Dawa aina ya (valium) zitolewe kwa kibali maalum

Shin Lim

JF-Expert Member
Mar 27, 2012
7,593
13,763
Sina hakika kama hizo ndio spelling zake, ila wenyewe ndio wanatamka hivyo.

Vibaka wengi na wenye mwonekano wa kiteja wanazitumia hizo dawa kama dawa za kulevya.
Unajua wanafanyaje?
Hizo dawa wanazisaga, wanazimix na ganja kisha wanavuta. Hapo akikunyanyulia panga, lazima alishushe.

Kama mtaani kwako ulisikia kuna mtu alijeruhiwa na kibaka na kunyang'anywa simu, basi ujue alikutana na huyu aliyechanganya valium na ganja. Ni kwamba yeye akipigwa anakuwa hasikii maumivu yaani kwa kifupi anakuwa amedata.

Faida nyingine wanasema huwa wanalala usingizi mtamu sana, yaani wanahisi dunia yote ni yao. Kibaya zaidi wanaotumia hayo madude ni hawa watoto wa under 20, sisi tuliovuta bangi enzi hizo hatukuyajua haya.

USHAURI:
Hizi dawa ziuzwe kwa kibali maalum cha daktari, zisinunuliwe kama vocha.
 
!
!
vijana wa siku hizi huwa wanajaribu sana aisee....kuna wengine wamejaribu na kufanikiwa kuwa hadi mashoga tayari.
 
Du! mleta uzi kumbe ulishawahi kuvuta bhangi! nasikia pafu moja tu haliishi mwilini hadi miaka saba, kwa hiyo na wewe hapo ulipo umejaa bangi mwilini! Kama bado unatafuta ajira usije ukathubutu kuomba nafasi ya polisi maana siku hizi CCP wanakifaa mkienda depo wanapima hata kama ulivuta ulivyokuwa na miaka minne pafu moja tu kifaa kinaread hapo sasa ndio unakuwa umegraduate upolisi kabla ya wakati
 
Kweli tupu!
Shule niliyosoma o-level wanafunzi waliitumia dawa hii kama kilevi, wakikosa walikuwa wakitumia ugoro na ilikuwa na wasichana kwa wavulana.
 
Hizo valium zinauzwa kwenye pharmacy zetu nikanunue?
zipo, vijana huwa wanasagia kwenye bangi na nyingine wanakunywa kama wagonjwa.
Ile alosto inaisha na mwili unapata ganzi wanavyosema wao.
 
Madawa yenyewe ya kulevya kama marijuana, heroin, cocaine, amphetamines hayauzwi hata kwa kibali chochote lakini bado watumiaji wake wamezagaa nchi nzima. Sembuse hizo valium zitakazonunuliwa kwa kibali maalumu?
 
Hizo valium zinauzwa kwenye pharmacy zetu nikanunue?
aisee usinunue kuna chalii hapa jirani alitumia na bangi si akaenda nyumbani kwao yaani tulishtukia kondoo wako juu ya bati wameshavunjwa hadi miguu........

ila kesho yake tulimchapa fimbo sabini na kwa sasa amenyooka!
 
Hazina madhara kwa kiwango hicho unachosema hao vibaka ni bangi tu ndio inawaharibu
Kama hujui chochote bora ukae kimya, kuna best yangu alitumia hii kama dawa ya kulevya, alinipa story jinsi zikivyompa stimu.
Hata piliton zinatumika dizaini hii.
 
aisee usinunue kuna chalii hapa jirani alitumia na bangi si akaenda nyumbani kwao yaani tulishtukia kondoo wako juu ya bati wameshavunjwa hadi miguu........

ila kesho yake tulimchapa fimbo sabini na kwa sasa amenyooka!
Hahaaaaaa. Mimi situmii bangi. Nataka tu kuitumia kama dawa ya kutibu
 
Kama hujui chochote bora ukae kimya, kuna best yangu alitumia hii kama dawa ya kulevya, alinipa story jinsi zikivyompa stimu.
Hata piliton zinatumika dizaini hii.
Mimi ni taaluma yangu ambayo nimesomea kwa zaidi ya miaka mitano kwa hiyo wewe ndiyo ukae kimya kama huna swali
 
Mimi ni taaluma yangu ambayo nimesomea kwa zaidi ya miaka mitano kwa hiyo wewe ndiyo ukae kimya kama huna swali
Basi ni kilaza kwenye taaluma yako, hiyo kitu ukiitumia unatoa hadi udenda na unalala ukiwa umekaa. Itakuwa unachukua certificate UDOM ww.
 
Back
Top Bottom