Dawa ya kusafisha tumbo

Vladimir Lenin

JF-Expert Member
Jul 21, 2018
3,613
5,100
Salaam wakuu,

Hivi kuna dawa yoyote ya kusafisha tumbo/ kusababisha kuharisha?

Jirani yangu ameniomba nimshauri lakini nikatoka kapa, anadai anapata choo kwa taabu sana, nimemshauri anywe magnesium ila sina hakika kama zinasaidia. Masaada tafadhali.

Nia anataka dawa itakayomsaidia kuharisha sana.
 
Salaam wakuu, hvi kuna dawa yoyote ya kusafisha tumbo /kusababisha kuharisha?? Jirani yangu ameniomba nimshauri lkn nikatoka kapa, anadai anapata choo kwa taabu sana, nimemshauri anywe magnesium ila sina hakika kama zinasaidia. Masaada tafadhali. Nia anataka dawa itakayomsaidia kuharisha sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Atafute kati yafuatayo.

1.Mafuta ya mbono/mnyonyo/castor oil, achange ya kutosh kwenye maji glasa moja. Aweke vijiko hata vitatu

2.Atengeneze juisi ya papai

3.juic ya ukwaju

Afanye hivyo. Mambo mukide,

Akion anaendesha sana, apige glass ya maji baridi, kupunguza kasi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama kuna mtu anajua karanga pori Inapatikana wapi Naomba anijulishe nimeitafuta sana bila mafanikio
 
Atengeneze juisi ya ukwaju, iwe nzito kama uji mwepesi. Anaweza kuchanganya na asali (hata sukari) ili kupunguza uchachu , kisha anywe kama glasi mbili hivi. Baada ya kama saa moja hivi shughuli itaanza.
Aisee hii juisi nilitengeneza mwaka jana hakika ni tiba nzuri mno na inafaa sana kwa kusafisha tumbo nakumbuka nilinunua mafungu 2 ya ukwaju nikasafisha vizuri na maji ya vuguvugu kisha nikatengeneza juisi nzito ya ukwaju na nilitumia kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 6.
Nilienda chooni siku ile si mchezo
 
kuna dawa moja hivi ya kimasai ya mizizi inachanganywa na supu. ni chungu sana ila mziki wake si wa kitoto. unaweza kuharisha nje ndani. ni nzuri sana maana inakufanya uwe stebo kwenye mambo mengi.
 
kuna dawa moja hivi ya kimasai ya mizizi inachanganywa na supu. ni chungu sana ila mziki wake si wa kitoto. unaweza kuharisha nje ndani. ni nzuri sana maana inakufanya uwe stebo kwenye mambo mengi.
Hiyo nakumbuka niliinywa NATRON hiyo ni habari ingine!nadhani ni the best kuliko zote duniani.maana baada ya hapo unakuwa mwepesi km messi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom