Dawa gani ya asili (herbal) ulishawahi kutumia ikakusaidia?

Author

JF-Expert Member
Jan 24, 2014
1,709
8,007
Habari wana JF,

Duniani siku hizi kuna maradhi mengi sana, na changamoto kubwa imekuwa jinsi ya kupata tiba sahihi (hasa za asili) kwenye tatizo lako. Japo kwenda hospitali ni muhimu ili kucheki afya yako na kufahamu maradhi yanayokusumbua lakini tiba za asili (mizizi,majani,matunda,mbegu n.k) zimethibitishwa kuwa msaada mkubwa kwenye maradhi mbalimbali.

Binafsi nimetumia sana mmea wa Alovera (una majina mengi kulingana na unapotoka) na ulinisaidia sana kwenye kutibu homa,Malaria, na hata kupaka kwenye ngozi iliyoathiriwa na fangasi (fangasi za katikati ya vidole zilinisumbua sana). Utaratibu ni kuchemsha na maji safi kisha unaacha ipoe,unakunywa kikombe kimoja asubuhi na jioni.

Wadau karibuni tujumuike ili wengine wanaopitia changamoto za maradhi mbalimbali waweze kuelimika.

ANGALIZO: Ni muhimu kwenda keenye kituo cha afya kupima kujua unasumbuliwa na nini kabla ya kuanza kutumia dawa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunadhani hii inaweza kuwa tiba ya hili janga?
IMG-20200402-WA0024.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilishawai kutumia mchanganyiko wa maziwa mtindi na mafuta ya nazi + maji ya alovera kutibu fungus sugu eneo la siri.
Nusu kikombe cha mtindi nilikuwa nachanganya na kijiko kimoja cha mafuta lakini kabla yakupaka nilikuwa napaka Kwanzaa maji ya alovera naacha eneo lipigwe na upepo kama dakika 15 hivi ukipaka Alvera unawashwa sana na kama kunawaka moto hivi kwaiyo baada ya dakika 15 nilikuwa nachukua maji vuguvugu nakausha eneo kwa kitambaa safi then baada ya hapo ndio nachukua mchanganyiko wa mtindi na mafuta napaka eneo la siri napaacha wazi hivo mpaka asubuhi. Nilitumia hivi kwa 10 days nikapona.
 
Hiyo sehemu ya Siri ni ya ke au me?
 
Kuna kimbegu flani cha kutoa uchafu mwilini, ukila unaendeshaaa mpaka mwili una factory reset ,,wadau mnikumbushe kinaitwaje
Nilikuwa mbishi nikisema mie huwa siendeshi hovyo hovyo hata iwe dawa. Jamani jamani nikapewa kamoja tu
Nilitapika na kuendesha mpaka nikahisi iziraili ananinyemelea. Hizo mbegu hapana
 
Back
Top Bottom