Dawa na njia mbadala za Kupunguza unene/uzito | Weight Loss techniques and advice

Nimeona watu wametoa michango mingi sana ila kuna wale wanapotosha, eti kuna mbinu ya kupunguza kilo moja kwa siku. Huo uwongo tu, ifahamike kilo moja ni grams 1,000 hilo haliwezekani.
Binafsi mimi nilikua mnene sana kupindukia, unywaji wa pombe ulichangia pakubwa, zikiwemo hata konyagi ambazo kuna wengine wanadanganya eti inapunguza uzito kisa ina ukali. Ifahamike Konyagi kama pombe zingine ina wanga.

Kilichonisaidia mimi hadi nikawa napunguza kilo moja kwa wiki
- Nilianza kula tango, ifahamike tango ina calories kidogo zaidi ya vyakula vyote. Hivyo kabla sijaanza kula chakula, ilikua naanza na tango kadhaa, kiasi kwamba nahisi nimeshiba halafu sasa hapo nabugia msosi. Hivyo najipata nakula chakula kidogo maana tango zimejaza tayari.

- Nikapunguza wanga, ugali nakula kidogo lakini pembeni najaza vyakula visivyokua na wanga kama mamboga mboga
- Nikaacha pombe kabisa
- Nikaendelea na mazoezi, ifahamike nilikua napenda mazoezi tangu hapo awali japo sikua napunguza uzito hata nikifanya mazoezi makali kiasi gani.

Hivyo vitu vichache tu, baada ya miezi mitatu watu wakaanza kunishangaa. Halafu huna haja ya mazoezi mazito, tembea kilomita tano kwa siku basi.

Great msaada mkuu. Thanks
 
Mkuuu ua right.. Me nilikuwa mnene na kitambi zaidi ya Komba (R. I. P) mazoezi hayakusaidia.. Nikaacha pombe.. Nikapunguza msosi.. Mazoezi sana tena home tu (Yaani chuma ya nondo) ..saizi nakaribia kuwa na Six Pcks.. Baunsa wa kutosha
 
Poa sana, japo hapo pa kupunguza msosi ndio panafaa kueleweka vizuri, maana watu wanajitesa kwa njaa bila kuwa na mikakati. Ifahamike ukianza kujitesa kwa njaa na utashangaa maana hutapungua hata kilo moja, maana mwili ukihisi kuna mapungufu ya chakula, unaanza kuingia kwenye defensive mechanisms na kugoma kuchoma mafuta kwa kasi.

Chakula unafaa kula, japo kwa kufuata mkakati. Kwa mfano unapunguza wanga, halafu unakula chakula kidogo kidogo ila kwa interval fupi.
 
Kuna madhara gani ya kutumia dawa za kupunguza unene/kitambi/nyama uzembe?

Ni dawa ipi sahihi ya kufanya hayo?

Ni kweli kuna dawa za kufanya hayo?

Na je ukitumia hizo dawa na kufanikiwa hautonenepa tena?
 
1.acha kula wanga na sukari(soda juisiza maboksi chupa ugali wali mkate maharage andazi chips nk nk)
2.kula mayai, nyama samaki kuku dagaa mboga zote za majani kula mafuta yote kwny nyama usitoe
3.kula matunda usikamue juice ni mbaya kula tunda lenyewe tu kwa kiasi isipokuwa ndizi matunda yenye sukari km nanasi embe kula kidogo mara moja moja tango parachichi kula uwezavyo
3.fanya mazoezi kidogo hata ya kutembea nusu saa kwa siku
4.kunywa maji mengi uwezavyo walau dumu la azam kubwa kwa siku
Hapa tunaondoa unene wa wanga ukichepuka haitasaidia ukikomaa nayo hii ratiba kwa miezi miwili utaona tofauti kubwa sanaaaa ukifilia lengo la uzito wako unaweza kula vilivyokatazwa kwa kiasi tu kidogo achana na dawa mwili wako ni chakula unachokula na si vinginevyo mazoezi yanachangia 20% chakula 80% kuwa makini kwenye kula zaidi hata ukushinda gym haisaidii kama utaendelea kula wanga mfn wali ndondo ugali nk nk tena unakula usiku saa 4 hivii unaenda kupigana huko ndotoni ukahitaji ule sahani la ubwabwa na miharage
 
Sidhani kama kuna dawa ya kupunguza unene!

Watch what you eat and excercise is the solution for overweighted people.
 
1.acha kula wanga na sukari(soda juisiza maboksi chupa ugali wali mkate maharage andazi chips nk nk)
2.kula mayai, nyama samaki kuku dagaa mboga zote za majani kula mafuta yote kwny nyama usitoe
3.kula matunda usikamue juice ni mbaya kula tunda lenyewe tu kwa kiasi isipokuwa ndizi matunda yenye sukari km nanasi embe kula kidogo mara moja moja tango parachichi kula uwezavyo
3.fanya mazoezi kidogo hata ya kutembea nusu saa kwa siku
4.kunywa maji mengi uwezavyo walau dumu la azam kubwa kwa siku
Hapa tunaondoa unene wa wanga ukichepuka haitasaidia ukikomaa nayo hii ratiba kwa miezi miwili utaona tofauti kubwa sanaaaa ukifilia lengo la uzito wako unaweza kula vilivyokatazwa kwa kiasi tu kidogo achana na dawa mwili wako ni chakula unachokula na si vinginevyo mazoezi yanachangia 20% chakula 80% kuwa makini kwenye kula zaidi hata ukushinda gym haisaidii kama utaendelea kula wanga mfn wali ndondo ugali nk nk tena unakula usiku saa 4 hivii unaenda kupigana huko ndotoni ukahitaji ule sahani la ubwabwa na miharage
hujaeleweka kabisa!
 
