Dawa ya kitambi hii hapa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dawa ya kitambi hii hapa

Discussion in 'JF Doctor' started by NGULI, Nov 12, 2009.

 1. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #1
  Nov 12, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Kwa wenye vitambi tu nipigieni simu mje hapa kinokleini ulizieni nguli, akina wapwa ni free of charge.
  =========================

  Kitambi ni hali ya kiafya ya mtu mnene ambapo mafuta ya ziada mwilini huongezeka eneo la tumbo kwa kiasi kikubwa.

  Mtu akiwa na kitambi anapata athari kubwa ikiwamo kupungua kwa umri. Katika karne hii, hili ni mojawapo ya tatizo kubwa la kiafya duniani. Hata hivyo, tatizo la kitambi kiafya linarekebishika.

  Katika mawazo ya kizamani na hata sasa katika baadhi ya nchi mtu akiwa na kitambi anaonekana ni tajiri.

  Tatizo la unene na vitambi litazidi kuongezeka ikiwa serikali, hususan wananchi wenyewe hawatachukua hatua za dharura na mipango madhubuti kulikabili. Tatizo hili limezidi kuwa kubwa kwa vijana wengi miaka ya hivi karibuni kwa sababu ya aina ya maisha wanayoishi (lifestyle), ambapo hula vyakula na vinywaji vyenye wanga kwa wingi (junk foods) kama vile chips, pizza, soda, bia na hawana muda wa kufanya mazoezi, na hata kufanya shughuli ambazo zitaushughulisha mwili (mazoezi, kutembea umbali mrefu, kukimbia,kubeba mizigo). Ukiwa na kitambi, maana yake ni kwamba, unakula chakula kingi mno kuliko mahitaji ya mwili wako, hivyo kupelekea chakula/nishati ambayo mwili wako hauhiitaji kubadilishwa na kuwekwa katika mafuta (fat), na kuhifadhiwa katika maeneo ya tumbo lako.

  Vitambi vina madhara mbalimbali kiafya ikiwemo

  1.Kuongeza uwezekano wa kupata magonjwa ya shinikizo la damu na magonjwa ya moyo- Tafiti zinaripoti kuwa, mtu mwenye kitambi, yuko kwenye uwezekano mkubwa zaidi wa kupata magonjwa ya moyo, mara 5-10 zaidi ya mtu asie na kitambi

  2.Kuongeza uwezekano wa kupata magonjwa ya kisukari, saratani ya tumbo; watu wenye vitambi wana uwezekano mkubwa zaidi wa kupata ugonjwa wa kisukari kuliko wale wasio na vitambi.

  3.Kupunguza uimara wa mwili (physical fitness), na kumfanya mtu awe mzembe; mtu mwenye kitambi hana uwezo mkubwa wa kuwa na mwili ambao ni imara, na wenye kuhimili shughuli zinazohitaji nguvu na pumzi kama vile kukimbia, na hivyo kumfanya awe mzembe na goigoi

  Ili kuepukana na athari hiyo watu wahakikishe wanabadili namna wanavyoishi na milo yao. Wengi wana muda mchache sana wa kutayarisha vyakula visivyo na mafuta mengi majumbani mwao, hivyo wanakula nje zaidi, yaani kwenye hoteli na migahawa na matokeo yake ni kuwa na vitambi.

  Kuna wengi wanatambua athari za tatizo la unene na vitambi, lakini hawafanyi chochote kulirekebisha, hii inatokana na ukweli kwamba idadi kubwa ya watu hawajui maana halisi ya kuwa na afya njema.

  Watu wengi, hasa vijana wamekuzwa kwa kula chipsi, mikate na vyakula vya sukari,na si mbogamboga na matunda.

  Ukweli ni kwamba watu wengi hawafanyi mazoezi ya kutosha kama ilivyokuwa zamani hivyo, watu wenye vitambi wanaongezeka kila sehemu.

  Kwa ujumla, umri wa mtu mnene mwenye kitambi huwa pungufu kwa miaka 8 had 10 ukilinganisha na mtu mwenye umbo la kawaida.

  MAGONJWA

  Hii inatokana na ukweli kwamba uzito wa mtu husababisha magonjwa ya moyo, aina fulani ya kisukari, magonjwa ambayo huua mamilioni ya watu duniani kote. Kifupi ni kuwa ukiwa na mafuta mengi mno utakuwa kwenye hatari ya kukumbwa na magonjwa kama ya kupanda kwa presha, magonjwa ya moyo, kansa. Kuongeza uzito au kunenepa kunasababisha mwili ushindwe kupata sehemu ya kutosha ya kuhifadhi mafuta na hivyo kuanza kuyatunza mafuta hayo kwenye sehemu za ndani ya mwili, kuuzunguka moyo na ndipo matatizo yanapoanza.

