Dawa gani ya meno ambayo ukitumia hiyo kusukutua siku zote hautang'oa meno kabisa?

Utaendelea kung'oa meno hadi pale utakapoanza kula vyakula vyenye calcium kwa wingi kama vile maziwa,soya e.t.c!.....Hakuna dawa ya meno yenye uwezo wa kuzuia meno kung'ooka!.....Achana na chips,anza kula vyakula vyenye tija na afya yako!
We, Soya kwa wanaume inapunguza nguvu za kulima!
 
Uimara wa meno si dawa za kusukutua ila usafi:

Safisha meno kila baada ya kula chakula kwa:
1) kusukutua kwa maji
2) kupiga mswaki kwa kwenda juu na chini, ndani na nje ya meno kinywani
 
DFP dental formula power.nilitumia mwaka 2009 nikarudia 2010 mpaka leo jino halijauma tena
 
DFP dental formula power.nilitumia mwaka 2009 nikarudia 2010 mpaka leo jino halijauma tena
 
colgate.jpg


So, je uko salama, je dawa ya meno unayotumia haina kiambata hiki kinachosababisha cancer. By the way, Colgate walifanya utafiti miaka kumi ku-develop hiyo ingredient, na wakaiingiza kwenye dawa ya meno ambazo zilikuwa marketed kwenye zaidi ya nchi 100 kabla ya kuomba kukubaliwa kuingiza kiambata hicho kwenye dawa za meno zinazouzwa Marekani. Lakini, kwenye story pia kunaonekana udhaifu wa FDA ya Marekani ambayo inategemea ushahidi wa kisayansi wa kampuni za kibiashara kujua iwapo ingredient zina madhara kwa binadamu ama vinginevyo.

Kwa mujibu wa repoti ya Bloomberg, Colgate Total inayotengenezwa na kemikali moja inayojulikana kama triclosan inadaiwa kuongeza cells za kansa mwilini. Mamlaka ya kudhibiti vyakula na Madawa Tanzania (TFDA) imesema inafahamu kuwepo kwa hiyo ripoti na tayari imeshaagiza wataalamu wake kuifanyia kazi kabla ya kujua hatma ya dawa hiyo ya meno.

TFDA imeongeza kuwa Colgate Total imekubaliwa kutumika nchini baada ya mamlaka hiyo kuifanyia majaribio na kukuta kuwa ina kiasi cha asilimia 0.3 za triclosan ambazo hazina madhara ya kiafya kwa binadamu. TFDA imeongeza kuwa kiwango hicho cha asilimia 0.3 za triclosan kwenye Colgate Total zinafaa kwa matumizi ya binadamu wenye umri wa kuanzia miaka 12 na kuendelea.

Kwa mujibu wa The Citizen, Colgate Total inauzwa katika supermarkets na maduka mbalimbali nchini. Colgate Palmolive ambao ni watengenezaji wa colgate hapa nchini wamesema kuwa Total Colgate haina madhara kiafya, huku waki-cite mchakato wa FDA ya Marekani iliyofanya kabla ya kuidhinisha Total Colgate mwaka 1997.

Hata hivyo, kwa mujibu wa ripoti ya Bloomberg, mchakato wa maombi ya kuidhinishwa kwa dawa hiyo unaonyesha kuwa matokeo ya tafiti za kisayansi yaliyotumika kuonyesha usalama wa triclosan kwenye dawa hiyo hayakuwa ya moja kwa moja. Pia matokeo ya tafiti hizo yamewekwa hadharani mwaka huu pamoja na kuwa tafiti zilifanyika miaka kibao iliyopita.

FDA ya Marekani iliidhinisha dawa hiyo kutumia tafiti zilizodhaminiwa na kampuni inayomiliki dawa hiyo. Maombi ya kuidhinisha dawa hiyo yalikuwa na kurasa 35 zikijumuisha tafiti za ki-toxicology juu ya triclosan. FDA imeweka mchakato huo wa maombi kwenye tovuti yake kutokana na kesi iliyofunguliwa over a Freedom of Information Act request. Bloomberg News ilipofanya follow-up, FDA wakaamua kuweka mambo yote hadharani.
Chanzo: TheCitizen
 
Sensodyne inatumika kwa mtu mwenye sensitive teeth problems

Ukitaka using'oe jino hakikisha unabrush meno yako kila baada ya chakula hususani sugary foods

Ukiacha sugary remnants kwenye meno,bacteria huziferment na kutengeneza organic acids ambazo zikireact na kalsiam kaboneti ya kwenye jino hulivunja na kulitoboa (dental caries)

Tundu likifikia kuexpose pulp kwenye hewa ndio maumivu yanaanza inabidi ukazibe au ufanye extraction

Ushauri wangu:Tubrush meno kila baada ya chakula hususani cha usiku na chenye sukari
Tusafishe meno kwa kutumia zile nyuzi ambazo husafisha hadi sehemu brush haiezi fika (dental floss)
Tupende kutumia toothpaste zenye triclosan au triclocarban
Tupende kutumia sana cloves husaidia ulinzi wa meno
 
Salaam
Wandugu, kila siku asubuhi tunasukutua meno kwa kutumia dawa, lakini bado tunaugua meno kiasi cha kutupelekea kuyang'oa, je ni dawa gani ya meno ambayo ukitumia hiyo kusukutua siku zote hautang'oa meno kabisa?
Usitumie dawa yoyote ya Mswaki dawa ya kizungu na wala Mswaki wenyewe Tumia njia yangu ya asili itaweza kukusaidia ukifuata ushauri wangu hutoweza kung'oa meno tena na

meno yako yatakuw ani meupe. Fanya hivi ununuwe Mswakiwa kijiti nenda Sehemu zamiisikiti wanauza hiyo Miswaki ya kijiti ndio uwe unatumia kupigia
mswaki kila siku asubuhi na pasipo na kuweka Dawa ya aina yoyote ile. na ikifika kila baada ya siku 7 Tumia njia hii hapa chini kusafisha meno yawe masafi


Namna rahisi ya kung’arisha meno yako

Namna ya kuandaa:




    • Chukua limau kubwa moja ikate katikati, chuja kupata maji maji yake (juisi) kisha changanya Magadi Soda Chapa ya Simba ya unga kijiko kidogo kimoja cha chai. Changanya vizuri mchanganyiko huo.
    • Sukutua kinywa chako vizuri ukitumia mswaki na huo mchanganyiko ndiyo iwe dawa yako ya meno. Sukutua (piga mswaki) taratibu kama dakika 3 hadi 5 hivi na mwisho jisafishe kinywa na maji safi.
Mhimu: Fanya zoezi hili nyakati za jioni au usiku unapokaribia kwenda kulala na ufanye mara moja tu kwa wiki na si zaidi ya hapo kwani unaweza kuharibu fizi zako kwa dawa hii usipokuwa makini. Ukifanya hivi mara 4 yaani mwezi mmoja utaona tayari meno yako yameanza kuwa meupe na yanayong’aa na kupendeza.

Tooth_stick_cover.jpg

Mswaki wa asili wa kijiti.

MAGADI SODA CHAPA YA SIMBA.jpg

Magadi Soda Chapa ya Simba

limau.jpg

Limau
 
Back
Top Bottom