Ndugu hili tatizo ni sugu sana. Kinachotakiwa ni mke wako mwenyewe awe na nia ya kupungua. Kama hana utajisumbua bure tu.

Ili apungue anatakiwa apunguze vitu vya sukari sana na mafuta. Soda, bia, chips, juice zenye sukari nk akae navyo mbali. Najua hapa ni pagumu.

Awe anafanya mazoezi. Kuruka kamba au jogging inamtosha sana. Ahakishe kila siku atenga nusu saa ya mazoezi ya kutokwa jasho.

Nasisitiza km yeye hana nia ya mazoezi utakuwa unajisumbua bure.

Unaweza kumshawishi mfanye wote jogging au kuruka kamba.
mazoezi bila kubadili aina ya vyakula...kamwe hantofanikiwa
 
1.acha kula wanga na sukari(soda juisiza maboksi chupa ugali wali mkate maharage andazi chips nk nk)
2.kula mayai, nyama samaki kuku dagaa mboga zote za majani kula mafuta yote kwny nyama usitoe
3.kula matunda usikamue juice ni mbaya kula tunda lenyewe tu kwa kiasi isipokuwa ndizi matunda yenye sukari km nanasi embe kula kidogo mara moja moja tango parachichi kula uwezavyo
3.fanya mazoezi kidogo hata ya kutembea nusu saa kwa siku
4.kunywa maji mengi uwezavyo walau dumu la azam kubwa kwa siku
Hapa tunaondoa unene wa wanga ukichepuka haitasaidia ukikomaa nayo hii ratiba kwa miezi miwili utaona tofauti kubwa sanaaaa ukifilia lengo la uzito wako unaweza kula vilivyokatazwa kwa kiasi tu kidogo achana na dawa mwili wako ni chakula unachokula na si vinginevyo mazoezi yanachangia 20% chakula 80% kuwa makini kwenye kula zaidi hata ukushinda gym haisaidii kama utaendelea kula wanga mfn wali ndondo ugali nk nk tena unakula usiku saa 4 hivii unaenda kupigana huko ndotoni ukahitaji ule sahani la ubwabwa na miharage
Nimecheka hizo line A mwisho mwisho jamani...
 
Mkuu mbona hii inafanana na maple syrup?
Mkuu hapana hiyo siyo Maple Syrup. Maple Syrup hii hapa chini angalia picha.

MPLE SYRUP.jpg
 
Habari wakuu,

poleni na majukumu naomba mwenye kujua jinsi ya kupunguza kilo ,mwanzoni nlikuwa na kilo 74 ila sasa zimeongezeka hadi 87,nlikuwa natamani nirudie kilo zangu za mwanzoni ,maana kwa hizi kilo najisikia mzito na magonjwa ya kila mara,nakiri sifanyi mazoezi kabisa na naelewa kilo ni kuhusu kupunguza calories intake daily.

My condition
Nlipo siwezi kusema naweza kujipikia misosi ya kupunguza wese kama kuna dawa isiyokuwa na madhara iwe ya kienyeji au ya kizungu ningependa kutumia.
===

MAONI YALIYOTOLEWA NA WADAU
Kabla ya kuamua kupunguza uzito,

Wengi huchukizwa na muonekano wa sehemu za tumbo, mapaja na mikono. Hivyo ni rahisi zaidi kupunguza uzito kama utaondoa nyama zembe katika sehemu hizo.

Ili kuondoa nyama zembe unatakiwa kupunguza ulaji wa vyakula vya wanga na ngano (hasa zilizokobolewa).

Vilevile kupunguza ulaji wa vyakula vyenye sukari nyingi na unywaji wa bia.

Ule nini sasa?

Mbinu ya Kwanza
- Kula mbogamboga
- Chai ya Tangawizi, mlonge, n.k
- Kula Samaki
- Matunda
- Wanga & Ngano zisizokobolewa
- Mbegu za Maboga, karanga, korosho, nyonyo, ufuta n.k
- Kunywa maji mengi

Jitahidi kula vyakula hivi mara tu unapohisi njaa. Kama huhisi njaa usile.

Vyakula hivi vitakusaidia kuhisi umeshiba kwa muda mrefu wakati huo huo mafuta ya nyama zembe yatakuwa yanachomwa.

Kama utakula vyakula hivi kila siku kwa wiki 4 hadi 6 utaweza kupunguza kilo 5 mpaka 10 haijalishi kama ni unene wa urithi au uzazi.

