Dawa ya kudhibiti ukimwi yaanza kutumika rasmi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dawa ya kudhibiti ukimwi yaanza kutumika rasmi

Discussion in 'JF Doctor' started by Saint Ivuga, May 18, 2012.

 1. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #1
  May 18, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,267
  Likes Received: 19,409
  Trophy Points: 280
  IMG_0288.JPG

  MAMLAKA ya Chakula na Dawa ya Marekani (FDA), imeidhinisha dawa ya Truvada kuwa tiba ya kuzuia kuenea kwa Virusi Vya Ukimwi (VVU).Dawa hiyo ambayo awali ilikuwa katika kundi la zile zinazotumiwa kwa ajili ya Kupunguza Makali ya VVU (ARV), imepandishwa chati wakati ambapo tayari ipo sokoni ikiuzwa kama moja ya ARV za kawaida.

  Kwa mujibu wa maelezo ya FDA, mwathirika anayetumia dawa hiyo anaweza kujamiiana na mwenza wake ambaye hana VVU bila kutumia kondomu na hatomuambikiza.

  Matokeo ya utafiti huo yaliwahi kuchapishwa kwenye gazeti hili toleo la Februari 12, mwaka huu na sasa kilichofanyika ni FDA kuidhinisha Truvada ambayo ilionyesha kufanya kazi vizuri ikilinganishwa na ARV nyingine.

  Uidhinishaji wa dawa
  Jopo la wanasayansi 22 wa FDA waliokutana Jijini Washington wiki iliyopita, walipitisha Truvada baada ya kupitia ripoti ya utafiti kuhusiana na ufanyaji kazi wa dawa za ARV.

  Wanasayansi hao waliisifu dawa hiyo baada ya kuonekana kufanya kazi vizuri kwa watu waliopo kwenye hatari ya kuambukizana VVU kwa kasi zaidi.

  Kwa namna dawa hiyo inavyofanya kazi, mwathirika akiitumia hawezi tena kumwambukiza mtu mwingine ambaye atashiriki naye tendo la ndoa bila kutumia kondomu.

  Lakini, dawa hiyo masharti yake hayatofautiani na yale ya ARV kwani mtumiaji atapaswa kuitumia maisha yake yote ili kumwekea kinga asiwaambukize wengine na yeye aishi muda mrefu.

  Kulingana na ripoti ya utafiti uliofanyika Marekani, dawa hiyo ina uwezo wa kuzuia maambukizi ya VVU hadi asilimia 90.Hata hivyo, kwa watu ambao wamekuwa wakitumia dawa holela hasa za ARV, hali imekuwa tofauti kwani Truvada imeonekana ikifanya kazi kwa kiwango cha asilimia 44 tu.

  "Hii ni ishara kwamba kuna kundi la watu ambao dawa hiyo haitafanya kazi kikamilifu kutokana na mazingira ya matumizi ya dawa holela,"ilisema sehemu ya ripoti.

  Hata hivyo, wanasayansi wanasema tatizo hilo linafanyiwa uchunguzi ili kupata njia bora ya kukabiliana na tatizo hilo.

  Faida ya Truvada
  Wataalamu wameeleza kwamba itasaidia watu ambao wana VVU lakini, hawapendi kufanya tendo la ndoa kwa kutumia kondomu."Leo ni siku ya tukio la kuwasisimua wengi katika kuzuia maambukizi ya HIV,” alisema mmoja wa wataalamu kutoka Taasisi ya kujitolea kusaidia jamii ya Fenway, Dk Kenneth Mayer ambaye alikuwa miongoni mwa wajumbe wa FDA walioipitisha dawa hiyo.

  "Ingawa (Truvada) haikuweza kuonyesha uwezo wa asilimia 100 kuzuia maambukizi ya VVU, namna inavyofanya kazi itakuwa na matokeo mazuri ya kupambana na Ukimwi duniani,” alisema Dk Mayer.