  USHAURI WA KUJIKINGA NA KITAMBI
  1.Hakikisha unapata walau nusu saa kila siku ya kufanya mazoezi/kutembea umbali mrefu/kukimbia hadi utokwe na jasho; hii itakusaidia kuondoa mafuta ya ziada katika mwili wako

  2.Punguza kwa kiasi kikubwa matumizi ya vyakula vyenye mafuta mengi kama vile chips, vyakula vya kukaanga; pia punguza matumizi ya sukari; na hakikisha katika mlo wako unakula matunda na mboga za majani kwa wingi (inashauriwa kuwa uwioano wa chakula cha wanga na mboga za majani/matunda uwe nusu kwa nusu katika kila mlo wako)

  3.Achana na matumizi vinywaji vyenye sukari vya viwandani kama vile soda, pia epuka matumizi ya pombe hasa bia.

  “Kitambi sio afya, ni dalili ya magonjwa, piga vita kitambi”

  SIGNATURE
   

  Attached Files:

 2. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #2
  Nov 12, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Nguli una mambo wewe attachment inaniletea mawenge
   
 3. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #3
  Nov 12, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Bonge la treak, jamaa stage ya pili lazima alipungua kilo 20 hahaha
   
 4. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #4
  Nov 12, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  Hii ni jokes Nguli, maana mie nimeishia kucheka tu.:)
   
 5. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #5
  Nov 12, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135

  Jitahidi uione nimeshawasiliana na modes waikuze, nakuomba umpelekee shemeji atoe kitambi ndoa izidi kunoga, tupunguze muda wa kutoa ushauri kwa matatizo ya ndoa.
   
 6. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #6
  Nov 12, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135

  Ni joke inayofundisha kutoa kitambi, hio stage ya mwisho ungekuwa mwanaume ungepungua kilo ishirini kwa kumuona tu.
   
 7. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #7
  Nov 12, 2009
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Ha ha ha ha aaaaaaaaaa. Very interesting
   
 8. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #8
  Nov 12, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135

  Acha ubaili gonga thanks mazee, okey ngoja nianze.
   
 9. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #9
  Nov 12, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,041
  Likes Received: 24,021
  Trophy Points: 280
  Knock! Knock! Hahaha! Mpwa bana!
   
 10. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #10
  Nov 12, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135

  Kwa wewe hii dozi ni mara 3 kwa siku Fidel80 mara 2 hali sio mbaya sana kwake, Geof mara 1 kwa siku. George Porge mara 4 tena stage 2 ya lile baunsa leusi. Burn mara 1 pia yeye ndio anaanza kuharibika.
   
 11. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #11
  Nov 12, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hahahaha mpwa hii dose ndo yenyewe lakini mm naweza nikaongeza mpaka mara 4
   
 12. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #12
  Nov 12, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135

  Kwenye stage gani no. 1 au no. 2
   
 13. Radical

  Radical JF-Expert Member

  #13
  Nov 12, 2009
  Joined: Jun 3, 2009
  Messages: 374
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Dawa ya kitambi puli tu!
   
 14. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #14
  Nov 12, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135

  Ooh! ooo! ur damaging ur health bro.
   
 15. Radical

  Radical JF-Expert Member

  #15
  Nov 12, 2009
  Joined: Jun 3, 2009
  Messages: 374
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  How?
   
 16. mabina

  mabina JF-Expert Member

  #16
  Nov 12, 2009
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 215
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35

  Oya acha utani!!!! Nit2mia e your contact nikcheki nipngze tambi, sipati raha hasa kwenye mashinduzi
   
 17. mabina

  mabina JF-Expert Member

  #17
  Nov 12, 2009
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 215
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  nitumie ur contacts nje nchukue
   
 18. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #18
  Nov 12, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135

  Mimi ni mtu maarufu sana hapa kinokleini ndio kazi yangu hii. Kwa JF PREMIUM MEMBERS ni free of charge wasiliana na MAXENCE utanipata.
   
 19. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #19
  Nov 12, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,041
  Likes Received: 24,021
  Trophy Points: 280
  Hahaha! Nimeona juhudi zako mpwa. Tutakoma tusipoangalia.
   
 20. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #20
  Nov 12, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Embu wasiliana naye na wewe uwe premium. Ila jana kapiga chuma sana sijui kama ataamka sasa ananyanyua kilo 120kg kwenye mkono pekee kifua 150kg. Anajitahidi sana mkuu wetu wa kaya.
   
Loading...