David Tarimo naye amejitoa kamati ya Madini?

Asha Abdala

JF-Expert Member
Mar 21, 2007
1,130
44
Yule David Tarimo wa PWC naye anaelekea kutaka kujitoa. Walau huyu anastahili heshima kwa kutambua mgongano wa kimaslahi kuliko Machunde aliyesingizia CHADEMA

Kamati ya madini yageuka kama maigizo
*Mwingine aandika barua ya kujitoa
*Aliyejitoa wa kwanza, wa pili wahudhuria

* Iddi Simba ahamaki waandishi kuwako ndani

* Bomani awataka wajumbe kuweka maslahi ya taifa mbele

Muhibu Said na Mwanaid Omary

KAMATI ya Kuangalia Upya Mikataba ya Uchimbaji Madini nchini, imeanza rasmi kazi zake jana, huku wajumbe wake wawili walioomba kwa Rais Jakaya Kikwete kujitoa , wakishiriki.

Wajumbe hao, ni Peter Machunde kutoka Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) na Mkaguzi wa Mahesabu kutoka Kampuni ya Kimataifa ya Ukaguzi wa Mahesabu ya PriceWaterhouse Coopers, David Tarimo.

Hata hivyo, wakati hayo yakijiri, katika moja ya kazi zake, kamati hiyo imepanga kukutana na wenyeviti wa kamati zilizoteuliwa katika siku za nyuma kuchunguza kuhusu madini ili kupata uzoefu wao katika suala hilo, kuanzia Jumatatu na Jumanne wiki ijayo.

Kamati hizo, ni ile ya Jenerali Robert Mboma iliyoundwa mwaka 2001, ya Brigedia Mang'enya ( 2003), ya Dk Kipokola (2004) na ya Masha (2006).

Machunde alitangaza kujiuzulu wiki iliyopita kwa madai ya kukerwa na maneno ya baadhi ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ya kumtaka ajitoe katika kamati hiyo kwa madai ya kuwa na urafiki wa karibu na mmoja wa mawaziri wa serikali ya awamu ya nne.

Taarifa za Tarimo kuomba kujitoa , zilitangazwa jana na Mwenyekiti wa Kamati hiyo , Jaji Mark Bomani wakati akifungua kikao chao cha kwanza katika Ofisi za Bunge, jijini Dar es Salaam.

Akitoa taarifa hiyo, Jaji Bomani, alisema Tarimo aliwasilisha barua ya kujitoa katika kamati hiyo kama mjumbe kwa madai kwamba kampuni yake inatumiwa na baadhi ya makampuni ya madini, hivyo, ana wasiwasi ushiriki wake unaweza kuleta mgongano wa maslahi, lakini alisisitiza kuwa, atakuwa tayari kutoa ushauri utakapohitajika.

Hata hivyo, Jaji Bomani alishindwa kusoma barua ya Tarimo, baada ya mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo, Iddi Simba kumzuia asifanye hivyo mbele ya waandishi wa habari kwa madai kwamba, iwapo jambo hilo litawafikia wananchi, linaweza kuibua malumbano mitaani.

" Watupishe kwanza waandishi wa habari, tujadili sisi wenyewe, pengine baadhi yetu tunataka (Tarimo) asijitoe," alisema Iddi Simba na kuungwa mkono na Mbunge wa Msalala (CCM), Ezekiel Maige.

Kutokana na ushauri huo, Jaji Bomani aliwataka waandishi wa habari wasitangaze habari hizo kwa muda huo na badala yake wasubiri hadi kamati imalize majadiliano kuhusiana na jambo hilo, kisha mchana watapewa taarifa.

Maelekezo hayo ya Jaji Bomani, yalipingwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, aliyesema kuwa, haoni ni busara kuwaita waandishi wa habari kila baada ya kikao na kuishauri kamati iwaruhusu wakaripoti yale waliyokwishayapata kwa muda ule.

Mapema, Tarimo alikataa kuzungumza chochote alipoulizwa na Jaji Bomani kama ana jambo la kuzungumza kuhusiana na hilo na kumuomba mwenyewe (Bomani) azungumze badala yake.

Awali, akieleza sababu za kuendelea kushiriki kwenye kamati, Machunde alikiambia kikao cha kamati kuwa, amelazimika kufanya hivyo kwa kuwa hadi kufikia jana alikuwa hajapokea majibu kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete ya kuomba kujitoa katika kamati hiyo.

" Mpaka sasa sijapata jibu la ombi langu kwa Rais. Hivyo, nitakuwa mkosefu wa heshima kama sitashiriki katika vikao vya kamati kabla sijapata jibu kutoka kwa Rais," alisema Machunde.

Baadaye mchana, Jaji Bomani alikutana na waandishi wa habari na kuwaeleza kuwa, wajumbe walioomba kujitoa kwenye kamati hiyo, walishiriki kikao cha jana na kuongeza kuwa ana matumaini kuwa wataendelea kushiriki.

Hata hivyo, tofauti na alivyosema awali, alikanusha Tarimo kuwasilisha barua ya kuomba kujitoa, bali barua hiyo inahusu wasiwasi wa kushiriki kwake kwenye kamati.

" Tunatumai wasiwasi hautakuwapo, atafanya kazi vizuri na hakutakuwa na mgongano wa maslahi, " alisema.

Kuhusu wajumbe wengine waliotakiwa na Chadema kujitoa kwenye kamati hiyo kutokana na kutuhumiwa kwa ufisadi au mgongano wa maslahi, alisema katika kikao cha jana, hakukuwapo na majadiliano kuhusu wajumbe wengine zaidi ya Mchunde na Tarimo.

Jaji Bomani, alisema kikao cha jana ambacho kilihudhuriwa na wajumbe wake wote, isipokuwa wawili kutokana na kupatwa na udhuru, kili panga ratiba na kuafikiana namna kamati itakavyotekeleza majukumu yake.

Alisema mbali na kukutana na wenyeviti au wawakilishi wa kamati zilizoteuliwa katika siku za nyuma kuchunguza kuhusu madini, pia watakutana na wadau mbalimbali pamoja na umoja wa wachimbaji madini na kutembelea kwenye maeneo yenye shughuli za machimbo.

Jaji Bomani , alisema katika ratiba hiyo, pia watembelea nchi zenye sekta ya madini ili kujifunza namna wanavyoedesha shughuli za madini na kutoa nafasi kwa wananchi kutoa maoni kabla ya kamati kukaa na kutafakari waliyoyapata na kuandaa ripoti watakayoiwasilisha serikalini katika muda muafaka.

Hata hivyo, alisema kutokana na muda na gharama kuwa finyu, watachagua nchi chache ambazo zimepata mafanikio katika shughuli za madini na kwamba, hadi kufikia jana walikuwa bado hawajakamilisha orodha ya nchi hizo na tarehe ya kuanza ziara hiyo.

Awali, akifungua kikao hicho, Jaji Bomani aliwapongeza wajumbe kwa kuteuliwa kwenye kamati, lakini akawapa pole kwa maelezo kwamba, jukumu walilopewa ni nyeti na zito.

Hata hivyo, alisema watafanya kazi kwa bidii, uaminifu wa hali ya juu ili mapendekezo yatakayotolewa na kamati yawe na maslahi mazito kwa taifa.

Aliwataka wajumbe wawe huru kutoa maoni yao wenyewe, na siyo ya kutumwa na chombo au taasisi au chama, kwani wameteuliwa kwa sifa binafsi.

" Tutoe fikra zetu na mependekezo yetu, tusiwe na ubinafsi, tutapelekea kupishana katika kutoa mapendekezo ya kamati. Tutoe mapendekezo ya kamati ili kazi yetu ifanyike kwa uwazi, siyo kwa siri siri. Pia katika ratiba yetu tutoe nafasi watu watoe mawazo yao hadharani na wakaribishwe wasomi watoe mawazo yao ili yafanyiwe kazi, " alisema Jaji Bomani.

Alisema kabla ya kutangaza mapendekezo yao, watashauriana na Rais Kikwete kwamba, wayatangaze au wampe ayapitie kwanza.

Akizungumza katika ufunguzi huo, Mbunge wa Bariadi Mashariki (UDP), John Cheyo, alisema kazi iliyo mbele yao ni nzito, hivyo, akawataka Watanzania wawaombee kwa Mwenyezi Mungu wapate hekima ya kutoa maamuzi mazuri kwa kuwa, nia yao ni moja ya kujaribu kusaidia taifa kupata maslahi kutokana na utajiri wa madini uliopo nchini.

Wajumbe wengine wa kamati hiyo ni Mwanasheria wa Wizara ya Nishati na Madini, Salome Makange, Kamishina wa Sera Wizara ya Fedha, Mugisha Kamugisha, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Makazi Wizara ya Ardhi, Edward Kihundwa, Mbunge wa Kyela (CCM), Dk Harrison Mwakyembe na mtaalamu wa masuala ya kodi na Mkurugenzi wa Madai na Sheria za Kimataifa, Wizara ya Katiba na Sheria, Maria Kejo.

