Dawa ya kiungulia nini?

Nsagali

Member
Mar 4, 2011
90
12
habari wandug wana JF nina tatizo moja nikila maharage yaliyolala au yaliyoweka kwenye friji huwa nasikia kiungulia sana labda kama kuna mtu anayefahamu dawa yake huwa ni nini
 
habari wandug wana JF nina tatizo moja nikila maharage yaliyolala au yaliyoweka kwenye friji huwa nasikia kiungulia sana labda kama kuna mtu anayefahamu dawa yake huwa ni nini
Tumia vidonge vinavyoitwa Omeprazole kimoja kwa siku kwa muda wa miezi miwili mfululizo kitakwisha kabisa, hata kabla ya muda huo.
 
Kiingulia ni acidity iliyozidi kifuatia kula kitu chenye acidity. Maharage yakilala yana ferment hivyo kutengeneza more acidity state hivyo ukiyala vimengenyo vya pelipeptaid, peptaid na pepton vyenye kazi ya kuyeyusha wanga vinatoa acid nyingi ukichanganya na ile ya maharage matokeo yake ni kiungulia.

Dawa ya kiungulia ni kunywa alcalinine yoyote au base ili kuineutralize ile acid na kutengeneza chumvi na maji hivyo kutokuwa na madhara tena.

Dawa ya kawaida sana ni vidonge vya magnesium tricilicate au actal. Majivu yakichanganyika na maji yanatengeneza alcaline solution ambayo pia inaneutralize ile acid. Tatizo la majivu hakuna kipimo sahihi ukizidisha, hata ile acid ya kawaida ya kusaga chakula inakuwa neutralized hivyo chakula kinashuka kilivyo.

Usipotafuta suluhisho la kudumu kuicontrol hiyo acid tumboni kwako, inaweza kumungunya mpaka ngozi laini ta tumboni hivyo kusababisha vidonda vya tumbo vinaitwa ulcers.
 
Meza Omeprazole au Lansoprazole.

Mkuu hapo naona unataka kuua 'panya' kwa 'gobole'....Nadhani Pasco katoa ushauri mzuri zaidi, Omeprazole au Lansoprazole kwa kiungulia is too much.

Nsagali pia jaribu kuepuka hivyo vyakula vinavyokupa kiungulia, kwani unajiweka katika risk ya kupata vidonda vya tumbo.
 
habari wandug wana JF nina tatizo moja nikila maharage yaliyolala au yaliyoweka kwenye friji huwa nasikia kiungulia sana labda kama kuna mtu anayefahamu dawa yake huwa ni nini

Nsagali, mwili unakuambia unaishiwa maji.
ukifikiri kutaka kula chakula fulani au ukikiona chakula na kukifikiria kula au unapokaribia chakula mezani, tumboni kuna kitu kinaitwa 'haidrokroliki aisidi' hutentengenezwa ili kusaidia mfumo wa mmeng'enyo wa chakula. lakini haidrokroliki aisidi hii lazima ipunguzwe makali (must be neutralized) kabla hujaweka chakula mdomoni, lasivyo pamoja na mambo mengine itakusababishia kiungulia na baadaye itaanza kutoboa kuta za tumbo na kukuletea vidonda vya tumbo.

sasa, inapunguzwaje makali?, kwa kunywa maji glasi mbili kila nusu saa kabla ya chakula. humu humu kwenye JF Doctor kuna post nafikiri page ya pili ina kichwa cha habari; ''Hatunywi maji ndiyo maana tunauguwa'', isome taratibu hasa sehemu ya chini inapoanza kuelezea kwanini unywe maji nusu au robo saa kabla ya chakula.

Chini utasoma namna ya kuitambuwa kiu:

NAMNA MPYA YA KUITAMBUA KIU:

Ikiwa 'mdomo uliokauka au kiu' siyo kiashiria kikuu cha mwili kuhitaji maji, ni vipi hasa viashiria vya mwanzo na sahihi vya mwili kupungukiwa maji?.