  Tahadhari
  Hata hivyo, wataalamu hao walihimiza kuwepo kwa uchunguzi zaidi wa kitafiti ili kujua kama Truvada itafanya kazi vizuri duniani kote.Mtaalamu wa Dawa kutoka Taasisi ya Taifa ya Saratani nchini Marekani (NCI), Dk Lauren Wood alilalamika akisema kuwa utafiti huo haukuzingatia matatizo ya figo.

  Alisema matatizo ya figo yamekuwa yakijitokeza kwa waathirika wengi wa Ukimwi hasa barani Afrika."Mimi sikufurahishwa sana kwa sababu utafiti huu haukuzingatia maeneo ambayo watu wengi wako kwenye hatari ya maambukizi,” alisema Dk Wood.

  Lakini, alisema utafiti uliofanyika nchini Marekani umeonyesha wazi kwamba ni dawa inayoweza kupunguza kwa kiwango kikubwa kasi ya kusambaa kwa VVU.

  Wataalamu kadha nao walisema pamoja na Truvada kupitishwa na FDA, ni lazima maelezo ya kitaalamu yatolewe kwa madaktari ili wawe na uelewa wa kutosha kuhusu matumizi yake.

  Mabingwa hao walipendekeza kwamba, wanaotumia kabla ya kuruhusiwa kutembea na wenzi wao bila kondomu lazima wachunguzwe kitaalamu ili wajulikane kama dawa iyo imewakubali au la.

  Mwanasayansi kutoka Chuo Kikuu cha Afya cha Cincinnati, Dk Judith Feinberg alikosoa ripoti ya uchunguzi akisema ilipaswa kwenda mbali zaidi katika kuchunguza madhara yanayoweza kujitokeza kwenye matumizi ya dawa hiyo.“Tusipokuwa makini katika hilo, tunaweza tukawa tumepitisha jambo ambalo litasababisha madhara zaidi kuliko faida,” alionya Dk Feinberg.


  Utafiti wa ARV
  Wanasayansi kutoka Chuo Kikuu cha Johns Hopkins ni miongoni mwa wale ambao walifanya uchunguzi juu ya ARV, kuwa moja ya dawa zinazopunguza maambukizi ya VVU.

  Watafiti hao walibainisha kuwa wale wanaotumia ARV baada ya muda fulani, huweza kushiriki tendo la ndoa bila ya kutumia kondomu na mtu ambaye hana VVU na asimwambukize kwa asilimia 95.

  Mkuu wa Mtandao wa Maabara za Kuchunguza VVU katika chuo hicho, Profesa Susan Eshleman alisema kwenye ripoti ya ugunduzi huo, wamebaini dawa za kurefusha maisha kwa waathirika wa HIV, sasa zinaweza kutumika kama sehemu ya kuzuia maambukizi.

  Profesa Eshleman alisema kwamba, mwathirika wa VVU anayetumia ARV kikamilifu, anaweza kujamiiana na mtu ambaye hana virusi bila kondomu na asimwambukize.

  “Huu ni ugunduzi wa kustajabisha,” alisema Profesa Eshleman akifafanua: “Matokeo haya yameleta mapambazuko mapya katika sayansi ya kuzuia maambukizi na inawaweka watafiti kwenye mazingira mazuri zaidi ya kupata suluhisho la kukabiliana na maradhi haya.”

  Walivyogundua
  Profesa Eshleman anasema utafiti huo walioupa jina la HPTN 052, walifanya kupitia maeneo mbalimbali ya dunia.

  Kwenye ripoti hiyo ambayo pia ilichapishwa kwenye jarida maarufu la kisayansi linaloitwa Science, watafiti hao walisema mtu anapotumia ARV, hufikia wakati fulani wingi wa virusi mwilini hupotea kiasi kwamba anakuwa karibu sawa na yule ambaye hajaambukizwa.

