Davis Mosha, Makamu Rais Yanga apigana Uwanjani Tanga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Davis Mosha, Makamu Rais Yanga apigana Uwanjani Tanga

Discussion in 'Sports' started by Reyes, Oct 25, 2010.

 1. R

  Reyes Senior Member

  #1
  Oct 25, 2010
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 188
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Amakweli Yanga imechagua wahuni kuongoza, Yanga ya sasa imevamia na wahuni ambao wanaharibu jina zuri la klabu yetu, Jana nilijivinjari uwanja wa Mkwakwani Tanga, nilishuhudia timu yangu ya Yanga ikitoka sare na Azam FC.

  Baada ya Mchezo kuisha Davis Mosha alienda upande ambao Azam FC walikuwa wamekaa, akamuuliza kijana mmoja ambaye sijamtambua jina lake, "Na wewe Azam FC siku Hizi?" yule kijana akajibu mimi napenda mpira siyo sifa na Azam FC ndiko kwenye mpira wa kweli. Jibu lile lilimuudhi Mosha na kama mtu aliyepagawa akaanza kushusha makonde na Matusi kwa yule kijana

  Watu walioshuhudia tukio lile wakapigwa na Butwaa, iweje kiongozi wa Hadhi ya Mosha apigane hadharani? pia wakajiuliza, hivi Mosha ana akili sawasawa?

  Jamaa mmoja pale uwanjani akasema, eti hata kule kupigwa kwa Ndimbo na Mtawale wakihusishwa na imani za kishirikina Mwanza kulishawishiwa na Mosha, Alikuwa ni mosha aliyewachochea mashabiki wa Yanga wawapige akina Ndimbo halafu Mosha akakimbilia kupiga simu vituo Vya Redio kutangaza lile tukio.

  Kifupi Mosha ni Mchochezi, Mzushi, Mhuni, na Mwehu, haiwezekani klabu kubwa kama Yanga kuongozwa na Mtu mwenye Tabia za Mosha kwani ipo siku atasababisha maafa kwa kuwachochea Yanga kufanya Fujo viwanjani

  MOSHA JIREKEBISHE
   
 2. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #2
  Oct 25, 2010
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,547
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  leta ushahidi . sio mnagombana huko mtaani kiaina unakimbilia huku.
   
 3. R

  Reyes Senior Member

  #3
  Oct 25, 2010
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 188
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Katika pitapita yangu kwenye Google kusaka ushahidi kama media zimeripoti nimekutana na hii kwenye Facebook Page ya Azam FC

  Matokeo ya mwisho Azam FC 0-0 Yanga, Azam FC imecheza soka la hali ya juu Yanga SC ilikuwa hoi dakika zote lakini uchezeshaji mbovu wa Mwamuzi na ubovu wa uwanja wa mkwakwani uliwaathiri Azam FC Lakini Samba la Itamar Tumeliona

  Davis Mosha makamu mwenyekiti wa Yanga kapigana uwanjani, ni aibu kubwa kwa kiongozi wa hadhi ya Mosha kupigana uwanjani

  Azam FC | Facebook
   
 4. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #4
  Oct 25, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Duh jamaa ana jazba!!!!!!!!!!!!!
   
 5. NG'OTIMBEBEDZU

  NG'OTIMBEBEDZU JF-Expert Member

  #5
  Oct 25, 2010
  Joined: Aug 11, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Si akapigane na Manji ili amlipe Papic malimbikizo ya mshahara wake!!
   
