Dawa NKONG'OTO ya Ntwara na Binti Subira | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dawa NKONG'OTO ya Ntwara na Binti Subira

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Lekanjobe Kubinika, Aug 5, 2011.

 1. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #1
  Aug 5, 2011
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Source: Wapo FM

  Subira binti mdogo kule Ntwara Kata ya Malata (?) kagundua dawa inaitwa NKONG'OTO. Ati iinakong'ota magonjwa yote sugu na tunavyoongea sasa watu kibao kutoka Nsumbiji na Tanzania wamejaa kupata kikombe cha Subira. Clinical Officer mmoja aliyehojiwa na kituo hicho cha redio maarufu hapa DSM asubuhi hii, anadai kwamba ndiye anayeshughulikia maswala ya HIV/AIDS na anadhibitisha kwamba amewapima wagonjwa waliokuwa positive na walipopata kikombe akawapima tena na walikuwa negative. Mganga huyo anaiomba serikali imsaidie ntoto huyo kuboresha mazingira ili asaidie watu wengi wakiwa katika mazingira salama. Nsumbiji wanakuja mahututi na wanarudi kwa miguu yao.

  Ati ntoto Subira alioteshwa ndotoni, akamwambia mama yake waende porini na wakaona jani ambalo ndilo dawa. Huko porini ati huweziona jani hilo mpaka Subira mwenyewe awepo. Waandishi walipokwenda kumhoji wanadai alienda kuwapokea lakini ghafla akazimia na kuzinduka baadaye kuendelea na mahojiano. Wazazi wake wanadaiwa kukiri kwamba kuna mazingira ambayo binti yao anazimia ili apate majibu na kisha uliza swali lolote anakujibu.

  Wao! Tutaipata mwaka huu! Labda huyo atakubalika kwa Haji Mponda na wenzake wasiomkubali Babu, maana yeye anaswali sana Subira.
   
 2. Mbaliche

  Mbaliche JF-Expert Member

  #2
  Aug 5, 2011
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 292
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  mkuu nami nimeipata. Tusubiri kama kweli mambo yatafahamika tuu
   
 3. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #3
  Aug 5, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kama kawaida watz kwa kupenda mtelemko na bila kutafakali watajaa huko kama mvua
   
 4. Mbaliche

  Mbaliche JF-Expert Member

  #4
  Aug 5, 2011
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 292
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  <br />
  <br />
  shida ndio hufanya ivo
   
 5. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #5
  Aug 5, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Na mimi bado kidogo ntakuja na yangu
  Ninshaona watz nnapenda nterenko.
   
 6. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #6
  Aug 5, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  naaanza kuona msururu wa v8 za ssm na sirkaliiii ka loli ondoooo
   
 7. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #7
  Aug 5, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Tz hakwishi mambo,sasaivi wanasema inatibu baada wakisha chukua pesa za watu wanasema hakuna anaepona,hicho kituko kimpya.wanataka kutiana TB na hivyo vikombe.
   
 8. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #8
  Aug 5, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Loliondo itahamia kusini sasa!
   
 9. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #9
  Aug 5, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Hii yote ni kutokana na ujinga wetu...
   
 10. M

  Maengo JF-Expert Member

  #10
  Aug 5, 2011
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  siku za mwisho zikikaribia WATATOKEA MANABII WA UONGO! naona maneno ya Jizaz yanaanza kutimia!
   
 11. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #11
  Aug 5, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,923
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Kikombe sh ngapi??
   
 12. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #12
  Aug 5, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  Du ntwara si nchezo bhaaa,tanzania zaidi ya uijuavyo.........kesi ya jairo na shimbo wanataka waifunike hapo hakuna lolote!!! Tafakati chukua hatua..............
   
 13. Sabung'ori

  Sabung'ori JF-Expert Member

  #13
  Aug 5, 2011
  Joined: Jul 19, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 150
  Trophy Points: 160
  Hii ni janja ya serekali, kila inapokuwa imebanwa ktk mambo muhim inanzisha vijimambo iliwatu waondoe umakini wa kufuatiliaji wa yaliyo muhim wafuatilie huo uzushi...hapa adanganyiki mtu,tunataka maelezo ya huo wizi aliofanya Shimbo
   
 14. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #14
  Aug 5, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  kazi ipo
   
 15. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #15
  Aug 9, 2011
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Sasa kali zaidi yule binti akihojiwa Jumamosi na WapoFM asubuhi, Subira mwenye umri miaka 12 alisikika akisema live kwamba anasoma shule ya makaburini sura ya tano. Alipodadisiwa zaidi alidai ameoteshwa dawa hiyo na mungu lakini sio Mungu yule wa Yesu Kristo ila anayepatikana baharini. Ati anaendaga kule kila mara na hata ameambiwa atoze sh 500 tu kwa kikombe kama babu. Akadai anamfahamu babu kimiujiza ati wanakutanaga makaburini na baharini huko. Utata unakuja kwamba Babu anasema ameoteshwa na Mungu wa Yesu Kristo na hata shukrani anakataa kupokea anawaambia wakatoe kule kila mtu anakoabudu pasipo kujali dini. Yule mungu wa baharini kamwe hawezi kukuagiza uende Kanisani kupeleka shukrani maana kwake kufanya hivyo ni kama kujinyonga.

  Inadaiwa Subira peke yake ndiye awezaye kuutambua mti anaochimba dawa yake, ambao unazo rangi tatu, mama yake anapokuwa anachimba mizizi ya mti huo, Subira yeye huning'inia kama popo kwenye tawi la mti huo ambao unashuka ghafla na kutoweka anapomaliza kuchimba mzizi ambapo Subira hushuka kwenye mti ambako ati anajikunja mithili ya mkasi akijishikiza kwa miguu kichwa kikining'inia chini kama popo. Siku ya kwanza ati mama yake akiendelea kuchimba dawa aliona nyoka mkubwa anashuka kuelekea kwa Subira, lakini Subira akamwambia mamaye "we endelea kuchimba hiyo dawa, nyoka huyo ni mmoja wa wakubwa zangu wanaoniletea dawa hii. Alipomaliza kuchimba, nyyoka alishikwa kichwani na Subira kama alama ya kuagana kisha akashuka na wakaondoka zao na nyoka akapotea na mti.

  Ajabu zaidi, kwamba kama umekusudia kumtembelea anakuona tangia maili kibao na kusoma nia yako. Anaweza kuja kukulaki. Aliwatambua majambazi wakiwa maili 40 akawaunganisha wanakijiji kwenda eneo ambapo aliwahakikishia wanakijiji kwa kuwaonyesha alama walizoacha vichakani na akampumbaza mmoja ambaye aliongozana na ye mpaka kijijini wakati wenzake wamekimbia.

  Tofauti na Babu, Subira anakiri kwamba anafundishwa makaburini na baharini. Ila watu wa Msumbiji wamehojiwa live na wanakiri wanapona kabisa. Kweli tuko nchani mwa mwisho wa dunia. Mungu mwenyewe atajidhihirisha kuonyesha kweli iko wapi, tena sio mbali kutoka sasa. Wanamaombi wakazane kupiga magoti, lakini wasimwombee mtu afe kwa sababu ya tiba zake.
   
Loading...