Wiyelelee
JF-Expert Member
- Nov 9, 2012
- 1,071
- 347
Hivi karibuni, kuliibuka tetesi kwamba mwanamme na mwanamke waligandana huko Temeke Mkoa wa Salidalama baada ya kusaliti ndoa zao. Jana niliskia kwenye redio moja kwamba kuna Mganga ameibuka kwamba dawa hiyo anayo! Mimi niliposkia kwamba sasa itaanza kupatikana kiholela nimeogopa sana kwamba hali itakuaje?
Hii dawa ikianza kutumika hovyo, je itakuwa mke au mme anamkomoa mwenzake au ni kudhalilisha ndoa? Maana chukulia kama mke wangu amenigandisha na HG, wakaja watu kunishangaa pale nyumbani. Nani atadhalilika zaidi, mke wangu au mimi niliyegandisha na HG? Nadhani huko sio kumkomoa mtu bali ni kudhalilisha familia nzima. Cha ajabu, eti mwanamme anamgandisha mke wake na mtu mwingine, sio aibu hiyo?
Lazima jamii ielimike na kuachana na mambo haya ya kijinga.