 6. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #6
  Oct 25, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,007
  Trophy Points: 280
  huyo kiongozi ni zao la Riz 1 Kikwete, ndio aliyemuweka pale kinguvu baada ya kuuvuruga uchaguzi wa Yanga
   
 7. BASIASI

  BASIASI JF-Expert Member

  #7
  Oct 25, 2010
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 3,111
  Likes Received: 345
  Trophy Points: 180
  umbea udaku hapa si mahali pake change ur channel
   
 8. MTWA

  MTWA JF-Expert Member

  #8
  Oct 25, 2010
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 1,024
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Kwa kifupi mimi nilikuwa uwanajni jana na tukio lilitokea,
  Kwa kifupi mashabiki na viongozi wa Yanga wanahitaji kujifunza sana.
  jana ni matusi kila wakati, matusi makubwa kwa kitu kidogo tu, kila mwanayanga (except very few) walikuwa wamekaa kishari na si kushangilia
  Hii ni tofauti kabisa (japo mimi si mwanamsimbazi) Kwa Simba- kulikuwa na watu wakishamngilia all the time. lakini kwa yanga tofauti kabisa, Matusi na vitisho all the time, na mijitusi kibao.

  Anyway ni mambo ya kibongo sana, lazima tujifunze. otherwise mpira wetu utaendelea kuwa wa kibabaishaji, maana hata mashabiki nao wana nafasi yao kuwahamasisha wachezaji. na siyo kuwatusi pale wanapokosea na sifa kiduchu wanapopatia.

  nashangaa kwa wachezaji waliotoka Yanga pia, japo hawakufanya kosa lolote, mda wote mashabiki wameishia kuwatukana sana! Toafauti na wenzetu wanapokuwa na appreciation kwa wachezaji waliowaletea heshima dimbani kwao.

  Kwa kifupi mashabiki hasa wa YANGA lazima tubadilike tuwe wastaarabu, tukiongozwa na viongozi wetu
   
 9. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #9
  Oct 25, 2010
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Acha unafiki ndugu yangu, hebu jaribu kuwa mkweli kidogo tu, hao wenzetu ni kina nani? si unazungumzia ulaya bila shaka.

  Hebu niambie kama washabiki wa everton wanampokeaje wayne rooney, niambie washabiki wa arsenal wanavyompokea adebayor, niambie mashabiki wa mani yuu wanavyompokea tevez, niambie mashabiki wa aston villa wanavyompokea gareth barry.

  Kwenye mpira hilo ni jambo la kawaida sana, sio bongo tu. Labda issue hapa ni mosha kupigana, lakini la kuzomeana na kutukanana sio habari kabisa kwenye mpira duniani kote.
   
 10. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #10
  Oct 25, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280

  hahaa umeniwahi mkuu nilitaka kusema hivo hivo
   
 11. m

  mosesk Member

  #11
  Oct 25, 2010
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ushahidi wa kutoka Azam hauwezi ukawa ushahidi huru, hivyo hakuna ushahidi bali ni porojo na uongo tu.

  Ni sawa sawa facebook ya CCM haiwezi kumuandika vizuri Dr. Slaa sawa sawa vile vile Facebook ya CHADEMA haiwezi kumuandika vizuri JK.

  Hapo haueleweki ina maana vyombo vya habari vyote havikuwepo? mbona hakuna taarifa hiyo.
   
 12. MTWA

  MTWA JF-Expert Member

  #12
  Oct 25, 2010
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 1,024
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Kama utakuwa makini hao wote uliowataja walishaonesha tabia mbovu kabla au baada ya kuondoka,

  lakini Mashabiki wetu wamezidi sana hadi watu tunakaa hatuna amani bwana, mpira ni urafiki na siyo kama vile. yaani mda wowote unaweza kutoka ngeu!
  Sisi hatuna ushabiki wa Kujenga lazima uwe muwazi!
   
