Dawa ya kutibu ugonjwa wa Ebola yagunduliwa

MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
40,228
Points
2,000
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
40,228 2,000
UGONJWA wa Ebola umekuwa tishio wakati unapoibuka kutokana kusambaa kwa njia ya hewa na kugusana, kitu ambacho humfanya mgonjwa kutokwa damu mwilini na kufariki baada ya muda mfupi. Kutokana na kutokwa huko na damu bila kikomo pindi mtu au mnyama anapopatwa na ugonjwa huo, asilimia 90 ya wagonjwa walifariki. Virusi vya ugonjwa
huo vilianza kugunduliwa mwaka 1976 nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kusababisha mamia ya wananchi kupoteza maisha. Kutokana na madhara yake, ilisababisha hofu kwa familia ambayo ingepata mgonjwa wa Ebola kutokana na kuelewa moja kwa moja kuwa mgonjwa wao kupona ni asilimia 10 tu. Tangu wakati huo, wanasayansi wakaanza kutafuta njia za kutibu maambukizi ya ugonjwa huo au kuuzuia usitokee. Pamoja na kwamba kumekuwa na mafanikio ya kuutibu, lakini uhakika umetolewa mei 28, mwaka huu pale Jarida la Lancet nchini Uingereza, lilipoeleza matokeo ya watafiti juu ya kuanza kupatikana kwa dawa ya kubitu Ebola kwa asilimia 100. Jopo la watalam lililoongozwa na Thomas Geisbert kutoka Chuo Kikuu cha Boston, waliweza kufanya majaribio kwa kumtibu nyani kwa dawa waliyoigundua. Geisbert alisema: " Nimefanya kazi ya utafiti wa dawa ya virusi hivyo kwa muda wa miaka 23 au 24 na tulifanikiwa kupata angalau uwezo wa kuzuia maambukizi kwa asilimia 50, lakini nilishituka baada ya kugundua kuwa hatimaye tumepata tiba kamili” Mtaalam wa utafiti wa masuala ya virusi, Heinz Feldmann, ambaye amekuwa akishirikiana na Geisbert katika tafiti mbalimbali lakini sio wa Ebola, aliuita utafiti huo kama ni ‘alama’ tu ya kuelekea katika mafanikio na si tiba kamili. "Nafikiri kunahitajika kufanyika utafiti zaidi kwa kutazama virusi tofauti tofauti kama Marburg, Lassa na Crimean-Congo, kwani Viwango vyao vya kuibuka vinaonekana kutofautiana.
MAJARIBIO KWA NYANI
Dawa ambayo imegunduliwa inaitwa Tekmira Pharmaceuticals (TP), ambayo inazuia virusi vinavyosababisha Ebola kutozaliana zaidi. Jopo la wataalam likiongozwa na Geisbert liliwagawa nyani katika makundi mawili ili kujaribu dawa hiyo. Kundi la kwanza liliwekewa virusi vya Ebola, na ambapo wanaeleza kuwa waliweka mara 30,000 ya virusi zaidi ya vile vinavyohitajika katika kuua mnyama. Baada ya dakika 30, waliamua kuwadunga sindano nyani watatu kwa kuwawekea dawa hiyo. Walirudia kuwapatia dawa siku iliyofuata mpaka siku ya tano. Nyani wawili kati ya watatu walipona ingawa walionekana kuwa na dalili za ugonjwa huo . Nyani wa tatu alikufa kama njia moja ya kukosa tiba imara. "Baada ya hapo tulijiuliza na kusema, tunahitaji kuendelea zaidi kuongeza matibabu?, hivyo tuliamua kuendelea na kutoa tiba mpaka siku ya saba na wakati huu nyani wanne tuliowapatia dawa walipona na hawakuonekana na dalili zozote za Ebola na nyani ambao hawakupatiwa dawa walikufa,” anasema Pamoja na kupata mafanikio hayo, kiuhalisia ni vigumu wagonjwa wa Ebola kupata matibabu baada ya dakika 30 kama walivyofanyiwa wanyama hao, hivyo Geisbert anapanga kuendeleza utafiti zaidi. "Je, tufanye kwa dakika 24 , 48 au 72 kabla ya kuanza matibabu? Je, tukiongeza muda mrefu tunaweza kupata mafanikio ya asilimia 100 ya tiba?. Yalikuwa maswali waliyojiuliza watafiti hao. Wataalam wengine wanasema iwapo utafiti huo utafanikiwa, itabidi kufanya utafiti wa kitaalam zaidi kwa binadamu, hiyo ni kutokana na ukweli kwamba watu watakaojitolea kujaribiwa dawa hizo , watataka kuona kama dawa zina matatizo. Aidha, wataalam wanasema inawezekana utafiti huo usiwe na maana sana kutokana na virusi vya Ebola kutofautiana kutoka sehemu moja hadi nyingine. Kwa mfano, wanaeleza kuwa virusi vya Ebola vilivyoibuka Afrika ya Kati vilionekana kusambaa kwa kasi zaidi kuliko vile vilivyoibuka sehemu nyingine duniani. Lakini Feldmann anaeleza kuwa, anahofu kukosekana kwa fedha na biashara katika kuwekeza katika tafiti za kutafuta dawa za Ebola. "Binafsi naona hakuna juhudi za kina katika kushughulikia suala hili, na sababu kuu ni kwamba, hakuna fedha za kutosha kushughulikia utafiti huu,”anaeleza.
HISTORIA YA EBOLA
Jina Ebola lina asili ya Mto Ebola ulipo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Inaelezwa kuwa tukio la kuibuka kwa ugonjwa huo lilielezwa mwaka 1976 nchini humo. Nchi ya pili kwa kupata ugonjwa huo ilikuwa Sudan Magharaibi ambapo watu 602 walielezwa kuugua na watu 397 kati yao walifariki dunia. Ndiyo maana awali ulitambulika kama Ebola-Zaire(EBO-Z) na Ebola-Sudan(EBO-S). Taarifa inaeleza kuwa kiwango cha vifo kilichotokea Sudan kilikuwa asilimia 50 tofauti na asilimia 90 ya vifo vilivyotokea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Mwaka 1990, virusi vinavyofanana na Ebola viligundulika Reston, Virginia ambavyo vilielezwa kupelekwa na nyani waliosafirishwa kutoka Ufilipino na uliitwa Ebola-Reston. Matukio mengine ya Ebola yalitokea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mwaka 1995 na 2003, Gabon (1994, 1995 na 1996), na Uganda (2000). Mwaka 1994 viligundulika virusi vingine nchini Ivory Coast, vilivyoitwa EBO-CL. Kwa jumla, baadhi ya wataalam wanasema ni vigumu kutabiri ugonjwa huo kutokana na kuibuka mwaka 1976 na baadaye kutoweka hadi mwaka 1989. Wataalam wanaeleza kuwa kuna uwezekano ugonjwa huo ukaendelea kuenea zaidi katika nchi zilizo na nyani wengi hasa katika nchi za Afrika na Asia kutokana na kuonekana kuwa, nyani ndio chanzo cha ugonjwa huo.


Dawa ya kutibu ugonjwa wa Ebola yagunduliwa
 

Forum statistics

Threads 1,336,416
Members 512,614
Posts 32,538,783
Top