Kwa mjibu wa dr.Batmanghelidj na maoni ya kisayansi, kuna mafungu ya aina mbili tofauti ya hisia, yanayotoa ishara ya kiu ya eneo moja au mwili mzima.



Mafungu haya yanajumuisha; Maono ya jumla ya kimawazo na zile ishara kubwa zaidi za dharura za sehemu moja au za jumla za kupungukiwa maji.

Ishara za kimawazo zinajumuisha baadhi ya viashiria vifuatavyo ambavyo vimepewa majina kama 'matatizo ya kisaikolojia', nazo ni:



  • Kujisikia umechoka (uchovu): sababu maji ndicho chanzo kikuu cha nguvu.

  • Hasira bila sababu: maji ndicho chanzo kikuu cha nguvu cha ubongo, mwili unapopungukiwa maji, ubongo unakosa nguvu kushughurika na hali mpya, mawazo na vitendo. Hasira inatokea kuwa ndiyo namna ya ubongo kujibu hali mpya zinazohitaji majibu, "Siwezi kufanya jambo hili”, sababu hauna nguvu za kutosha.

  • Woga na aibu: dr.Batmanghelidj amepata barua ya ushuhuda toka kwa mtu aliyekuwa akisumbuliwa na woga na aibu (agoraphobic) aliyejitibu kwa tiba ya maji.

  • Kujisikia umetengwa na usiyemkamilifu - huwezi kutimiza yale uyatakayo.

  • Kujisikia unaonewa.

  • Kichwa kizito uamkapo asubuhi: hakuna nguvu za kutosha kufungua mifumo ya mishipa ya fahamu.

  • Kukosa mantiki au sababu za maana unapoongea au kujibu na kukosa uvumilivu.

  • Kukosa usikivu na ufuatiriaji hasa kwa watoto na vijana; 'Uwezo wa akili wa mwanafunzi unapungua wakati kiasi cha maji mwilini kinakuwa chini ya wastani, kushuka kwa asilimia 2 tu ya uzito wa mwili sababu ya upungufu wa maji, kunapelekea matatizo ya usikivu na ufuatiriaji na uwezo mdogo wa kumbukumbu miongoni mwa wanafunzi'.

  • Kukosa usingizi mororo na kuota ndoto za kuogofya (nightmares).

  • Pumzi fupi, hatua za mwanzo za pumu, inashauriwa pia kunywa maji kabla ya michezo au mazoezi.

  • Utegemezi kwa vinywaji vya viwandani na vilevi (conditional reflex).

  • Kukata tamaa na hasira, ubongo hauna nguvu za kutosha kushughurika na matatizo mapya na unataka kuachana na mada (wacha lipite bwana, liwalo na liwe), ndiyo maana wahenga walipomwona mtu ana hasira, watampa glasi ya maji hata kiasi kidogo cha chumvi.

Kabla upungufu wa maji (dehydration) haujakudhuru kufikia hatua ya umaututi, Mwili utazitoa moja kati ya ishara hizi za pili kubwa na za dharura (emergency calls) za uhitaji wa maji mwilini zifuatazo; vidonda vya tumbo, tumbo kunyonga, kiungulia, mafuta yaliyozidi, kansa ya utumbo mdogo, kukinaishwa na chakula, na ernia.

Ishara zingine ni; Kansa, kisukari, kifua kikuu (TB), shinikizo la damu (BP), mfadhaiko (stress), matatizo ya moyo na kuzimia, magonjwa ya tumbo, magonjwa ya ngozi, magonjwa ya Ini, pumu (Asthima), mzio (Allergy), chunusi, homa, kupunguwa nguvu na kinga ya mwili, matatizo ya kina mama, magonjwa mengine ni pamoja na homa ya uti wa mgongo, kansa ya kizazi, kikohozi, kuharisha, kikundu, nyongo, matatizo ya tumbo, kupungua uzito, upungufu wa damu (anaemia), vichomi, utipwatipwa na uzito kupita kiasi, kuzeeka mapema, na ishara nyingine nyingi.

