Dawa ya kukomesha Malaria na Dengue plus magonjwa mengine yanayoenezwa na Mbu!

Jumong S

JF-Expert Member
Jul 3, 2013
7,312
10,492
Habari!
....Nakumbuka siku Rais Obama anakuja Tanzania mitaa yetu ya Dar ilikuwa inatoa harufu nzuri ya marashi ya dawa ya kuua mbu! Hii ilifanyika ili mgeni wetu asiugue malaria. Barabara zetu zilipigwa deki, machinga walipigwa bakora wasituaibishe kwa kwenda kwenye madirisha ya ile gari maarufu "The beast" kuanza kuuza vyupi vya mtumba kwa akina Michele ha ha haaaa!

Yes, mgeni njoo mwenyeji apone au akome! Ndugu watanzania, kwa nini bunge lisizuie ununuzi wa ndege kubwa ya bilion 270s na kuamua kuspray dawa na kupunguza mbu? Kuna nchi za wenzetu wamefanya hivyo na NO MALARIA!

Afya ya mlipa kodi ni ya muhimu sana kwani akifa hata serikali itakosa hiyo kodi ya kununua dreamers!

Ni ajabu, tunadeki barabara kisa kaja The Potus halafu akiondoka tunaendelea kuhara, kutapika na kuchafua mitaa kama kawaida!!!

Kiongozi atakumbukwa kwa kufocus kwa kipaumbele hata kimoja kitakachodumu miaka elfu na sio kudonoa donoa vipaumbele!!!

Thinking like Albert Eisten!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu umeongea kitu muhimu mno,na tatizo kubwa la sisi watanzania ni usahaulifu na ndio maana politicians wetu wameshatugeuza wapumbavu,wakati nchi inaelekea kupoteza heshima yake,Japan walikuja na mradi mkubwa sana wa kutokomeza mbu kwenye jiji letu,pesa nyingi sana za watoa kodi wa kijapani zilitolewa kwa serikali yetu katika mradi huu,kilichotokea fedha nyingi zilielekezwa kwenye personal accounts za vigogo(huku wakilindwa na wanasiasa) na matokeo yake mradi ule ulishindwa na kufa na kama kawaida yetu tumesahau,ILA umakini ungefanyika katika project ile leo suala la mbu lingekuwa hadithi za kale kwenye jiji letu,hivyo hivyo kwenye masuala mengine kama elimu(kumbuka fedha nyingi kutoka Sweden-SIDA),maji kutoka Denmark(DANIDA) etc etc,tutasubiri sana na kupata taabu mno.
 
Yes, nakumbuka kuna mradi pale Kibaha upo chini ya Prof D Gabagambi ulikuwa targeted kwa mikoa yote but wilaya nyingi walichukua dawa ila hawakuifanyia kazi na hawakulipa kabisa pesa. Nchi ngingine waliichukua na kuifanyia kazi. Sisi sijui nani katuroga. Mfadhiri kapatikana watu wanakula hela na wkt na wao Malaria inawasumbua!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom