Dawa ya Ceftriaxone kwa mjamzito

matwin

Senior Member
Jan 7, 2016
124
133
Habari zenu jmn.... hii dawa ya kuchoma kwenye mishipa kwa mjamzito kwa ajili ya uti ni salama? haiwezi kuleta madhara kwa mtoto. ujauzito ni wa wiki 28...
 
Ameandikiwa hospitali ya Serikali au Private?

Matumizi mabaya ya antibiotic

Atumie tu Caps Amoxyclline kwa muda siku 7

Na pia awe anakunywa Maji ya kutosha
 
Habari zenu jmn.... hii dawa ya kuchoma kwenye mishipa kwa mjamzito kwa ajili ya uti ni salama? haiwezi kuleta madhara kwa mtoto. ujauzito ni wa wiki 28...
Ni Ceftriaxone,dawa ni salama in brief.
Sio cetriaxone
 
Private hosp
Tunatumia Ceftriaxone injection mahali ambako Mara nyingi hapastahili na hii ndiyo inayofanya kujenga usugu mapema sana wa sawa ambao ni muhimu kwa tiba.

Mahali ambao daktari angetumia antibiotic ya level ya kwanza au pili unakuta daktari anatumia antibiotic ya level ya tatu au ya nne ambayo ni ya juu kabisa bila sababu yoyote ya msingi. Mwisho wa siku tunatengeneza usugu wa sawa

Haya mambo kwa wenzetu wa ulaya na america huwezi kuyaona hata kidogo wanazilinda sana antibiotics zao ili kutozitumia ovyo Ku avoid kusababisha usugu wa sawa

Hapo ni changamoto kwa Madaktari, wafamasia,na mamlaka za usimamizi na ufuatiliaji wa huduma za afya
 
Mkuu uko sawa kabisa nakuunga mkono,mie naona Si changamoto kubwa sana kwa suala la huyu matwin,kati ya dawa zilizotumika na amabazo zinatumika in indiscrimate way ni dawa za familia ya penicillin,mfano shida za mfumo wa hewa kama mafua makali au kikohozi ,ni kama mtu anavyoweza kununua paracetamol mtu atakimbilia kununua Amoxicillin bila kupata ushauri wa mtaalamu. mtoa huduma alikuwa Sawa tu,ila kama ningekuwa ni Mashauri wake ningemuomba ampe Cefdnir badala ya Ceftriaxone maana ni ya vidonge hivyo mgonjwa hatapata traumatic treatment.Ceftriaxone ni dawa ya kawaida tu,third generation cephalosporin inategemea pia na culture and sensitivity results.
Kingine ninachokiona kila mtoa tiba anapo tizama mwenzie katoa tiba kwa mgonjwa anaona hayuko Sawa ila yeye ndo yuko Sawa zaidi anaanza kuponda Hata kwa tiba ambayo haina konakona.
Suala la biashara kwenye tiba nalo ni tatizo baadhi ya hospital binafsi wanakurundikia midawa kibao bila sababu za msingi wapate chao.
 
Kunadawa za daraja la chini ambazo zinafanya jazi vizuri tuu, na gharama rahisi.
Kama zipi? Na hii ni daraja la juu kivipi ?ila kwenye suala la gharama nakubaliana na wewe lakini si dawa hatarishi wala si dawa ya juu kivile,in brief it is broad pharmacological.May be walifanya culture & sensitivity,all in all is safe to be used in pregnant mother.
 
kwa TANZANIA rational use of medicines ni tatizo linalokuwa kwa kasi sana haswa baada ya tiba kufanywa zaidi kibiashara kuna hospital kama ALMC ya pale arusha ukiandikia mgonjwa dawa kama amoxycicline lazima wakufukuze kazi wao wanata uwaamwandikie mgonjwa dawa kama cefalexin, ceftriaxone, cefadroxil, flucamox , ili pesa ipatikane kwa wingi
 
Tunatumia Ceftriaxone injection mahali ambako Mara nyingi hapastahili na hii ndiyo inayofanya kujenga usugu mapema sana wa sawa ambao ni muhimu kwa tiba.

Mahali ambao daktari angetumia antibiotic ya level ya kwanza au pili unakuta daktari anatumia antibiotic ya level ya tatu au ya nne ambayo ni ya juu kabisa bila sababu yoyote ya msingi. Mwisho wa siku tunatengeneza usugu wa sawa

Haya mambo kwa wenzetu wa ulaya na america huwezi kuyaona hata kidogo wanazilinda sana antibiotics zao ili kutozitumia ovyo Ku avoid kusababisha usugu wa sawa

Hapo ni changamoto kwa Madaktari, wafamasia,na mamlaka za usimamizi na ufuatiliaji wa huduma za afya
Mpaka mbongo aende hospital ujue ameshajidunga mi antibiotic ya kutosha ...ningekubaliana na wewe kwamba kabla ya kuitibu hiyo UTI basi kufanyike C/S.

Na kuhusu wazungu kuzilinda antibiotics zao hapo sikubaliani na wewe kwani wao ndio wa kwanza kukimbilia madawa makali na kimsingi washaacha antibiotics nyingi za 1St generations na wanatumia advanced antimicrobial just to deal with minor infections.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom