Elections 2010 Dawa ya CCM ni Kuwatimua Mijini Kwanza

Ng'wanangwa

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
10,827
4,172
CCM ni mfumo. Na ili kuuangusha mfumo wowote, lazima uufahamu.

Pamoja na ufisadi na rushwa vinavyoabudiwa na CCM, mfumo wao wameujenga katika kupumbaza watu wa vijijini hasa wasio na elimu.

Wengi wa maharamia wa CCM wanaishi mijini ambako watu wengi 'zimo'. Ni katika maeneo ya mijini tu ambako raia wanaweza kuona namna CCM kilivyo uchi na wakakifanyia kitu chochote wanachotaka, kama walivyokivua nguo mwaka huu katika miji ya Mwanza, Musoma, Arusha, Moshi, Mbeya, Iringa, Tarime, Mpanda, na kwingineko.

Safari ni ndefu na ngumu. Ninavishauri vyama vya upinzani kushirikiana katika kuwamaliza hawa mafisadi wa CCM hasa maeneo ya mijini. Halmashauri zote za mijini ziwe chini ya upinzani baada ya uchaguzi mwaka 2015.

Kama kuna mahali CUF wanakubalika, vyama vingine viunge mkono, kama kuna mahali Chadema kinakubalika, vyama vingine viunge mkono na iwe hivyo hivyo kila mahali.

Tukifanikiwa 'kuwafukuza mijini', basi itakuwa ni rahisi kuwaeleza watu wa vijijini waache 'ujuha' wa kupewa fulana za kichina na kugawa kura kwa CCM huku wakiendelea kulia na umasikini wao.

Kata ninayoishi tumepata diwani wa Chadema bila kuwa hata na matawi, tukipata matawi je?

Nawasilisha.
 
Nitaishangaa sisiem ispo elekeza macho vijijini ambako wamepata kuchaguliwa . Muda ni muafaka sasa kuendeleza huduma za jamii vijijini ili kuweza kuwafanya hawa jamaa wa vijijini wasije kata tamaa na hiki chama kama hawa wamijini
 
Hata kuwaondoa vijijini inawezekana.
Kuna vijiji sasa hivi vimeanza kupata uelewa tofauti na miaka ya nyuma so effort kidogo tu inahitajika. ingawa nina mashaka na maeneo ya pwani bado wamelala usingizi.
 
Hata kuwaondoa vijijini inawezekana.
Kuna vijiji sasa hivi vimeanza kupata uelewa tofauti na miaka ya nyuma so effort kidogo tu inahitajika. ingawa nina mashaka na maeneo ya pwani bado wamelala usingizi.

Watu wa Pwani (isipokuwa Dar Es Salaam) tutawaachia CUF.
 
Hapata mkuu, tuna anza mijini na vijijini kwa mpigo.Hujasikia mpanda? tunapiga kote kote hawa wamekuwa simba wazee.
 
Hapata mkuu, tuna anza mijini na vijijini kwa mpigo.Hujasikia mpanda? tunapiga kote kote hawa wamekuwa simba wazee.

Sijasema kama vijijini tunawaachia CCM, hapana. Hoja yangu ni kwamba 'njia ni nyeupe' mijini. Vyama vifungue matawi na visajili wanachama wa kutosha ili mtu akitoka kijijini akaja mjini ajue kuwa kweli kumbe hata watu wanaowadhania wanamaisha mazuri (ndiyo mentality ya watu wa vijijini kuhusu watu wa mijini) wanataka mabadiliko!!?

Siyo kama ilivyo sasa. Ukienda kijijini, bendera za CCM zimetawala. Ukija mijini hata wagonga kokoto nao wanapeperusha bendera za CCM.
 
Back
Top Bottom