Dawa ya kung'atwa na nyuki, anayeijua msaada unahitajika haraka

365

JF-Expert Member
Nov 28, 2014
1,377
1,456
Jamani nimeng'atwa na nyuki usoni macho yamevimba kiasi kwamba sioni bila kuyatanua macho.

Naombeni msada kwa anayejua dawa ya kuondoa uvimbe.

Asanteni
 
Ulipo ng'atwa ilitakiwa usugue kwakutumia kitunguu maji. Ikitokea tena fanya hivyo mheshimiwa.
 
Tafuta karafuu zisage, weka maji kidogo kwenye unga uliopata kisha paka sehemu husika
 
Mbona muda si mrefu uvimbe utakwisha. Swali kidogo; hivi mbwa anang'ata na nyuki naye anang'ata? Kung'ata ni nini? Hiki kiswahili ni chetu ila mhh!
 
  • Thanks
Reactions: 365
Mkuu kama una reaction kubwa ni heri ukaenda kituo cha afya, kuna sindano waweza pata kupunguza...
 
  • Thanks
Reactions: 365
jamani nimeng'atwa na nyuki usoni
macho yamevimba kiasi kwamba sioni bila kuyatanua macho...naombeni msada kwa anayejua dawa ya kuondoa uvimbe.....

asanteni
Duu pole sana halafu umeweza kuingia JF na kupost? Sumu ya nyuki pata maziwa ya mzazi akukamulie machoni
 
pole sana ndugu.

Kupunguza maumivu chukua kitambaa kisafi na barafu au maji ya baridi.

Weka kitambaa juu ya eneo ulilong'atwa na kisha juu yake weka barafu.

Hii ni huduma ya kwanza,kwa matibabu zaidi nenda hospitali.
 
Back
Top Bottom