Kamati hiyo iliundwa na Rais Kikwete Novemba 13, mwaka huu na itatekeleza kazi yake kwa kipindi cha miezi mitatu ambayo ni pamoja na kuchambua mfumo wa kodi unaotumika katika sekta ya madini na kupitia mfumo wa usimamizi wa shughuli za uchimbaji mkubwa unaofanywa na serikali.

Mengine ni kukutana na taasisi zinazosimamia madini na wadau wengine na kutakiwa kutoa taarifa yenye mapendekezo na kupitia mikataba ya madini na nyaraka nyingine zitakazohusu migodi ya mikubwa nchini.
 
HAIWEZEKANI MTU ALIYEJITOA NA KUTANGAZWA KATIKA VYOMBO VYA HABARI KUHUDHURIA VIKAO AKIDAI KWAMBA HAJAPATA MAJIBU KUTOKA KWA RAIS, KWANI YEYE ALIMWANDIKIA RAIS BARUA KUKUBALI UTEUZI? KWANI ASIPOHUDHURIA ATASHITAKIWA? HIVI KUDAI KWAMBA KUTOSHIRIKI ANGEONEKANA ANAMDHARAU RAIS KUNA TOFAUTI GANI NA KUTANGAZA KUJIUZULU ALIKOFANYA NA KUPELEKA TAARIFA KATIKA MAGAZETI? AMA NDIO BAADA YA DK. RASHIDI KUOMBWA ARUDI NA WAO SASA WANATAKA WABEMBELEZWE NA RAIS? SASA ITAKUA KILA ANAYEBANWA KUJIUZULU ANAFANYA HIVYO HALAFU ANATEGEA KUOMBWA NA ARUDI AKIWA AMEVUNJA ZILE NGUVU ZA WANAOTAKA AJIUZULU? TANZANIA KUNA MBWEMBWE ZA AJABU SANA.

Hapa dalili kubwa kwamba siasa zinaweza kutumika kuhakikisha wajumbe hao ambao walikwishakujitoa wabaki na hiyo inatokana zaidi na Chadema kutoa kauli ya "Kumtaka" rais atekeleze mambo fulani fulani, huku Ikulu na CCM wakitoa majibu ya kupinga kauli hizo. Kuanzia hapo suala hilo sasa limegeuka kuwa "mtaji" mpya wa kisiasa wa CCM baada ya Chadema kuonekana kuchezea "shilingi chooni", shilingi ambayo si CCM pekee bali hata vyama vingine viliitamani sana. Chadema pamoja na kuwa na sababu za msingi kabisa kutilia shaka Kamati hiyo, walidhihirisha uchanga wao katika mikakati ya kisiasa kwa kushindwa "kufanya siasa" na badala yake wakamwaga hadharani mambo ambayo wangeweza kutumia mbinu za kuyawasilisha kwa awamu na kwa maandalizi ya kutosha ili kuweza kuendelea na nguvu kubwa waliyoipata katika suala zima la kuonekana kutetea rasilimali za taifa na hasa madini amnbayo ni utajiri mkubwa ambao hauonekani kwa watu wa kawaida.

Pamoja na hali hiyo, Chadema/wapinzani bado wana nafasi kubwa ya kuendelea kutumia hoja ya madini kwani bado wananchi hawajabadilika pamoja na propaganda kubwa ya CCM kuonyesha kwamba wao/serikali ndio yenye dhamira/nia/mkakati/lengo la kuhakikisha madini yanawanufaisha wananchi wote. Hata ikionekana kwamba Chadema/wapinzani hawana hoja/takwimu/taarifa sahihi, bado wananchi wataendelea kuamini kwamba "serikali/CCM" wametumia nguvu ya dola na uwezo wa kifedha katika kuficha taarifa hizo.

Naamini kama Chadema/wapinzani wana nia ya kuendelea kupata kuungwa mkono, basi watumie gharama ili kushirikisha watu wa aina mbalimbali wanaoaminika katika kutoa ushauri ama kupanga mikakati ya kuhakikisha badala ya kurudi nyuma wanasonga mbele. Wakipoteza nafasi hii watajuta na CCM haitawapa tena nafasi ya kufurukuta nina hakika CCM itatumia kila aina ya mbinu walizo nazo ikiwamo fedha, vyombo vya habari, dola, wataalamu, vibaraka na hata mbinu nyingine chafu zaidi kuhakikisha wanadhibiti kasi ya Chadema/wapinzani kusonga mbele.