 13. MTWA

  MTWA JF-Expert Member

  #13
  Oct 25, 2010
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 1,024
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  labda kama mimi, niseme kuwa hiyo haikunifurahisha mwenyewetu,
  na kama maoni ya shabiki lazima tuwe na ushangiliaji wa kujenga haiwezekani mchezaji wa kwetu basi anakosea halafu mijitusi kibao!
  Sasa tunajenga au? lazima tuwape moyo hiyo haikuwa hivyo pia hadi tugomnbane sisi kwa sisi
   
 14. Belo

  Belo JF-Expert Member

  #14
  Oct 25, 2010
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 11,280
  Likes Received: 4,286
  Trophy Points: 280
  Simba bana mbona KADUGUDA haya yalikuwa mambo ya kawaida kwake
   
 15. N

  Nasolwa JF-Expert Member

  #15
  Oct 25, 2010
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,830
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  hata ulaya sio kila mchezaji anapongezwa anaporudi uwanja wa timu aliyoihama. Mechi ya kwanza aliocheza ashley cole emarate akiwana na chelsea alizomewa muda wote na kuandaliwa pound bandia zenye picha yake na maneno "cashley cole".hivi huo kwa maoni yako ulikuwa ni ustarabu??? Acha hizo wewe
   
 16. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #16
  Oct 25, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Ushahidi unao utaka wewe ni upi? je Mosha hakupigana yaani mleta hoja mzushi au unataka taarifa kutoka yanga au picha Mosha akirusha makonde
   
 17. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #17
  Oct 25, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Nenda kwenye facebook ya Kikwete uone walivyo mchana watu sikuhizi wanataka fact na siyo bla bla...kwa hiyo kama wewe ni yanga jirekebisheni na siyo kuponda eti porojo tulete ambazo siyo porojo...
   
 18. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #18
  Oct 25, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  ni kweli kadugunda alikuwa na tabia hiyo hasa ukimletea ubabe lakini alikuwa si mtu wa kumfata mtu na kuanza kumtukana au kumshambulia mara nyingi utakuta kazwa halafu yeye anamaliza iwe kwa mshabikia au kiongozi mwenzake....
   
 19. g

  gutierez JF-Expert Member

  #19
  Oct 26, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 1,254
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  hahahaha eti Kaduguda ilikuwa zake kupigana,umenichekesha na umenikumbusha mbali ile pub ya kwa chichi kama sikosei pale uwanja wa taifa zamani(uhuru stadium sasa) kabla ya kuingia uwanjani au mechi kuanza ya simba ni sharti umkute Kaduguda pale anakandamiza ulabu akiwa na simba friends na makomandoo wa kiume na wa kike wa simba pale,ukisifia simba tu,utasikia lete bia usihesabu watu hesabu viti.
   
 20. g

  gutierez JF-Expert Member

  #20
  Oct 26, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 1,254
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  ndio maneno yako yanaweza kuwa na pointi kidogo kama uliondoka sio kwa ubaya hawakuzomei,ila ukitaka kuwafunga kama umewakosa wanakuzomea,eg uliona Man utd vs Ac Milan pale old trafford Beckham kaingia wakamshangilia,ila alipopiga faulo ikapaa juu kidogo wakamzomea,sambamba na Thierry Henry Arsenal vs Barca emirates stadium,nae hivyohivyo kaingia kashangiliwa alipowakosa wakamzomea,Etoo nae Barca vs Inter Milan Nou camp mechi zote mbili maana walikutana mara 4,2 ktk makundi,2 ktk nusu fainali,zote alipoingia walimshangilia sana,ila kila alipogusa mpira kutaka kuwafunga hususan ktk mechi ile ya ktk makundi ambayo Barca alishinda 2-0 walimzomea mara kwa mara,hata juzi Eduardo ilikuwa tayari Arsenal kishaongoza 5-0 hata alipofunga goli hawakumind sana,ila ingekuwa ni ktk kuwania nafasi fulani ushindi mgumu wangemzomea,ulaya watu hamnazo hawajali hata kama ulileta mafanikio ktk timu ila ukicheza vs nao wanakuzomea,Gary Neville na Cristiano Ronaldo walikuwa wote wachezaji wa Man Utd ila ilipokutana Ureno na England,Neville anamchezea rafu Ronaldo utadhani hawapo timu 1.
   
Loading...