Chiwaso
JF-Expert Member
- Oct 21, 2009
- 5,726
- 3,762
Wasanii wa Nigeria wamekua wa kwanza kwenye stori kubwa au kuvunja rekodi kadhaa kwenye muziki wanaoufanya ambapo miongoni mwa rekodi walizozivunja ni pamoja na P Square kufanya kolabo na Rick Ross, Davido na Meek Mill.
Usiku wa January 20 2016 Taifa la Nigeria limekua taifa la kwanza Afrika kwa kuvunja rekodi kupitia msanii wake ambaye ni Davido kwa kuingia makubaliano na kuwa msanii wa kwanza wa Afrika kutia saini ya record deal na kampuni ya sony music.
Sony Music Entertainment ni kampuni ya maswala ya muziki ya Marekani na dili hili inamaanisha kwamba Davido sasa hivi atakua kwenye mikono mikubwa zaidi na hata jina lake litazidi kuwa kubwa duniani kutokana na Sony ambao wamefanya kazi na mastaa kama Alicia Keys, Beyonce, Bruno Mars, Drake, Bow wow, Ciara na wengine.
Davido aliipost hii picha hapa chini na kuonyesha furaha yake kama msanii wa kwanza wa Afrika kusaini dili ya kazi na Sony Music kwa dunia akisema pia Mama yake atakua anatabasamu huko mbinguni kwa kinachotokea sasa hivi, stori yake ndio kwanza inaanza
Wasiwasi wangu sijui kama anajua mwisho wake na jamaa hawa utakuwaje?