Dawa ya kumpa apetite mtoto | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dawa ya kumpa apetite mtoto

Discussion in 'JF Doctor' started by Parachichi, Apr 28, 2009.

 1. P

  Parachichi JF-Expert Member

  #1
  Apr 28, 2009
  Joined: Jul 22, 2008
  Messages: 517
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Wakuu polen na kazi mingi!Ee bwana mimi natafuta dawa ya mtoto mdogo wa umri wa mwaka mmoja na miezi mitatu ya kumpa apetite.Mimi mwanangu ni mvivu sana wa kula anaweza kukaa siku nzima bila kula kitu chochote.Nilijaribu kumpeleka kwa Dokta kuchek Minyoo wanasema hana minyoo wala nini ila akashauri tuwe tunamlazimishia chakula.

  Najua huku jamvini kuna wataalamu waliobobea naombeni msaada wenu wakuu.

  Naomba kuwasilisha.
   
 2. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #2
  Apr 28, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,933
  Likes Received: 2,084
  Trophy Points: 280
  Maswali machache kwanza:

  • Ulianza kumpa chakula (i.e. anything zaidi ya Maziwa ya mama au kopo-lactogen, S26 etc) akiwa na umri gani?
  • Wakati unaanza kumpa vyakula hivyo, ulikuwa unamlazimisha kula? Au likuwa napenda mwenyewe kula?
  • Ulikuwa unampa vyakula vya aina gani? Na sasa unampa vyakula gani?
  • Mtoto anapata njaa? Akiwa na njaa ana-behave vipi?
  • Nani huwa anamlisha mtoto?
   
 3. Saikosisi

  Saikosisi JF-Expert Member

  #3
  Apr 28, 2009
  Joined: May 4, 2007
  Messages: 528
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Angalia uzito wake kwenye kadi ya kliniki umekuwa ukiendaje. Kama uzito unaongezeka na uko kwenye rangi ya green ama juu zaidi maana yake mtoto anakula na kukua vizuri, mambo ya appetite itakuwa pressure zako tu (wazazi wengi huwa wana-pressure hizo unnecessarily).

  Otherwise utamlazimisha hata kama kashiba, matokeo yake ni childhood overweight/obesity ambayo iko associated na magonjwa kibao akifikia utu uzima.
   
 4. P

  Parachichi JF-Expert Member

  #4
  Apr 29, 2009
  Joined: Jul 22, 2008
  Messages: 517
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Asante sana kwa reply yako mkuu!kuhusu swali la kwanza alianza kutumia S26 na uji kidogo baada ya kuwa na umri wa miezi mitatu manake alikua analia sana usiku halali tulipoanza kumchanganyia maziwa alikua analala raha mustarehe!

  Kuhusu swali la pili alikua halazimishwi kula wala nini!alikua anakunywa uji hadi tunaogopa kumzidishia!

  Swali la tatu alikua anatumia uji wa unga wa lishe na mtori na hadi hivi sasa vyote amevikataa na tumejaribu kumbadilishia labda kinamboa lakini wapi!tumempa Cerelac wapi,maziwa ya Ng'ombe ndio hataki kusikia hata harufu yake,viazi hataki kabisaaaaaaaaaaa.

  Akiwa na njaa anakua hana raha unajua tu kuwa ana njaa.

  Msichana wa kazi ndio huwa anashinda nae home mchana na jion mama yake anaporudi frm mizunguko ya mjini ndio anamlisha.

  Asante mkuu nadhani maswali yako nimeyajibu ipasavyo.
   
 5. H

  HAZINA Member

  #5
  Sep 18, 2012
  Joined: Sep 15, 2012
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mpatie vitamin B complex , atapenda kula !
   
 6. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #6
  Sep 18, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Madogo wengi siku izi kula issue pole mkuu
   
 7. REX

  REX JF-Expert Member

  #7
  Sep 19, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 330
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kuna namna nyingine ya kuweza kuwasaidia watoto wapate hamu ya kula lakin kabla hujafanya hili angalia growth chat ya mtoto kama yupo kwenye green its ok! Kama yupo kwenye grey unamlisha sana hahitaj zaid anachokula kinamtosha na unatakiwa kupunguza na kama yupo kwenye red then tafuta
  .forever kids.ni malt vi amin ya kutafuna ambayo imeboreshwa kwa kuongeza madalanzi na mnukio wa machungwa.inafaa sana kwa wototo kuwaongezea apetite.
  .Forever bits and peaches.hii ina aloe vera na matunda ya peaches,huwasaidia watoto kupata ham ya kula na kuwakinga na maradhi mbalimbali.
   
 8. k

  kokwemage Member

  #8
  Sep 19, 2012
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 62
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  kuna dawa fulani kama sikosei inaitwa phamactin imechorwa katoto juu kanacheza mpira, nilikuwa nikimpatia mwanangu ilikuwa inasaidia sana
   
 9. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #9
  Sep 19, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Mimi wangu amepewa Multivitamins na ORS lakini yeye alikuwa anapata choo chepesi sana.

  Sasa na mimi sijaelewa mantiki ya kumpa vitamins wakati ananyonya vizuri ,mwanzo nilibisha asitumie hizo dawa lakini naona mama mtu anampa tu.
   
Loading...