Mjadala: Ni ipi dawa ya kutibu maumivu ya jino bila kung'oa?

Man Ngosha

JF-Expert Member
May 2, 2012
219
69
Maumivu ya Jino.jpg

Habari zenu wana JF,

Mimi ninasumbuliwa na maumivu ya jino kwa muda mrefu sasa,nimevulia kwa muda mrefu tatizo hili japo wengi wananishauri niende kwa doctor nikang'oe jino!

Je, kuna dawa yeyote ya kutibu jino bila kung'oa?Saidia mimi,nateseka sana hasa wakati huu wa baridi!

Mbarikiwe sana.

Nawasilisha.
WADAU WENGINE WENYE UHITAJI WA MBADALA WA KUNGOA JINO
Salaam JF,

Nimeleta uzi huu kwenu nikijaribu kupata ushauri kwa wataalamu au watu ambao mlipitia hali hii ya maumivu makali ya meno. Je, mlitatua vp hali hizo?

Nina mdogo wangu anasumbuliwa sana, yaani mno na maumivu ya meno. Ameshawahi Kung'oa baadhi, na ameshaenda hospital na kutumia dawa kadhaa. Lakini hali hii imekuwa ikijirudia kwake.

Siku mbili zilizopita ameumwa usiku kucha bila kulala kwa maumivu ya jino/gego ambalo kwa nje hata halijatoboka, namuonea huruma kwa jinsi anavyoteseka.

Kwa mwenye kufahamu dawa, daktari, ushauri wa kadhia hii ushauri wenu ni wathamani, kabla ya kufikiria Kung'oa.

Ahsanteni
Naombeni mnijuze ni dawagani naweza2mia ili jino langu liache kuuma? Tangu juzi linanisumbua kupitakiasi na niki2mia diclopa au diclofenac linatulia maramoja na baada ya masaa machache linaanza tena. Naombeni ushauri maana nimekula diclopa mpaka nahisi zinawezaniletea madhara.
Jino linanisumbua sana kwa sasa yaan kama mnavyojua maumiv ya jino usiku hakuna usingizi wala nn utafikiri godoro lina maji. Daah! nilikua nahitaji kujua dawa ya jino tofauti na kulin'goa.


MICHANGO YA WADAU MBALIMBALI
DHANA YA JINO LINALOUMA LAZIMA LING'OLEWE SI SAHIHI
Hii dhana ya kuwa jino likiwa linauma hakuna matibabu zaidi ya kung'oa si sahihi, kung'oa mara nyingi huwa inashauriwa kama matibabu mengine yameshindikana, ukiona jino linauma sana, maumivu yanaanza yenyewe na mara nyingine linakuamsha usiku, tafsiri yake ni kuwa caries (uozo? ) umekwenda chini sana mpaka kwenye sehemu hai ya jino (pulp) ambako kuna mishipa ya fahamu (nerves ) na mishipa ya damu (blood vessels), jino liliofikia hatua hii linaweza pia kutibiwa bila kung'olewa, matibabu yake yanahitaji kuuwa mishipa ya fahamu kwenye mizizi ya jino, kwani mishipa ya fahamu ndio inayoleta maumivu, halafu linazibwa, hivyo utaendelea kuwa na jino lako ila hutosikia maumivu sababu mishipa ya fahamu imetolewa, haya matibabu kwa kitaalamu yanaitwa ROOT CANAL TREATMENT

MCHANGANYIKO HUU HUMALIZA KABISA MAUMIVU
Unasumbuliwa na tatizo la jino/meno kuuma.

Huna haja ya kung'oa jino lako.

Dawa hii ina ufanisi wa katika kuondosha na kumaliza tatizo la maumivu ya jino/meno.

Mahitaji
1. Mafuta ya karafuu/clove oil.
2. mafuta ya Nazi/coconut oil.
3. Kitunguu maji.
4. Kitunguu swaum.
5. Pilipili manga.
6.Chumvi ya mawe/unga wake

MAANDALIZI
Ponda ponda Kitunguu maji, Kitunguu swaumu,chumvi ya mawe na pilipili manga kisha changanya na mafuta na Nazi na mafuta ya karafuu kwa kiasi kidogo (robo kijiko kidogo cha chai) kisha chukua mchanganyiko huu kisha uweke juani kwa muda wa dakika 15 kisha toa juani

MATUMIZI
1.ikiwa jino lina tundu
chukua uji uji wa mchanganyiko huu kisha weka katika tundu na mafuta yake yapakaae pembezoni mwa jino linalouma.

2.ikiwa jina halina tundu
pakaa mafuta ya mchanganyiko huu pembezoni kulizunguka jino linalouma

Tumia dawa hii kutwa mara tatu kwa muda wa siku tatu jino lako litakuwa limepona kabsaa kwa .

MUHIMU:
Dawa hii inamatokeo ya haraka sana ambapo unaweza kutumia papo hapo jino likapoa,hivyo hakikisha unamaliza dozi kwa muda ulioelekezwa

Jiepushe na kunywa vinywaji vya moto sana au vya barid sana mpaka umalize dozi kwa muda uliopangwa.

Imeandaliwa na THABIT MAPANDE HERBAL CENTRE na kuchapishwa nami Nutritionist Kilindila.

Kwa mfululizo wa makala zitakazo kufundisha na kukupa elimu waweza kutufatilia kwenye page zetu;JipimeAfya
KITUNGUU SAUM, NDULELE NA MAFUTA YA TAA
Unaweza kutumia kitunguu saumu kiponde ponde halafu weka kwenye jino linalouma au vipande vya ndulele (kama tatu) vikate kate kisha chemsha vikisha poa kamulia limao moja na dondoshea matone matatu ya mafuta ya taa kwa kutumia unyayo wa kuku kwenye mchanganyiko wako kwenye sufuria yako, chuja vizuri weka mchanyiko weka mahala pazuri ukipoa sukutua kutwa mara tatu kwa siku saba, meno hayatakusumbua.
Changanya unga wa tangawizi,peke la parachichi,mdalasini na pilipili manga,tumia unga huo kupiga mswaki na kusukutua asubuhi na jioni kwa siku saba au 14 kama tatizo ni kubwa sana.
DAWA YAKUTIBU MENO NA FIZI

1) Tangawizi ya unga unachanganya pamoja na chumvi kisha unapiga mswaki. Hii inaondosha maumivu ya kuumwa na meno na kuvimba na ufizi na pia kutoa meno harufu mbovu.

2) Maji ya moto na chumvi uwe unasukutuwa kwa mara 3 au 4 kwa siku. Hii inaondosha kuvimba na ufizi na maumivu makali ya meno.

3) Kutafuna karafuu pia inasaidia kuondosha maumivu na uvimbe na harufu.

Tumia mojawapo kati ya hizo Dawa hapo juu ukisha pona uje utupe feedback.

ukiwa na matatizo yako ya kibinafsi wasiliana na mimi kwa njia ya baruwa ya pepe email Address yangu hii

hapa fewgoodman@hotmail.com
MAGOME YA MLELE/MSELE

Habari Jf,

kuna hii dawa ya mti shamba kama sijakosea mti wake unaitwa Mlele/msele.
Jinsi ya kuianda.

Toa magome ya mti huo ya chemshe kwa maji safi kisha tumia maji hayo kusukutua mdomoni kwa dakika chache.

95ab7e9b64d62800f71b59ddcc8318f2.jpg

6ed7a6363186c3c14e3a84d4a92b4e78.jpg

1a93aace32ab9c415b3c7fe843389b79.jpg
MATONE YA MAFUTA YA KARAFUU
Dawa ya Jino
Chukua dawa hizi zote ziwe za unga tena laini sana
Shabu
Makata nyeupe/ au ya bluu
changanya pamoja kipimo sawasawa kisha changanya kwenye mafuta halisi ya karafuu
MATUMIZI
Dondoshea tone moja kwenye jino lenye matatizo mara mbili kwasiku kwa muda wa siku 5-7
PANDE LA MGOMBA
Dawa za hospitali zipo japo sijawahi kuzitumia binafsi.

Ila kwa kienyeji kuna dawa moja matata sana inaitwa, mgomba.

Unachukua kipande cha mgomba, wengi wanapendelea mzizi wake au hata lile danda la ndani lenye unyevu nyevu, unaliweka kwenye moto kidogo, dhen likianza kuungua yale maji maji unayachukua unayaweka kwenye jino linalouma.

Baada ya muda, maumivu yatakata na utasahau milele yote.
 
Mkuu Man Ngosha najuwa upo ulaya ingawa hujatuambia upo nchi gani dawa ya jino kuuma ni kuling'owa tu hakuna ushauri wowote ule mwengine Mkuu.
 
Last edited by a moderator:
Unaweza kutumia kitunguu saumu kiponde ponde halafu weka kwenye jino linalouma .au vipande vya ndulele kama tatu vikate kate kisha chemsha vikisha poa kamulia limao moja na dondoshea matone matatu ya mafuta ya taa kwa kutumia unyayo wa kuku kwenye mchanganyiko wako kwenye sufuria yako, chuja vizuri weka mchanyiko weko mahala pazuri ukipoa sukutua kutwa mara tatu kwa siku saba, meno hayatakusumbua.
 
Muone Dr Kifimbo anatibu jino bila kung'oa mimi nilishatumia dawa yake ni kweli imenitibu.
 
Mkuu@Man Ngosha najuwa upo ulaya ingawa hujatuambia upo nchi gani dawa ya jino kuuma ni kuling'owa tu hakuna ushauri wowote ule mwengine Mkuu.

Hii dhana ya kuwa jino likiwa linauma hakuna matibabu zaidi ya kung'oa si sahihi, kung'oa mara nyingi huwa inashauriwa kama matibabu mengine yameshindikana, ukiona jino linauma sana, maumivu yanaanza yenyewe na mara nyingine linakuamsha usiku, tafsiri yake ni kuwa caries (uozo? ) umekwenda chini sana mpaka kwenye sehemu hai ya jino (pulp) ambako kuna mishipa ya fahamu (nerves) na mishipa ya damu (blood vessels), jino liliofikia hatua hii linaweza pia kutibiwa bila kung'olewa, matibabu yake yanahitaji kuuwa mishipa ya fahamu kwenye mizizi ya jino, kwani mishipa ya fahamu ndio inayoleta maumivu, halafu linazibwa, hivyo utaendelea kuwa na jino lako ila hutosikia maumivu sababu mishipa ya fahamu imetolewa, haya matibabu kwa kitaalamu yanaitwa ROOT CANAL TREATMENT
 
Huwezi kutatua tatizo bila kujua chanzo cha Tatizo. Dawa ni kwenda kwa daktari wa meno ili aone kama limetoboka ili walizibe kitaalam(u?) au lina matatizo mengine ambayo pia yatashughulikiwa kitaalam(u?). Dawa za kienyeji ni tiba ya muda tu.
 
Very Good "Yakuonea" kama ni mtihani ni 100% umeshinda.

Dawa ya jino si kung'oa, unapong'oa ni sawa na ukawa na kidonda mkononi ukaomba kukatwa mkono. Dawa ya jino unaanzia simple restoration up to root canal treatment kutegemeana na wewe mwenyewe unavyokuwa aware na mabadiliko yanayotokana na kuoza kwa jino. Nashauri unaposikia dalili za mwanzo kabisa za maumivu ya jino ni bora ukaenda kwa madaktari wa meno mapema ili upate suruhisho la tatizo lako.

Pamoja daimaaaaa!
 
Unaweza kutumia kitunguu saumu kiponde ponde halafu weka kwenye jino linalouma .au vipande vya ndulele kama tatu vikate kate kisha chemsha vikisha poa kamulia limao moja na dondoshea matone matatu ya mafuta ya taa kwa kutumia unyayo wa kuku kwenye mchanganyiko wako kwenye sufuria yako .chuja vizuri weka mchanyiko weko mahala pazuri ukipoa sukutua kutwa mara tatu kwa siku saba .meno hayatakusumbua

Hivi huu ni uganga wa kienyeji au ni nini, yaani niweke mafuta ya taa mdomoni na huo unyayo wa kuku ni kwa ajili ya nini?
mimi pia nina tatizo hilo. Naomba ndugu yangu ukipata maelekezo unielekeze tafadhali.
 
Man Ngosha,

Watafute forever products, wana dawa ya kusukutulia meno inauzwa 13,000/- ukitumia hiyo, jina lako itakuwa historia. Kwani uko wapi tukuunganishe na hao jamaa?

Kama uko mwanza, duka lao ni moja tu, lipo PPF gorofa ya tano karibu na mzunguko wa samaki.
 
unaweza kutumia kitunguu saumu kiponde ponde halafu weka kwenye jino linalouma .au vipande vya ndulele kama tatu vikate kate kisha chemsha vikisha poa kamulia limao moja na dondoshea matone matatu ya mafuta ya taa kwa kutumia unyayo wa kuku kwenye mchanganyiko wako kwenye sufuria yako .chuja vizuri weka mchanyiko weko mahala pazuri ukipoa sukutua kutwa mara tatu kwa siku saba .meno hayatakusumbua
Teh teh teh ! we utaua watu wewe!
 
dawa ya jino ni kung'oa.


Mkuu hii sio sahihi na niupotoshaji mkubwa kusema dawa ya jino ni kung'oa, nafikiri inaonyesha ni jinsi gani baadhi yetu hatuna uelewa na elimu juu ya afya ya kinywa ( oral health awareness and education). Jino ni kiungo muhimu sana kama kilivyo kiungo chochote katika mfumo wa mwili , hivyo ung'oaji wa meno si jambo linaloshauriwa kitaalamu hata kama jino linauma, kwani kuna taratibu na matibabu mengine yanaweza fanywa ukabakia na jino lako bila maumivu, ung'oaji wa memo usio na mpangilio mara nyingi husababisha madhara kwenye kinywa, mfano mpangilio mbaya wa meno kwenye kinywa (malocclusion) unaweza sababishwa na ung'oaji meno usio walazima, occlusal disharmony inaweza pia kutokea esp. When there is bilateral loss of posterior teeth, and with continued resorption of alveolar bone inaweza sababisha maumivu ya misuli ya uso (Myofacial pain), naomba tuondokane na hii dhana ya kuwa dawa ya jino ni kung'oa.
 
Back
Top Bottom