Prof Koboko
JF-Expert Member
- Aug 15, 2020
- 350
- 2,549
Sasa hatuwezi kuendelea kuwaachia nchi watu walioshindwa kuiendesha, haiwezekani gharama za maisha kupanda kwa kiasi kikubwa huku pesa mzunguko wake ni mbovu halafu kila siku kudumu Chama chaMapinduzi.
Sasahivi kununua vifaa vya ujenzi ukiwa mipakani Tarime kutoka nchi jirani ya Kenya ni nafuu, kununua vifaa vya ujenzi ukiwa Tunduma toka Zambia ni nafuu kuliko kununua toka Tanzania.
Hata kujaza gari yako mafuta kutoka kwenye nchi jirani ni ahueni kuliko nchi yetu, mtu unajiuliza hivi Bongo kuna mdudu gani? Kwanini tunaendelea kuuimizana makusudi? Vifaa vya ujenzi bei juu, Luku makato juu, Mafuta bei juu, Miamala ya simu bei juu, hivi wanataka tukaishi taifa gani?
Kama wenzetu wamewapa rais wao unafuu wa maisha sisi nchi kumwa yenye rasilimali asili kibao tunashindwa nini? Hivi nchi jirani wanatushinda kitu gani?
Kuna kauli fulani ya hovyo hovyo sana eti lipa tozo uchangie maendeleo yako, hii ni dharau kwa watu wenye mlo mmoja kwa siku.
Mnashindwa kusimamia uwekezaji wa kutosha kwenye Utalii, viwanda na madini tupate pesa ya kutosha tuache kuongeza tozo zinazowaumiza wananchi, mnafurahia kwa sababu mnalipwa mishahara mikubwa, shida za wengine hamzijui mnaamua mtakapo.
Nilichogundua ni kwamba lazima CCM itoke madarakani, haiwezekani bunge jua bubu linapitisha bajeti inavyoumiza wapiga kura wako kimya wanaogopa eti wanatishwa bunge litavunja, khaa si bora livunjwe wasimamie maslahi ya taifa?
CCM imeshindwa kabisa kumpunguzia mwananchi ugumu wa maisha na matokeo yake yake wamekua na visingizio eti bado wanatengeneza nchi. Lazima raia wafurahie taifa lake badala ya kutumia bila sababu za msingi.