Naomba kujuzwa dawa ya kupunguza Appetite

Wakuu mimi nakula sana, matokeo yake nina kilo 120 na nimfupi kwa hiyo niko kwenye risk ya kupata magonjwa. Ninasikia njaa kila baada ya lisaa. Nakula kitimoto kama kilo 2 na ugali sahani moja na tusker baridi 3. Milo mingine kama wali au chips ni kama nachiokoza koo tu. Vikuku vya kisasa labda viwili ndio nashiba. Kwa siku maji nakunywa kama lita 5 na ushee. Mayai asubuhi ya kuchemsaha nakula 6 na mkate mdogo mzima. Nisaidie mwenzenu sijui kwa nini hii appetite inakuwa kali hivi. Enzi hizo nikiwa nasoma walimu walinirudisha nyumbani nilikuwa hadi naiba chakula cha walimu kwa vile cha wanafunzi kilikuwa hakinitoshi. Mke wangu ananitania nitaua watoto.

Huo si Ugonjwa ni Ulafi na Utakuua kaka
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom