Davos: World Economic Forum Annual Meeting

Kuanzia kesho Januari 22, 2019 hadi Ijumaa tarehe 25, viongozi mbalimbali kutoka jumuia ya kimataifa, viongozi wa kiserikali, viongozi wa taasisi zisizo za kiserikali, viongozi watendaji wa mashirika makubwa duniani, wanasayansi, na watu wengine wa kila aina ya kada watakutana huko Davos, Switzerland katika mkutano wa mwaka wa jukwaa hilo la kiuchumi duniani.

Ushiriki wake huwa ni wa kualikwa. Kwa hiyo kama hujaalikwa, huwezi ukajipeleka tu na kushiriki.

Kipindi cha awamu ya tatu na nne, marais wetu walishiriki shiriki kiasi chake.

Niliwahi kumwona Benjamin Mkapa kwenye moja ya hiyo mikutano. Pia Jakaya Kikwete alikuwa akishiriki.

Lakini tokea awamu ya 5 iingie madarakani, sijawahi kumwona mwakilishi yeyote yule kutoka serikali ya Tanzania.

Kwa mwaka huu sijui kama tutawakilishwa tena.

Ingependeza kama nasi tungekuwa na mwakilishi wetu huko Davos.

Wewe mwananchi unaonaje? Funguka...
Kama Museveni atakuwepo, nashauri Magu audhurie na wakae karibu
 
Angetuma hata mwakilishi, sio vyema tukio kubwa kama hili kutokupewa umuhimu unaostahili.
 
Hatuhitaji urafiki na mabeberu sisi aka wizi wa rasirimali zetu..
Huo mkutano ni wamabeberu wakiwa na mkuu wa mabeberu USA hautuhusu sisi..

Sisi tunabaki Tanzania kuchapa kazi tu na kuijenga Tanzania.
Huku tukizinunua ndege kutoka kwao,na zingine mbovu.Yaani wanazidi kutupiga tuuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
USA ni beberu mwenzao wanajuana hao mabeberu wanachuzea akili tu, JPM piga kazi achana na hao mabeberu kwanza wameiba sana rasirimali zetu hao, hii ni vita ya kiuchumi na kuna siku tutawapa misaada wote hao na hivyo vikao watakuja kuvifanyia Dodoma.
Mbaya zaidi wanazidi kutuibia tu kwa kutuuzia madege mabovu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuanzia kesho Januari 22, 2019 hadi Ijumaa tarehe 25, viongozi mbalimbali kutoka jumuia ya kimataifa, viongozi wa kiserikali, viongozi wa taasisi zisizo za kiserikali, viongozi watendaji wa mashirika makubwa duniani, wanasayansi, na watu wengine wa kila aina ya kada watakutana huko Davos, Switzerland katika mkutano wa mwaka wa jukwaa hilo la kiuchumi duniani.

Ushiriki wake huwa ni wa kualikwa. Kwa hiyo kama hujaalikwa, huwezi ukajipeleka tu na kushiriki.

Kipindi cha awamu ya tatu na nne, marais wetu walishiriki shiriki kiasi chake.

Niliwahi kumwona Benjamin Mkapa kwenye moja ya hiyo mikutano. Pia Jakaya Kikwete alikuwa akishiriki.

Lakini tokea awamu ya 5 iingie madarakani, sijawahi kumwona mwakilishi yeyote yule kutoka serikali ya Tanzania.

Kwa mwaka huu sijui kama tutawakilishwa tena.

Ingependeza kama nasi tungekuwa na mwakilishi wetu huko Davos.

Wewe mwananchi unaonaje? Funguka...

Ni kweli Benjamin Mkapa na Jk walishiriki mikutano hiyo...Kualikwa kwao kkulikuwa na maana kubwa...Ben Mkapa alikuwa mstari wa mbele kutekeleza conditionalities za donors na International Financial Institutions (IFIs) kwa maana ya IMF na World Bank kwa kulegeza masharti mbalimbali ya kibiashara ikiwa ni pamoja na kuuza mashirika ya umma na kadhalika na kadhalika na ambao ni utekelezaji wa neo-liberal policies na ambazo kimsingi hazikutusaidia sana kiuchumi...Ni katika utawala wa Mkapa ndipo tulishuhudia mikataba ya madini ikitiwa saini na makampuni ya madini yakiingia nchini kuchinmba madini na kuchota kiasi kikubwa na sisi kubakiwa na kiduchu...ni wazi uncle Ben alikuwa ni 'mtu muhimu' kwa mataifa makubwa...Naye comrade Jk aliendeleza yale ya uncle Ben kwa kuleta makampuni mengi ya nje kufanya biashara hapa ndani na kukuza uhusiano kati yetu na Marekani...comrade Kikwete ni mwanadiplomasia mzuri na hakuwa na bughudha kwa 'wazungu'....Wote wawili yaani uncle Ben na comrade JK walikuwa na mtazamo kuwa ili Tanzania isonge mbele kiuchumi na kimaendeleo kwa ujumla ni lazima Tanzania ipate misaada na uzoefu na pia teknoljia kutoka nje...waliamini kuwa investments in our country should flow from the outside...But now in Tanzania we have a new sherrif in town in the name of Dr. JPM...Huyu ana mtazamo tofauti na hao wawili waliomtangulia...Yeye anaamini kuwa ili Tanzania isonge mbele ni lazima ikusanye uwezo wake wa ndani kwa maana ya capital accumulation from within...JPM anaamini kwamba hakuna taifa lililoendelea kwa kutegemea misaada kutoka nje..JPM anaamini katika utendaji kazi wa ndani, kukusanya kodi, kuondoa bureaucracy au urasimu, kupambana na wizi na ufisadi wa mali ya umma, kutumia vizuri raslimali zilizopo nchini...Yaani anachotaka JPM ni kupigania inward looking policies na kuhakikisha kuwa profit na surplus inayopatikana nchini ndiyo itakayoweza kuleta maendeleo...JPM anaamini kuwa Tanzania ni tajiri na kwamba ni lazima au umefika wakati watanzania wakatambua kuwa ni wao wenyewe ndiyo watakaojiletea maendeleo na siyo misaada kutoka nje ambayo mara nyingi ina masharti...In my opinion Tanzania ilichelewa kumpata mtu kama JPM...anafanana na JKN (Julius Kambarage Nyerere) kwa namna fulani.

Lakini anayofanya JPM hayawezi kuwafurahisha wazungu kwani wao huwa hawapendelei kiongozi wa Afrika mwenye msimamo katika kulinda raslimali za nchi na mwenye mtazamo wa kuleta maendeleo ya nchi na ku-downplay role ya donors na makampuni ya nje katika kupenyeza mirija ya unyonyaji...Kwa hiyo JPM kamwe hawezi kuwa 'dear/darling son' kwa nchi za magharibi...nitashangaa kama ataalikwa huko Davos... ...
 
Kuanzia kesho Januari 22, 2019 hadi Ijumaa tarehe 25, viongozi mbalimbali kutoka jumuia ya kimataifa, viongozi wa kiserikali, viongozi wa taasisi zisizo za kiserikali, viongozi watendaji wa mashirika makubwa duniani, wanasayansi, na watu wengine wa kila aina ya kada watakutana huko Davos, Switzerland katika mkutano wa mwaka wa jukwaa hilo la kiuchumi duniani.

Ushiriki wake huwa ni wa kualikwa. Kwa hiyo kama hujaalikwa, huwezi ukajipeleka tu na kushiriki.

Kipindi cha awamu ya tatu na nne, marais wetu walishiriki shiriki kiasi chake.

Niliwahi kumwona Benjamin Mkapa kwenye moja ya hiyo mikutano. Pia Jakaya Kikwete alikuwa akishiriki.

Lakini tokea awamu ya 5 iingie madarakani, sijawahi kumwona mwakilishi yeyote yule kutoka serikali ya Tanzania.

Kwa mwaka huu sijui kama tutawakilishwa tena.

Ingependeza kama nasi tungekuwa na mwakilishi wetu huko Davos.

Wewe mwananchi unaonaje? Funguka...
Mwenda bure sio sawa na mkaa bure...ingependeza
 
Back
Top Bottom