Pia tumbo na nyama zembe vitatoweka na utaanza kujihisi mwepesi na hata kuanza kufanya zile kazi ulikuwa huwezi kufanya kabla.

Mbinu ya Pili ambayo husaidia kuondoa nyama zembe kwa muda mfupi zaidi ni ulaji wa 'Mlo mbadala' asubuhi na jioni (Chrysanthemum Diet tea).

Njia hii imekuwa msaada kwa wengi kutokana na kuwa na uwezo mkubwa wa kuzuia njaa kwa muda mrefu na kuufanya mwili upate nguvu kutoka katika mafuta yaliyo kwenye nyama zembe hivyo nyama zembe kutoweka ndani ya siku chache tu baada ya kuanza kutumia mlo mbadala.

Kuendelea kupata mafunzo mengi kama haya kuhusu mbinu za kuondoa nyama zembe mwilini pamoja na matatizo mengine, tafadhali comment.
---
kupungua ni kwepesi sana hasa kwa wale walio amua na kutia nia. kinyume cha hapo ni kazi bure.
kifanyacho mtu kunenepa ni ulaji mwingi wa wanga na sukari, mtu ukiweza kuviacha hivyo matokeo unayapata kwa haraka zaidi ila ukivipunguza na kupunguza idadi ya milo kwa siku utapata matokeo ila taratibu sana ambako unaweza usigundue ka unapungua

Unene ni matokeo ya ulaji uliopindukia na amabao mara nyingi unaendana na kutokuwa na ratiba nzuri ya ulaji yani mtu anakula pale aonapo chakula pasipokuzingatia kuwa ananjaa ama la, pia milo mingi kwa siku yani mtu anakula saa 12 asubuhi, saa 4, saa 7 saa 10 na saa 3 usiku, na vyakula vingi alavyo ni wanga na sukari. kwanini mtu asiongezeke na afanane na funza?

Tuchukue hatua dhidi ya tatizo hili maana uzito mkubwa ni tatizo ambalo linaleta matatizo mengi katika mwili ambayo maranyingi hospitali hawawezi yatibu na yakatokomea maana chazo kinabaki na hakililiwi msisitizo na kuonekana ka tatizo.
---
Badilisha life style yako. Mazoezi, piga jogging sana, jogging inakata uzito, piga mazoezi ya kukata tumbo kila siku. Badili mlo wako. Mimi nikaamka nakunywa maji ya moto, then ninapiga jogging 8 kms everyday in the morning, baadae nakula matunda na glass moja ya maziwa.

Mchana nakula lunch ya nguvu ila naangalia sana mafuta. Jioni ni kachai tu au matunda tena. Hapo lazima afya yako ishike adabu. Usiwe unakulakula hovyo. kama mazingira yako hakuna sehemu ya kufanyia viongo, piga mazoezi hata chumbani kwako. Kila la kheri
---
Kupungua uzito kwanza inabid ujijue why umeongezeka uzito ghafla. Kuna watu wengne wana nature ya miili minene, kuna koo za namna hii, yan wao wale san wasile san wakifikisha umri flan wanakuwa mabonge automatically na kuna wengne ni viceversa, hata wafanyeje miili haiongezeki ng'oo.

Km unene wako sio geneticaly inherited basi kutakuwa na other causes ambayo ww binafsi unaijua. Kwa hiyo ukishaijua hiyo cause basi change that habit na utapungua bila wasiwasi.

Nikupe mfano, mm mwshon mwa mwaka jana nilikuw na 74kg. Kufika July mwaka huu zikaongezeka mpk 78kg. Kwa hiyo nikawa najiona mzito san plus kakitambi uchwara. Nikaona hii hali hapana. Lkn nikawa najua kabsa hii imesababishwa nature ya kaz yangu. Nilikuw nakula vzr lkn kile nachokula hakifanyi kaz ipasavyo.

Hivyo nikaamua kupunguza mlo, nikiwa kazin asbh sinywi chai nakula lunch tuu basi. Na nikirudi home sili tena chakula kizito, either nakunywa chai ya maziwa tuu ama naongezea na bites yyte ya kudanganyia tumbo. Ndani ya mwezi nilipunguza kilo 4, na mpk sasa znaendelea kupungua, nina 73kg now.

Kazi kwako.
---
Ngoja nikuambie ukweli unaokwepwa na watu wengi. Kupunguza uzito ni combination ya vitu viwili 1. Mazoezi 2. Diet. Ukifanya mazoezi ya nguvu na kuacha kula vyakula vya kunepepesha kwa wingi utapungua uzito. Kuna bondia anaitwa Tyson Fury kesho tarehe moja anapambana na Wilder.

Anakukuambia amepunguza kilo zaidi ya 50 kwa muda mfupi kwa kufanya mazoezi na kula milo sahihi. Usidanganyike: HAKUNA dawa za kupunguza uzito Narudia tena usidanganyike kuwa kuna mtu atakupa au kukuuzia dawa ya kupunguza uzito.

Utakuja kumeza madawa yenye madhara bure, na madhara yake utayaona baadae, si ajabu baada ya miaka kumi hata ishirini. Mazoezi yatosha.
 
Back
Top Bottom