Kumbuka kutembelea: Utangulizi | maajabu ya maji
Unaweza pia kunitumia sms katika 0769779533
 
duh, asanteni sana mwenzenu hata mimi nina hilo tatizo saaaana kiasi kwamba usiku mara nyingi huwa silali kabisa hadi night kali nadhani chakula kikishameng'enywa....thanks ila kwa maji nakunywa saaaaana hasa ya moto au vuguvugu kiasi kwamba hapa ofisini watu wananuna kwamba nawamalizia maji....kwa maji nakunywa sana
 
majivu ya nini mkuu? huku mjini labda majivu ya mkaa, yanafaa pia? asante
Usinunue dawa hosp...lamba majivu utaona maajabu.
majivu ni alkaline so yanaenda ku neutralize acid....
 
habari wandug wana jf nina tatizo moja nikila maharage yaliyolala au yaliyoweka kwenye friji huwa nasikia kiungulia sana labda kama kuna mtu anayefahamu dawa yake huwa ni nini
tumia vidonge vya magnesium vitakusaidia
 
duh, asanteni sana mwenzenu hata mimi nina hilo tatizo saaaana kiasi kwamba usiku mara nyingi huwa silali kabisa hadi night kali nadhani chakula kikishameng'enywa....thanks ila kwa maji nakunywa saaaaana hasa ya moto au vuguvugu kiasi kwamba hapa ofisini watu wananuna kwamba nawamalizia maji....kwa maji nakunywa sana

safi sana Elli kwa kunywa maji saaaaaana hasa ya moto au vuguvugu. Kunywa tu maji ni kazi rahisi kila mmoja anaweza kuifanya, bali kuna formula ya kunywa maji ambayo huyafanya maji kuwa zaidi ya dawa na si tofauti.

Asilimia 94 ya damu ni maji. Kwa ujumla kila seli ndani ya miili yetu ina bahari ya maji baridi ndani yake na bahari ya maji chumvi nje yake. Afya bora inategemea uwiano mzuri wa maji ya bahari hizo mbili.



Kisha kunywa maji, maji yanapaswa kubaki ndani ya mwili masaa 2 mpaka 2 na nusu ili kuupa mwili muda wa kutosha kuyatumia maji hayo vizuri. Ikiwa inakulazimu kukojowa kabla ya masaa mawili kupita baada ya kunywa maji, juwa kabisa kuwa utaendelea tu kuuguwa, bali ukinywa maji kwa formula sahihi hakuna ugonjwa utakaouguwa kwakuwa magonjwa ni ishara za mwili kupungukiwa maji.

Ili kujifunza zaidi, unaweza kusema ni kiasi gani cha maji unakunywa kwa siku, muda gani na ni chumvi gani unayotumia. Ahsante.
 
Hata mimi nilikuwa na tatizo kama hilo ila sasa limepungua sana. Kuna wakati nilishawahi kunywa dawa zinaitwa NEXIUM (sijui kama nimepatia) ni nzuri sana ila ghali kipindi hicho tatizo lilipungua ila baada ya muda lilirudi. Ni kama mwezi sasa toka nigundue "dawa" ya rejareja. Mi ilifika kipindi nikila chochote baada ya dakika chache naanza kusikia kiungulia na kitanisumbua sana, ila sasa namshukuru Mungu shida imepungua sana sana. Huwa nikimaliza kula sinywi maji baada tu ya kumaliza, nasubiri zaidi ya lisaa limoja au zaidi ndio nakunywa maji...........na wala kiungulia hakipo kabisa. Hivyo nakushauri jaribisha hiyo.........ni haina malipo yaweza kukusaidia. (source ni mimi mwenyewe na wala sina ushauri ya kitabibu)
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom