Dawa na njia mbadala za Kupunguza unene/uzito | Weight Loss techniques and advice

kama ushauri wa hapo juu pia apunguze kula vitu vya mafuta na kukaanga kaanga kama chipi zaidi apendelee mchemsho
 
Kuogelea ni zoezi zuri sana kama si mwoga wa maji au hili pia analiweka kwenye kundi la gym? lakini km walivyosema wengi hivyo vinyama uzembe ni mafuta ya ziada...bahati mbaya sana mahali mafuta ya ziada hukimblia ni hapo. Kuwa makini na vyakula na pia muda wa kula, wengi wetu hasa kwa mlo wa usiku/jioni, baada tu ya kumaliza kula ni kulala hili pia ni tatizo.
 
Watch your diet, beside sit ups, walking or jogging at least 5 days a week is very important..
 
Tatizo la mrundikano wa mafuta mwilini huchangiwa na sababu mbalimbali ikiwemo ulaji mbovu, uvaaji wa nguo zinazobana kama skin tight na jambo lingine ni ulaji wa kuogofya wa sukari na mafuta.
Nitatoa mfano mojawapo wa chanzo cha tatizo. Endapo mwanamke anapenda kuvaa skin tight, kiasi kikubwa cha mgandamizo juu ya ngozi hupelekea damu ipite kwa shida na hivyo kukwamisha uzambazwaji wa mafuta mwilini na lymphatic liquids. kiasi cha mafuta kinachoshindwa kupenya kushuka chini hujikusanya tumboni au pembezoni mwa kiuno na kusababisha kitu kinachoitwa kitambi au matuta.
Kitaalam mwili wa mwanamke hautakiwi kubanwa kwani kubanwa huko hupelekea kiasi kikubwa cha homorne kushindwa kubalance vizuri mwilini. Hali hii hupelekea matatizo kama kutopata hedhi kwa wakati muafaka au kupata kwa maumivu makubwa kutokana na kiasi kikubwa cha damu kuganda wakati inashuka na mishipa ya uzazi. Matatizo ya hedhi hutokana pia na matumizi kemikali ziwekwazo kichwani ambazo hupelekea sumu kubwa kupenya mwilini na kuleta matatizo kwa mtumiaji.
Muuliza swali anaweza kutumia mdalasini na asali kama kinywaji ili kuondoa mafuta ya ziada na kutojibana sana na nguo.
Maswali zaidi
uliza gmartttz@yahoo.com
 
Jaribu kufanya sit ups hii inasaidia na kupunguza kula pia!

Sit-ups pekee hazisaidii inabibi ziwe sehemu tu ya mazoezi,kitu cha kwanza ni kupunguza kula wanga na mafuta mengi[usiache kabisa mafuta yana kazi muhimu mwilini],pili aongeze uunguzaji wa chakula mwilini[metabolism] kwa kula milo midogo 5 badala ya mikubwa 3,atumie kahawa na chai ya rangi zinaongeza uunguaji wa chakula,anywe maji mengi na kuacha soda zote ila club soda/soda water ina magadi yanasaidia usagaji wa chakula.Tukija kwenye mazoezi akimbie mara 3 kwa wiki[aanze pole pole na keongeza umbali kila wiki],ajinyooshe-stretching kabla na baada ya mbio,na mwisho kabisa alale masaa 7-8 kwa siku hii pia inasaidia kupungua.Kuogelea ni zoezi tosha kabisa likifanyika hata mara 2 kwa wiki.
 
jamani manyamanyama kama hayo si ndo pouwa??? ...............sasa akikonda ukipeleka mkono utashika nini? ..................na je siku akiunganishwa kwenye nanihii ya taifa, machale yatachezea sehemu gani kama unataka aanze kunyanyua mabega sasa hivi?? ..............teh teh tih.................
 
Mazoezi ni muhimu. Namshauri ajitahidi kufanya mazoezi ya aerobics ambayo yanasaidia kupunguza mafuta, as we know body fats only burn with excessive oxygen intake, pamoja na weight lifting kidogo ili kukaza misuli.
 
Jamani kitu rahisi cha kupunguza tumbo kwa wabongo ni hivi wanawake pikeni vyakula vya kuchemsha mara tatu kwa wiki .pia visafari vifupi sio lazima upande gari.
asubuhi ukipata chai safi mchana chakula cha moto ,jioni sio lazima pia ushambulie ugali.chukua tu matunda,mtapona bila hivyo hamtafikisha miaka stini kama mama zenu.mimi nilienda Bongo mwezi mmoja ,nikajaribu kushindilia kama wadogo zangu nimerudi kwangu mume wangu alikasirika na sasa nimerudia hali yangu ya kawaida.kupika namafuta sio penzi,mpikie mumeo na wewe mwenyewe vyakula ambavyo vitawatunza mpaka muone wajukuu zenu.ni hayo tu
 
hakuna zoezi la "kupunguza tumbo" hauwezi kutarget area ya mwili wako unayotaka ipungue wataalamu wanaita hii "spot reduction" haiwezekani.

Unapunguza overall bodyfat kwa kutumia calories nyingi kuliko unazokula, calories out > calories in. Ukifanya hivyo utapunguza bodyfat, ila eneo ambalo litapungua inategemea na genetics zako, wengine wanapungua tumbo wengine mapaja etc. Hakuna njia ta ku-controll hili.

i love it
 
mazoezi muhimu yanasaidia kwa vile umesema unataka mazoezi ya ndani sit-ups zinasaidia na kingine mwache bi mkubwa ashughulike zaidi kwenye tendo la ndoa huwa inawasaidia wanawake wengine.kitu kingine fanya nae mazoezi kimbieni kwa pamoja hata mara mbili kwa wiki utakuwa unampa moyo sio unataka yeye afanye mazoezi wakate wewe hufanyi sio powa.na ni raha sana kufanya mazoezi na mke wako jaribu utaona.kitu kingine hale milo midogo dogo mara 5 kwa siku kila baada masaa matatu hii inasaidia ku-increase metabolism yako ambayo itamsaidia kuunguza calories zaidi. Hii milo ni mboga za majani,matunda,samaki na kuku bila kusahau maji mengi.aache kula wali badala anaweza kutumia viazi vitamu kidogo tu.mwisho wa kula atleast 8pm.na anaweza kuongezea kunywa green tea she should be good to go ukijumlisha na ushauri wa watu wengine.ukifutilia hivyo na akiwa mvulimu wa vyakula vya haina hio atafanikisha lengo lake.kumbuka mazoezi muhimu sana.

asante mkuu this too should work
 
Naomba tutajiane aina ya vyakula ambavyo vinasaidia kupunguza uzito, Kuna jamaa alinipa List ya vyakula ambayo anadai inaweza kupunguza uzito kwa haraka, naomba muipitie na tuelimishane
1-kuku au samaki wa kuchemsha au kuchoma tu(unaweza kutumia viungo lakini mafuta hapana)
2-maji au soda water: kunywa sana
3-chai au kahawa: kunywa bila ya maziwa wala sukari
4-multivitamin-kila siku kidonge kimoja
Hutakiwi kutumia chakula chochote zaidi ya hivyo vilivyotajwa


.....Hapo mna maoni gani??
 
