Dawa na njia mbadala za Kupunguza unene/uzito | Weight Loss techniques and advice

fanya mazoezi, pia weka mazoea ya kunywa maji ya moto(sio sana) kila asubuhi kabla ya chai.
na mlo wa usiku usiwe mgumu,uwe mwepesi na pia ule mapema sana kabla ya kulala.
 
Mimi pia nina kafriza lakini biere huwa napiga na kuacha siwezi kamwe, je nikifanya hayo yote kafriza katatoka?
 
Binafsi nilikuwa na kilo 72
lakini sasa nina 60 na tumbo
ndo lilikuwa tatizo kuondoa mafuta ..

Huwa na kimbia asubihi kwa 30mnts
Nafanya set ups na push ups..technic iliyonisaidia kabisa kuondoa tumbo na lovehandels nii hii lala na mgongo halafu nyanyua mguu wa kulia lakini upeleke kushoto na fanya hivyo na mguu wa kushoto pia.. mambo ya diet kweli sikuyazingatia sana
I hakikisha unapiga mazoezi zaidi...kama kukimbia kwa nusu saa huchoki kimbia dakika45 ...na zidi kuongeza dakika..

Kitu kingine kinachosaidia sana ni boxing
hakuna zoezi zuri kama boxing..
Jitengenezee punching bag safari ianze
all the best.. chagua zoezi na stick with it..
 
nimefurahishwa na majibu safi. jamani nampa angalizo, usinywe konyagi kwa maana ya kupunguza kitambi. hiyo ni kinywaji kunywa kwa starehe yako, tutazunguka sana ila hapo muarobaini wa tatizo la kitambi ni kufanya mazoezi, kupunguza wanga/starch na mafuta. wengi hatuna nidhamu ya kula na kunywa na mtu akifanya hivi tunamwona anajitesa na choka mbaya, tubadilike!
pia utamaduni wa mazoezi haupo na mbali na elimu kutolewa lakini tumekuwa wagumu sana kujenga utamaduni huu mzuri. hakika tubadilike jamani itatusaidia sana.
 
Tumbo/Kitambi kinasababishwa na mafuta yanayolundikana kwa sababu mwili unapata energy (chakula cha kuongeza nguvu/joto mwilini) nyingi kupita unavyotumia, na hivyo ziada inahifadhiwa kama mafuta sehemu mbali mbali za mwili, mara nyingi kwenye ukuta wa tumbo (abdominal wall).

Kwa hiyo basi, kuna njia tatu tu za uhakika kuweza kutatua hilo tatizo... 1. Kupunguza kiasi cha energy (chakula) unachokula ili kuzuia ziada isilundikane kama mafuta kwa kufanya diet, 2. Kutumia hiyo ziada ya energy (chakula) iliyolundikana tayari kama mafuta kwenye ukuta wa tumbo (kitambi) kwa kufanya mazoezi na kazi nyingine za nguvu, 3. Kama una hela..fanya upasuaji kutoa hayo mafuta yaliyolundikana (kama alivyofanya Mustafa Hassanali).

Hizo story za chai, sijui kufunga special belt, dawa za kumeza etc hazina ushahidi wa kisayansi kuwa zinafanya kazi, na kama matokeo yake ni ya kudumu.

in addition fanya situps kustrengthen abdominal muscles...kama una kitambi kilichopitiliza na huwezi ku control diet kuna operation za kupunguza urefu wa utumbo mwembamba ili usiabsorb chakula kingi baada ya kula...(NEW DEVELOPMENT)
 
Ukitaka kupunguza unene na maradhi mengi yaondoke ufuate yafuatayo muda wa mwezi au zaidi:

1. Kabla ya kula kwa nusu saa unywe maji gilasi moja au mbili au tatu au zaidi na baada ya nusu saa au robo saa:
2. Ule salata sahani kubwa sana sana na inaruhusiwa kula matunda na baada ya kula salata
3. Ule chakula chako kisiwe na mafuta mafuta.
4. Huruhsiwi kabisa wakati wa chakula kunywa maji na pia baada ya chakula ila baada ya masaa mawili.
5. Chakula cha usiku kiwe mapema na kidogo sana.
6. Ukiwa na tumbo kikubwa na huna mimba basi ili tumbo kiondoke haraka uchukue magamba ya kabichi uipashe moto kidogo sana yaani upate mvuke khalafu magamba uitie nje ya tumbo lako uifunge vizuri mpaka asubuhi katika siku mbili utaona kua umepungua zaidi ya kilo mbili.
 
Ukitaka kupunguza unene na maradhi mengi yaondoke ufuate yafuatayo muda wa mwezi au zaidi:

1.Kabla ya kula kwa nusu saa unywe maji gilasi moja au mbili au tatu au zaidi na baada ya nusu saa au robo saa:
2.ule salata sahani kubwa sana sana na inaruhusiwa kula matunda na baada ya kula salata
3.ule chakula chako kisiwe na mafuta mafuta.
4.Huruhsiwi kabisa wakati wa chakula kunywa maji na pia baada ya chakula ila baada ya masaa mawili.
5.Chakula cha usiku kiwe mapema na kidogo sana.
6. Ukiwa na tumbo kikubwa na huna mimba basi ili tumbo kiondoke haraka uchukue magamba ya kabichi uipashe moto kidogo sana yaani upate mvuke khalafu magamba uitie nje ya tumbo lako uifunge vizuri mpaka asubuhi katika siku mbili utaona kua umepungua zaidi ya kilo mbili.
Hiyo ya kabichi ,imekaa kishotishoti
 
kwa wanawake na wanaume walio na mwili wenye uzito na unene mkubwa yupo daktari kwa ajili yenu wa kuwapa huduma nzuri ya kupunguza unene na uzito na kurudi hali ya kawaida pamoja na kukupa ushauri wa kitaalamu ambapo mgonjwa ataridhika .
tuma maombi yako ktk email ifuatayo: lubaziemmanuel@yahoo.com
 
Kumbe tangazo, mi nilidhani kuna mtu ana hiyo shida ili nimpe darasa!!!

Subiri mkuu wenye shida watakutafuta tu!
 
Wizi tu hamna kitu hapo. Dawa ya unene ni mazoezi, waache uvivu. Full stop!
 
NDUGU ZANGU WAPENDA WANGU HUMU NIWATAKIENI HERI YA MWAKA MPYA WOTE KWA FURAHA NA UPENDO MLIOONYESHA KWANGU KWA MWAKA MZIMA,LAKINI NINA SWALI DOGO KWENU,MWAKA 2012 NATAKA NIPUNGUZE NUSU YA KILO NILIZO NAZO,NAOMBA MNISHAURI NI CHAKULA GANI NAWEZA KULA AU NJIA GANI NZURI YA KUPUNGUZA UZITO KWA KWELI SINA MUDA WA KUFANYA MAZOEZI KABISA ILA NAHITAJI UZITO UPUNGUE ,VITU NINAVYOPENDELEA SANA NI BIA BARIDI,KITIMOTO,SUPU ASUBUHI,KWA KWELI ITAKUWA VIGUMU KUVIACHA ILA KAMA KUNA JINSI BASI NISAIDIENI MAANA FURAHA YANGU IKO SANA KWENYE HAYO MASANGA HAHAHAAA,ILA NATAMANI SANA MWAKA HUU UNAOANZA NIPUNGUZE NUSU YA KILO ZANGU KWA SASA NINA KILO 192.

AHSANTENI SANA NARUDIA TENA KUWATAKIA MWAKA MPYA MWEMA,KARIBUNI MNISHAURi
 
Back
Top Bottom