo balaa.

ohoooo we endelea kusugulia izo steel woool kama hutatupa hio pasi..
 
Enzi zetu pasi za mkaa tunasugua kwenye mchanga, saivi ni mwendo wa panadol dah

Nunua msasa No1500 wa maji (INDASA) sugua mikwaruzo yote iishe.
 
Kuwa na tissue za kutosha na panadol za kutosha,

washa pasi uchafu hadi uyeyuke, sugua futa hadi uishe
Sijui ulikwamia njiani?
 
Panadol inaondoa uchafu ila ukipasi nguo nyeupe yale mabaki ya panadol yanaibadili hiyo shati rangi.

Solution ya uhakika ya kutoa uchafu kwa pasi ni Steel wool au stili waya ya kuoshea vyombo.. iweke pasi kwa umeme ikipata joto sugua nastili waya. mission accomplish.
Sio kweli

mabaki ya panadol si uyafute kwa nini unayaacha?.
 
Karibu wote wameshauri panadol. Una maana hakuna njia au mbinu ya kitaalamu mbali ya hii.

Namaanisha ushauri au maelekezo ya mtengenezaji. Hakuna "Owner's manual"?
 
Tumia asprin.. Ikishayeyuka, ule uchafu usugue kwa steel wool huku ukiishika kutumia kitambaa chenye maji maji!
 
Sote tunatumia panadol

iweje kwako upate madoa sie tusipate?

You are generosity.
Umetumia research gani kusema sote?

Panadol,Cetamol, Paracetamol, asprin ni laini zinapokutana na uchafu wakati unasugua kwa pasi zinanata na ule uchafu haziutoi...napasi daily hicho kitu nime observe.
Lakini steel wool ni tofauti ni chuma unapokwangua pasi(chuma) inafanya vilevile kama unavyokwangua sufuria kuondoa ukoko/mabaki ya msosi.

Ushauri wa madobi wengi njia ya uhakika ya kutoa uchafu ktk pasi ni steel wool na hawakosi steel wool kwa meza ya kupasi.
 
Back
Top Bottom