Chadema/wapinzani wamtumie Zitto kwa uangalifu na kwa kumshauri ili kutengeneza hoja na kuendeleza hoja zilizopo badala ya kumkatisha tamaa na kumshambulia kwani, WASIJIDANGANYE Zitto pamoja na kuwa ni kijana, amepata umaarufu mkubwa kwa sasa kuliko mwanasiasa yeyote wa upinzani na nafasi hiyo itumike kujenga nguvu ya upinzani kwa uangalifu na malengo ya muda wa awali, wa kati na muda mrefu. KAMA KUNA NIA YA DHATI YA KUWATUMIKIA WATANZANIA, Hakuna kinachoshindikana.
 
Tulikwisha sema tangu mwanzo, hii ilikuwa kazi ya bunge lakini kwa ajili ya umbumbumbu wanachaguliwa wajumbe kwa kura za turufu. Umefika wakati wabunge wasimame kidete ili wahesabiwe, kama kazi imewashinda wawaachie wenye machungu na nchi yetu.
 
Kabla hata page ya pili ya thread haijaingia yametokea soma mwananchi hapa...

http://www.mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=3191

MJUMBE wa Kamati ya Kuangalia Upya Mikataba ya Uchimbaji Madini nchini, David Tarimo, aliyeomba kujitoa katika ushiriki wa kamati hiyo, amebadili uamuzi wake.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Jaji Mark Bomani aliliambia Mwananchi jana kuwa Tarimo ambaye ni Mkaguzi wa Mahesabu kutoka Kampuni ya Kimataifa ya Ukaguzi wa Mahesabu ya PriceWaterhouseCoopers, alifikia uamuzi huo baada ya kushauriwa na wajumbe kuendelea kushiriki katika kamati.
 
hivi huu ndio mtindo wa kisasa "tishia kujiuzulu, halafu usijiuzulu"...

its the simplest way to catch peoples attention and make u feel so important
 
HAya Tanzania Daima haooo..... Ama kweli vituko.....ama SIASA ama SII HASA za BONGOLAND... hii ndio Ze Comedy haswaaaa

Vituko Kamati ya Madini

na Mwandishi Wetu

HALI ya mambo ndani ya Kamati ya Rais ya Kuchunguza Mikataba ya Madini nchini, bado haijatulia tangu wajumbe wawili wa kamati hiyo watangaze kujitoa kwa nyakati tofauti.
Habari za uhakika ambazo Tanzania Daima imezipata kutoka Ofisi ya Rais Ikulu zinaeleza kuwa, tayari Rais Jakaya Kikwete amesharidhia uamuzi wa mmoja wa wajumbe hao kujitoa, huku mwingine akiendelea kuwa mjumbe ndani ya kamati hiyo.

Ofisa mmoja wa juu wa serikali aliyezungumza na Tanzania Daima jana, alisema kwamba Rais Kikwete alikuwa ameridhia uamuzi wowote utakaochukuliwa na Mwenyekiti wa Soko la Hisa la Dar es Salaam, Peter Machunde, ambaye wiki iliyopita aliwasilisha barua yake ya kujitoa katika kamati hiyo ya watu 12 iliyoanza kazi yake rasmi juzi.

Kwa mujibu wa ofisa huyo, wakati Kikwete akiridhia uamuzi wa Machunde kujitoa au kuendelea kuwamo katika kamati hiyo, juzi mjumbe huyo alihudhuria kikao cha kwanza cha kamati hiyo kilichokutana katika ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam.

Ofisa huyo wa juu wa serikali alipoulizwa iwapo kuridhia huko kwa rais kunakinzana na kauli iliyotolewa juzi na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Jaji Mark Bomani, aliyesema wajumbe wote walikuwa wamekamilika, alisema suala hilo litapata ufumbuzi wa kudumu iwapo Machunde ataandika barua nyingine ya kufuta uamuzi wake wa awali.

Kimsingi anachosema rais ni kwamba, Machunde anao uhuru wa kuamua, kujiondoa katika kamati au la… Sasa kama kuna jambo lolote tofauti na kwa kuzingatia kwamba aliandika barua ya kujiuzulu, basi atapaswa kuandika barua ya kufuta uamuzi wake wa mwanzo," alisema ofisa huyo wa juu wa Ikulu ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini.

Kuhusu Tarimo, ofisa huyo wa Ikulu alisema kuwa anaendelea kubakia kuwa mjumbe katika kamati hiyo baada ya washirika wake katika kampuni ya kimataifa ya ukaguzi wa mahesabu ya Price Water Coopers (PWC) kuridhia.

"Unajua sababu kuu iliyomfanya Tarimo atoe sababu ya kutaka kujitoa katika kamati hiyo ilikuwa ni ukweli kwamba alikuwa hajaruhusiwa na partners (washirika) wenzake kuwa mjumbe katika kamati hiyo. Tatizo hilo halipo tena, kwani partners wenzake PWC wameridhia aendelee kubakia katika kamati," alisema ofisa huyo wa Ikulu.

