Dawa ya kutibu jino | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dawa ya kutibu jino

Discussion in 'JF Doctor' started by Man Ngosha, May 10, 2012.

 1. Man Ngosha

  Man Ngosha Senior Member

  #1
  May 10, 2012
  Joined: May 2, 2012
  Messages: 198
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Habari zenu wana jf,

  Mimi ninasumbuliwa na maumivu ya jino kwa muda mrefu sasa,nimevulia kwa muda mrefu tatizo hili japo wengi wananishauri niende kwa doctor nikang'oe jino!

  Je, kuna dawa yeyote ya kutibu jino bila kung'oa?Saidia mimi,nateseka sana hasa wakati huu wa baridi!

  Mbarikiwe sana.

  Nawasilisha.
   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  May 10, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Mkuu Man Ngosha najuwa upo ulaya ingawa hujatuambia upo nchi gani dawa ya jino kuuma ni kuling'owa tu hakuna ushauri wowote ule mwengine Mkuu.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. m

  mdoe mchaina Senior Member

  #3
  May 10, 2012
  Joined: Dec 1, 2011
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  unaweza kutumia kitunguu saumu kiponde ponde halafu weka kwenye jino linalouma .au vipande vya ndulele kama tatu vikate kate kisha chemsha vikisha poa kamulia limao moja na dondoshea matone matatu ya mafuta ya taa kwa kutumia unyayo wa kuku kwenye mchanganyiko wako kwenye sufuria yako .chuja vizuri weka mchanyiko weko mahala pazuri ukipoa sukutua kutwa mara tatu kwa siku saba .meno hayatakusumbua
   
 4. ldd

  ldd JF-Expert Member

  #4
  May 11, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 792
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  ng'oa tu ndo dawa pekee
   
 5. Man Ngosha

  Man Ngosha Senior Member

  #5
  May 11, 2012
  Joined: May 2, 2012
  Messages: 198
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Mimi nipo Tz yetu hii@mzizimkavu,nashukuru kwa advice zenu nzuri!!lkn ile ya kutumia ndulele nilishajaribu sema mi nilisukutua mara mojamoja kwa siku 3 tu!!wacha nijaribu hiyo mara 7,na ile ya vitunguu swaumu nitajaribu!!Baraka za Mungu ziwafunike!!
   
 6. C

  Charema Member

  #6
  May 11, 2012
  Joined: May 11, 2012
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Muone Dr Kifimbo anatibu jino bila kung'oa mimi nilishatumia dawa yake ni kweli imenitibu.
   
 7. Man Ngosha

  Man Ngosha Senior Member

  #7
  May 11, 2012
  Joined: May 2, 2012
  Messages: 198
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Dr.kifimbo anapatikana wap?@charema
   
 8. C

  Charema Member

  #8
  May 11, 2012
  Joined: May 11, 2012
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Mpigie Dr Kifimbo 0713218600/0717728100
   
 9. Man Ngosha

  Man Ngosha Senior Member

  #9
  May 11, 2012
  Joined: May 2, 2012
  Messages: 198
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Asante sana,nimempigia na amenielekeza anapopatikana!!!
   
 10. Y

  Yakuonea JF-Expert Member

  #10
  May 11, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 601
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hii dhana ya kuwa jino likiwa linauma hakuna matibabu zaidi ya kung'oa si sahihi, kung'oa mara nyingi huwa inashauriwa kama matibabu mengine yameshindikana, ukiona jino linauma sana, maumivu yanaanza yenyewe na mara nyingine linakuamsha usiku, tafsiri yake ni kuwa caries (uozo? ) umekwenda chini sana mpaka kwenye sehemu hai ya jino (pulp) ambako kuna mishipa ya fahamu (nerves ) na mishipa ya damu (blood vessels), jino liliofikia hatua hii linaweza pia kutibiwa bila kung'olewa, matibabu yake yanahitaji kuuwa mishipa ya fahamu kwenye mizizi ya jino, kwani mishipa ya fahamu ndio inayoleta maumivu, halafu linazibwa, hivyo utaendelea kuwa na jino lako ila hutosikia maumivu sababu mishipa ya fahamu imetolewa, haya matibabu kwa kitaalamu yanaitwa ROOT CANAL TREATMENT
   
 11. georgeallen

  georgeallen JF-Expert Member

  #11
  May 11, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 3,758
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Huwezi kutatua tatizo bila kujua chanzo cha Tatizo. Dawa ni kwenda kwa daktari wa meno ili aone kama limetoboka ili walizibe kitaalam(u?) au lina matatizo mengine ambayo pia yatashughulikiwa kitaalam(u?). Dawa za kienyeji ni tiba ya muda tu.
   