Kwa hakika ukifuata ushauri huo utaendelea kupungua uzito hadi pengine ufe.
Unahitaji kurejea au kuitafuta elimu ya lishe bora itakayokuelimisha kuhusa makundi matatu ya chakula yaliyo lazima na uwiano wa kuyala - kulingana na shughuli zako.
Jihadhari na wanaohamasisha njia za mkato.
 
ingia kwenye web ya 50cent, utona jinsi alivyopungua kwa kutumia diet liquid na mambo mengineyo
 
The following rules will help you achieve the weight loss and fat burning you want.
1. Drink lemon juice with warm water every morning. Starting the day with the juice of a lemon in a glass of warm water will stimulate your digestive system.
Water is also crucial to weight loss. Water aids healthy digestion and the elimination of waste, so make sure you drink six to eight glasses a day. Alcohol should be limited to one small glass of wine a day, and keep coffee and tea to a minimum. Avoid fizzy drinks and sweetened fruit juices.
2. Eat at least five portions of fruit and vegetables a day. All vegetables and most fruits are low-calorie nutritional powerhouses, rich in vitamins, minerals, fibre and nutrients that can boost immunity, balance hormones, calm the nervous system, aid digestion and help weight loss.
3. Balance your blood sugar levels. Irritability, poor concentration, fatigue and headaches are all symptoms of fluctuating blood sugar levels, which can make you crave sweet and fattening foods. When blood sugar levels swing too high, so does insulin. This hormone helps shuttle blood sugar (glucose) into your cells to be used as energy. In other words, it promotes fat storage.
Sprinkling lemon juice over your meal can be enough to lower the blood sugar impact by as much as 30 per cent - use it in all your cooking. Using peel in cooking helps ensure the sugar is released steadily into your bloodstream. Add peel to soups and salads, and sprinkle on fish and chicken. Lemons are also a fantastic source of fibre.
Eat protein with each meal, as it steadies your blood sugar by delaying the absorption of carbohydrates and fats. Eating five or six times a day will combat food cravings.
4. Cut down on sugar-rich foods. This give you a brief high followed by a big slump, and leave you feeling edgy and tired. Refined foods - such as white bread , white rice, instant potatoes and cornflakes - can act like sugar in your system, and end up being stored as fat. Instead, stick to whole grain, fruit, vegetables and protein.
Natural sugars in fruit can hit your bloodstream fast, so don't eat a piece of fruit without a handful of nuts or seeds to slow the impact. Beware of artificial sweeteners as they can increase sugar cravings.
5. Forgot low fat - your body needs some fat to lose weight. Unsaturated fats can help with weight loss by delaying the passage of carbohydrates into your bloodstream, keeping blood sugar levels stable and insulin down.
Avoid saturated fats - found in red meat, cakes and pastries - and trans-fatty acids in processed foods. These are low in nutrients and can increase your risk of heart disease and obesity.
Increase your consumption of omega 3 and omega 6 essential fatty acids found in nuts, seeds and oily fish, and unsaturated fat found in extra virgin olive oil.
6. Eat lots of fresh whole foods. Switch from processed to whole foods to boost your intake of the nutrients your body needs for weight loss. Whole foods such as beans, pulses and lentils also contain fibre, which stimulates the digestive system and can slow down the conversion of carbohydrates into glucose.
Best of all, whole foods are free of hidden sugar and chemicals that overload your liver, making it hard for your body to digest food and burn fat. Choose brown pasta, wholegrain bread and cereals, vegetables, fruit, fresh soups, smoothies and juices (not from concentrate), and eat a salad with every meal.
7. Slow things down. Eat slowly and chew properly. Chewing relaxes the lower stomach muscle and triggers nerve messages that activate the digestive process. If food is not properly chewed, nutrients remain locked in and undigested.
Keep portions moderate, and eat at regular times. If you find you're still hungry, wait 20 minutes for your brain to catch up with your stomach and recognise that you are full.
Your stomach and intestines are sensitive to stress. When you feel anxious, digestion will shut down, leaving food partially digested. So finding ways to manage stress is not only important for your emotional health, but your digestive health, too


Read more: http://www.dailymail.co.uk/health/article-501148/Lose-weight-Christmas-Lemon-Juice-Diet.html#ixzz0pL4Zfa00
 
watu wanatafuta unene we unatafuta wembamba...watu maisha magumu wanaona bora kama wakionekana wanene itawaficha kidogo...hapa hapa tz...
 
Mwenye Kutaka Kukonda kupunguza Uzito wa Mwili na Adumishe kula Nanaa kwa kiingereza inaitwa (Mint) na kunywa Siki ya Zabibu (vinegar) au Siki ya Apple vinegar Kijiko Kimoja Kabla ya kula Kitu na kabla ya kulala Usiku basi kwa Uwezo wake Mwenyeezi mungu atapunguwa Uzito mwilini mwake .
 
Maziwa ya mgando ni 'dawa' kupunguza unene Friday, 21 January 2011 20:52

Florence Majani

UTAFITI mpya umegundua kuwa, bakteria wanaopatikana katika maziwa ya mgando, mtindi na uji uliochacha vinaweza kufanya kazi mara mbili zaidi ya inayofanywa na vituo vya mazoezi (gym).

Matokeo ya utafiti huo yamekuja wakati mamilioni ya Watanzania wakihangaika kutafuta dawa na kufanya mazoezi ya aina mbalimbali ili kupunguza unene na uzito wa miili yao.

Utafiti huo uliotolewa hivi karibuni unaonyesha kuwa, bakteria rafiki, aitwaye ‘lactobacillus’ anayepatikana katika maziwa ya mtindi na vitu vingine vilivyochacha anao uwezo wa kupunguza unene na uzito kupita kiasi (obesity) na huzalisha kinga ya kuyeyusha mafuta ya ziada mwilini.

Dk David Mwaniki, Mwanasayansi kutoka Taasisi ya Utafiti ya nchini Kenya, alisema kuwa tangu mwaka uliopita wa 2010, wanasayansi wamejitahidi kuonyesha jinsi bakteria hao wanavyoweza kufanya kazi ya kumeng’enya mafuta katika mwili wa binadamu.

“Ninaamini kuwa, hii ni sehemu ya utafiti ambayo italeta mapinduzi katika kudhibiti fetma (obesity), vilevile jinsi virutubisho vyake vinavyofanya kazi nyingine za ziada,” alisema Mwaniki, ambaye taasisi yake imeonyesha hamasa ya kufanya utafiti kuhusu aina hiyo ya bakteria.

Wanasayansi hao walisema kuwa, watu wanaotoka katika jamii ambazo maziwa ya mtindi au uji ni sehemu ya mlo wao huwa wembamba kwa miili yao kutokana na aina hiyo ya bakteria.

"Wale wanaotumia maziwa ya mgando mara kwa mara au kwa muda mrefu wako katika nafasi ya kuwa na miili isiyo na mafuta pamoja na kupunguza kasi ya kushambuliwa na magonjwa yanayosababishwa na viumbe mbalimbali," alisema Mwaniki.

Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Tiba (NIMR), Dk Charles Massaga alisema, hana taarifa rasmi kuhusu utafiti huo, lakini akasema anakusudia kufuatilia kwa karibu ili ikiwezekana jopo la watafiti wa hapa nchini nao wachunguze kwa undani kama kweli maziwa ya mtindi yana uwezo huo.

“Kwa sasa sina taarifa kama kweli, maziwa ya mtindi yana uwezo wa kupunguza mafuta mwilini kama mnavyodai, lakini kwa kuwa habari kama hizo ni za msingi kwa watafiti kama sisi, hatuna budi kuzifanyia kazi kuanzia sasa,’ alisema Dk Massaga.

Dk Massaga alisema kama bakteria hao wanaopatikana katika maziwa ya mtindi wana uwezo wa kufanya kazi kama zilivyotajwa na wanasayansi hao itakuwa ni moja kati ya tiba nyepesi na zisizo na gharama kubwa.

