Dawa ni wizara nyeti ziongozwe na wanawake

Ili kuondoa ufisadi uliokithiri sasa ni wakati muafaka wizara nyeti kama vile fedha, elimu, maliasili na utalii, ulinzi, tamisemi, kilimo, biashara, maji, nishati na madini, ulinzi, mambo ya ndani, afya, mawasiliano na uchukuzi zishikwe na akinamama UWAZIRI, UNAIBu WAZIRI na KATIBU MKUU. Hiyo itakuwa ni mwarobaini wa kuondoa UFISADI, pia IGP, CDF and MKUU WA TISS, DPP, JAJI MKUU, MKUU WA TAKUKURU zishikwe na akinamama

binafsi sikubaliani na ww hata kidogo, siamini kama tumefikia hatua ambayo hatuna tena mwanaume wakutuongoza, nakuuliza hv hakuna wanaume wanaoaminika hapa nchini? Labda ungesema hawa mawazir wasiwe wanasiasa bali wawe na hzo professional kulingana na wizara tena wachaguliwe kwa interview na malengo yao ktk wizara husika.
 
wabunge wengi wa kike viti maalum magamba wana degree za 'private relations' tutauza nchi
 
Timu ya ushindi CCM kuelekea 2015
Waziri Mkuu - Rose Migiro
Waziri wa Fedha Anna Tibaijuka
Ulinzi - Sofia Simba
Mambo ya Ndani - Jenista Mhagama
Utamaduni na Michezo - Vicky Kamata
Nishati na Madini - Stella Manyanya
Kilimo na Mifugo - Dr. Ishengoma
Maliasili na Utalii - Ummy Mwaimu
Utumishi - Hawa Ghasia
Afya - Dr. Nkya
Biashara - Mary Nagu
Uchukuzi - Esther Bulaya

Kwa mtaji huu CHADEMA kimeandaliwa kaburi


katiba hairuhusu Migiro kuwa PM yaani Prime Minister
 
katibu wizara ya elimu dr. Ndalichako anaweza. Uwezo wake ni mara elfu moja ya kikwete
 
Lilombe!
Wacha ndoto ya mchana. Unamkumbuka Zakhia Meghji yule mama aliyepewa uwaziri wa fedha na JK ?
alishindwa inside out na imekuwa ni aibu and a national tragedy. Kikwete atakumbukwa kwa kituko alichokifanya kumteua Mwanamke mchovu aliyekuwa na kashfa kibao kutoka Enzi ya Mkapa . We all know how it ended. Kikwete took another failure in the name of Mustafa Mkullo kwa misingi ya kidini mpaka Leo ndiye Exchequer ona madudu alivyofanya kuanzia misamaha ya hovyo ya kodi. JK is a big failure na hataacha cha kukumbukwa apart from ngono na Dini!
 
dah sikubaliani na wewe kwamba wanawake wanaweza wote au wanaume wote hawawezi
 
Napendekeza waziri wa Fedha awe Sofia Simba, Nishati na madini Vicky Kamata.

inabidi katiba mpya tuweke kipengele cha kulipia mawazo tunayowaza ili kupunguza wanaowaza pumba. Hivi meghji si alikuwa waziri wa fedha kipindi cha kwanza cha jk? Blandina nyoni aliyenunua magari ya bilion 1.3? Nkya ni mwanaume?
 
kwani wanawake ndo sio mafisadi???Mbona Getruda Mongera hadi kule Bunge la afrika kafanya ufisadi mpaka kaitia aibu Tanzania??
Kumbe mambo mengi siyaelewi? Getruda huyu huyu mbeijin No. 1 au mwingine?
 
Wakati balali na wakina liyumba wanajichotea yale ma-zilioni yetu..nani alikuwa waziri wa fedha vileee??!?..that's right..kuwa mwanaume au mwanamke hakukufanyi uache kuwa idiot.
 
Hapa issue sio jinsia, nadhani ingekuwa vema sasa serikali ikubali kuzisimamia sheria na kanuni zilizopo kuhakikisha uwajibikaji wa viongozi wetu. Mtu akilikoroga alinywe, biashara ya kulindana sasa basi.
 
tatizo ndani ya ccm haijulikani nani mwanamke nani mwanaume wote wanafikra,mtazamo na maamuzi sawa.dawa ni Manumba na Hosea waachwe huru kufanya maamuzi bila kuingiliwa na wanasiasa vivyo hivyo na mahakama. inaweza kusaidia .
 
issue sio kuongozwa na mwanamke, kinachotakiwa ni kuongozwa na mtu mwadilifu, mchapakazi na mzalendo mwenye kuheshimu sheria za nchi bika kujali jinsia....
 
Ili kuondoa ufisadi uliokithiri sasa ni wakati muafaka wizara nyeti kama vile fedha, elimu, maliasili na utalii, ulinzi, tamisemi, kilimo, biashara, maji, nishati na madini, ulinzi, mambo ya ndani, afya, mawasiliano na uchukuzi zishikwe na akinamama UWAZIRI, UNAIBu WAZIRI na KATIBU MKUU. Hiyo itakuwa ni mwarobaini wa kuondoa UFISADI, pia IGP, CDF and MKUU WA TISS, DPP, JAJI MKUU, MKUU WA TAKUKURU zishikwe na akinamama

kama wanawake wenyewe ndio akina Anna Makinda, Mary Nagu, Hawa Ghasia, Celina Kombani... basi naomba tuanze kuwapa nafasi watoto sasa
 
Back
Top Bottom