  “Jambo la msingi katika utafiti huu ni kwamba dawa hizi za kurefusha maisha zinapotumiwa kikamilifu, hupunguza mzigo wa virusi mwilini kwa zaidi ya mara 200. Ni sawa na kusema inapunguza hadi kufikia karibu na sifuri,” inaeleza ripoti hiyo.

  Ni katika mazingira hayo, ripoti hiyo inasema kuwa damu ya mwathirika inakuwa haina virusi na hivyo uwezekano wa kumuambukiza mpenzi wake unakuwa haupo.

  Ripoti hiyo inaeleza kuwa ARV inafanya kazi mbili, kwanza kurefusha maisha ya mwathirika kwa kupunguza virusi mwilini na pili ni kumkinga asiambukize wengine.Sifa nyingine ya ARV, alisema ni kupunguza uwezekano wa waathirika kupata ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB) kutokana na kiwango cha kinga za mwili kuongezeka
   
 2. nxon

  nxon JF-Expert Member

  #2
  May 18, 2012
  Joined: Jul 16, 2011
  Messages: 1,149
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  cost yake sasa naskia ni kama 1.4 mill
   
 3. MUSONI

  MUSONI JF-Expert Member

  #3
  May 18, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 554
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Hilo gazeti halikuwa wazi na hiyo article haiongelei bei, kwani ni dawa ambazo zipo na serikali inazitoa bure kote nchini.....!!
   
 4. Kimbori

  Kimbori JF-Expert Member

  #4
  May 18, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 2,724
  Likes Received: 347
  Trophy Points: 180
  je umesoma masharti yake? Kuhu bei je? Na je umesoma ufanisi wake? ACHA NGONO ZEMBE ILI UNUSURIKE....
   
 5. stephot

  stephot JF-Expert Member

  #5
  May 18, 2012
  Joined: Mar 1, 2012
  Messages: 5,001
  Likes Received: 2,617
  Trophy Points: 280
  Kuwa mpole usijekimbilia haraka haya mambo na matokeo yake ikawa kama wale walio kimbilia dawa za babu kule Loliondo.
   
 6. M

  Morinyo JF-Expert Member

  #6
  May 18, 2012
  Joined: Aug 26, 2011
  Messages: 2,471
  Likes Received: 460
  Trophy Points: 180
  Safari bado ni ndefu
   
 7. Tripo9

  Tripo9 JF-Expert Member

  #7
  May 18, 2012
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 2,168
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Wadhungu wanataka watumalize. Stukaaaaaaa mtanzania!

  Najaribu ku-imagine sipati picha. Namcukua Mdada nampeleka ghetto kwangu. Ananiambia "Nina ukimwi kaka angu". Namuuliza umepima lini....Ananijibu "Ngoja nikuoneshe" Anaingiza mkono kwenye pochi yake ananipa kikaratasi toka hospital kimeandikwa HIV-Positive. Halafu na mimi bila kufikiria eti navua jeans yangu na kumtandika. Nafanya hivi lakini baada ya kufuata masharti yooote ya hiyo dawa.....

  Kwanza mimi ntakua mwehu, pili akili yangu itakua kama ya maiti. Sina uhakika kama mnio utasimama kama kweli mimi ni mzima!


  My take: HII DAWA NI DANGANYA TOTO. WANATAKA KUTUUA WAZUNGU
   
 8. s

  sugi JF-Expert Member

  #8
  May 18, 2012
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,367
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 160
  Wanataka kutuua ili wafanyeje?maana kila ki2 2nawapa!
   
 9. Tripo9

  Tripo9 JF-Expert Member

  #9
  May 18, 2012
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 2,168
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Hata 0713 zetu wanazitaka!
   
 10. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #10
  May 18, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,867
  Likes Received: 6,218
  Trophy Points: 280
  mmmmh nawatakia kutumia kwema (kwa watakao tumia....)
   
 11. s

  sugi JF-Expert Member

  #11
  Sep 23, 2012
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,367
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 160
  mbona kila siku wanapelekewa hiyo 0713?
   
Loading...