“Kama kweli bakteria wanaoishi katika maziwa ya mtindi wana uwezo wa kupunguza uzito, kuzuia maambukizi mbalimbali, wakati huo huo bado ikawa ni sehemu ya lishe tena ipatikanayo kwa urahisi basi itakuwa ni moja ya tiba za gharama nafuu na za muhimu,” alisema.

Dk Massaga aliongeza kwa kusema, kama nchi za Afrika zimeweza kuwa na wanasayansi wenye uwezo mkubwa kiasi hicho basi Afrika inatarajiwa kuwa tishio katika wakati huu ambapo sayansi na teknolojia ndiyo msingi wa kila kitu.

Hata hivyo, utafiti mwingine kama huo uliofanywa hivi karibuni na Profesa Jeremy Nicholson kutoka Chuo Kikuu cha Imperial nchini Uingereza unaonyesha kwamba, bakteria aina ya lactobacillus wana uwezo wa kupunguza kiasi cha mafuta kilichonyonywa na mwili, hivyo kuondoa uwezekano wa kupata fetma au unene kupindukia.

Kwa mujibu wa profesa huyo, bakteria hao muhimu huweza pia kuweka makazi katika uke na utumbo, kisha kuteketeza wadudu waharibifu wanaojulikana kisayansi kama ‘probiotics’.

Probiotics ni viumbe hai wanaosaidia kuimarisha mmneng’enyo wa chakula, kudhibiti vijidudu vya maradhi katika utumbo mpana, kuzuia ukuaji wa bakteria wenye madhara na kuongeza nguvu ya kinga ya mwili.

Utafiti huo unaeleza kuwa bakteria hao, wana uwezo wa kuimarisha kinga ya mwili na kumpa mwanadamu maisha yenye afya.

Dk Mwaniki alisema utafiti wa Profesa Nicholson na wenzake umeongeza vipengele muhimu katika vimelea hivyo vya probiotics ambavyo ni kuimarisha afya kwa watoto na watu wengine, hasa katika ugonjwa hatari wa Ukimwi.

Alisema bakteria hao (lactobacillus) wana uwezo mara mbili wa kuzuia kuharisha na kuzuia maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa watoto.

“Tumegundua kuwa, lactobacillus wana uwezo wa kubadilisha mimea midogomidogo katika utumbo na kuwafanya bakteria wanaosababisha madhara kwa watoto hata watu wazima wasiishi” alisema Dk Mwaniki.

Aliongeza kuwa: “cha kufanya kwa sasa, ni mataifa kuweka mipango ya kuwaongeza bakteria hao na kuanzisha sheria za nchi ambazo zitaonyesha jinsi watakavyotumika kama sehemu ya mlo ili kuimarisha afya za watu.”

Mbali na tafiti hizo utafiti mwingine uliofanywa hivi karibuni na Taasisi ya Taifa ya Afya nchini Marekani,(ANIH) umeonyesha kuwa bakteria wa probiotics wana uwezo wa kuzuia maambukizi ya VVU kwa watoto wakati wa kunyonyesha.

Wakati huo huo watafiti hao walisema, wanawake wenye kiasi kidogo cha asidi katika mazingira ya uke wana nafasi kubwa ya kupata maambukizi ya VVU kwa urahisi ukilinganisha na wale ambao sehemu zao hazina tatizo hilo.

Takwimu za utafiti huo zinaonyesha kuwa, asilimia 78 ya wanawake wasio na tindikali ya kutosha katika uke wanaweza kuambukizwa maradhi kwa haraka na kwamba tiba ya tatizo hilo ni kuongeza bakteria wa lactobacillus.

Habari zinasema, wanasayansi wanaendelea kushawishika kuwa matumizi ya bakteria wasio na madhara huenda ikawa ni njia nyepesi ya kuzuia maambukizi, kwa kuwaongeza bakteria hao katika vyakula kama maziwa, mtindi, sukari au hata unga tangu viwandani wakati wa uzalishaji.

 
Back
Top Bottom