 12. Mahmetkid

  Mahmetkid JF-Expert Member

  #12
  May 18, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 557
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 45
  Very Good "Yakuonea" kama ni mtihani ni 100% umeshinda.
  Dawa ya jino si kung'oa, unapong'oa ni sawa na ukawa na kidonda mkononi ukaomba kukatwa mkono. Dawa ya jino unaanzia simple restoration up to root canal treatment kutegemeana na wewe mwenyewe unavyokuwa aware na mabadiliko yanayotokana na kuoza kwa jino. Nashauri unaposikia dalili za mwanzo kabisa za maumivu ya jino ni bora ukaenda kwa madaktari wa meno mapema ili upate suruhisho la tatizo lako.
  Pamoja daimaaaaa!!!!!!!!!!!!!
   
 13. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #13
  May 18, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Mtafute Dr Salma kikwete naye ni dkt wa meno.
   
 14. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #14
  May 18, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,035
  Trophy Points: 280
  hivi huu ni uganga wa kienyeji au ni nini....? yaani niweke mafuta ya taa mdomoni .....na huo unyayo wa kuku ni kwa ajili ya nini......?
  mimi pia nina tatizo hilo....naomba ndugu yangu ukipata maelekezo unielekeze tafadhali.....

   
 15. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #15
  May 18, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  watafute forever products, wana dawa ya kusukutulia meno inauzwa 13,000/- ukitumia hiyo, jina lako itakuwa historia. Kwani uko wapi tukuunganishe na hao jamaa?

  Kama uko mwanza, duka lao ni moja tu, lipo ppf gorofa ya tano karibu na mzunguko wa samaki
   
 16. Mahmetkid

  Mahmetkid JF-Expert Member

  #16
  May 18, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 557
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 45
  Dr. Salma Kikwete yupo UK now.
   
 17. Ralphryder

  Ralphryder JF-Expert Member

  #17
  May 18, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 4,588
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Teh teh teh ! we utaua watu wewe!
   
 18. Mahmetkid

  Mahmetkid JF-Expert Member

  #18
  May 18, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 557
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 45
  Preta kuna dental clinic nyingi zina madaktari wazuri wa meno.
   
 19. dubu

  dubu JF-Expert Member

  #19
  May 18, 2012
  Joined: Oct 18, 2011
  Messages: 3,072
  Likes Received: 423
  Trophy Points: 180
  dawa ya jino ni kung'oa.
   
 20. Y

  Yakuonea JF-Expert Member

  #20
  May 18, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 601
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35

  Mkuu hii sio sahihi na niupotoshaji mkubwa kusema dawa ya jino ni kung'oa, nafikiri inaonyesha ni jinsi gani baadhi yetu hatuna uelewa na elimu juu ya afya ya kinywa ( oral health awareness and education). Jino ni kiungo muhimu sana kama kilivyo kiungo chochote katika mfumo wa mwili , hivyo ung'oaji wa meno si jambo linaloshauriwa kitaalamu hata kama jino linauma, kwani kuna taratibu na matibabu mengine yanaweza fanywa ukabakia na jino lako bila maumivu, ung'oaji wa memo usio na mpangilio mara nyingi husababisha madhara kwenye kinywa, mfano mpangilio mbaya wa meno kwenye kinywa (malocclusion) unaweza sababishwa na ung'oaji meno usio walazima, occlusal disharmony inaweza pia kutokea esp. When there is bilateral loss of posterior teeth, and with continued resorption of alveolar bone inaweza sababisha maumivu ya misuli ya uso (Myofacial pain), naomba tuondokane na hii dhana ya kuwa dawa ya jino ni kung'oa.
   
Loading...