Pamoja na suala hilo, taarifa za awali zinaonyesha kuwa, sababu nyingine ambayo ilimfanya Tarimo afikie uamuzi wa kujiuzulu, ilikuwa ni kuonekana kuwapo kwa mgongano wa kimaslahi unaotokana na kampuni yake ya PWC kuyakagua mahesabu ya kampuni kadhaa za madini.

Hata hivyo, taarifa za uhakika ambazo Tanzania Daima ilizipata kutoka kwa watu walio karibu na Tarimo zinaeleza kuwa, aliteuliwa kuwa mjumbe wa kamati hiyo bila ya kutaarifiwa.

Chanzo kimoja huru cha habari kilichozungumza na Tanzania Daima jana kilieleza kwamba, Tarimo alikuwa akitajwa kuwa mmoja wa watu muhimu ambao kuwamo kwao ndani ya kamati hiyo, kulikuwa kukipewa uzito mkubwa na Rais Kikwete mwenyewe.

Taarifa ambazo gazeti hili lilikuwa limezipata kabla ya jana zinaeleza kuwa, Machunde alihudhuria kikao cha kamati hiyo juzi kutokana na ukweli kwamba, ombi lake la maandishi aliloliwasilisha mwishoni mwa wiki iliyopita la kutaka rais amuondoe, lilikuwa halijapata majibu rasmi.

Sambamba na hilo, yeye pia alikuwa mmoja wa wajumbe waliogawiwa makabrasha yote muhimu yanayojumuisha mikataba yote ya madini na ripoti mbalimbali ambazo wanatakiwa kuzisoma hadi Jumapili ya wiki hii, kabla kamati hiyo haijakutana kuanzia Jumatatu ijayo.

Akizungumza na wanahabari baada ya kamati hiyo kukutana kwa mara ya kwanza juzi, Jaji Bomani, bila ya kuingia katika undani wa suala hilo alisema, kamati yake ilikuwa ikijumuisha wateule wote waliotangazwa na Rais Jakaya Kikwete, Novemba 13 na 14.

Bomani alieleza kuwa, kamati yake ilikuwa ikitarajia kuwaita wenyeviti wote wa kamati nne za madini zilizowahi kuundwa siku zilizopita, ambazo ripoti zake zilikabidhiwa kwa wajumbe wote wa kamati hiyo jana.

Kwa mujibu wa Bomani, wenyeviti hao wataitwa na kuhojiwa ili kuiwezesha kamati kupata kile ambacho tayari kamati walizoziongoza zilibaini katika sekta ya madini, hatua ambayo kwa kiwango fulani inaonyesha mwelekeo wa kujibu dukuduku zilizotolewa na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) siku chache zilizopita.

Jaji Bomani alisema hatua ya kukutana na viongozi hao, itasaidia kupata maelezo mahimu yatakatayoisaidia kamati yake kupata taarifa mbalimbali za kuzifanyia kazi.

"Tumekutana kwa mara ya kwanza tangu tulipoteuliwa na Rais Jakaya Kikwete, moja ya suala kubwa tulilokubalina na wajumbe wangu ni kukutana na viongozi waliowahi kuteuliwa kushughulikia migogoro katika sekta ya madini kwa siku za nyuma," alisema Jaji Bomani.

Kabla ya kamati hii ya Bomani, kamati nyingine za madini zilizopatwa kuundwa huko nyuma na miaka yake ikiwa katika mabano ni ile ya Jenerali Mboma (2001), Brigedia Mang'enya (2003), Dk. Kipokola (2004) na ya Masha (2006).

Bomani alisema mbali ya kukutana na viongozi hao wa kamati zilizopita, wamepanga kukutana na wadau na viongozi wa Umoja wa Wachimbaji Madini Tanzania, ili kupata maoni yao.

Alisema kamati yake itatoa fursa kwa watu mbalimbali kutoa maoni na dukuduku zao ambazo wanaamini kwamba zitawasaidia kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Alisema kikao hicho kimekubaliana kwa kauli moja kuwa kamati ifanye ziara katika baadhi ya migodi mikubwa hapa nchini, ili kujionea na kujifunza hali halisi na kupata maoni ya wakuu wa migodi hiyo.

Aidha, licha ya kutembelea migodi mikubwa hapa nchini, Jaji Bomani alisema wajumbe wa kamati wamekubaliana pia kuwa watembelee nchi kadhaa za Afrika, ambazo zimekuwa na mafanikio makubwa katika sekta ya madini. Hata hivyo hakuwa tayari kuzitaja nchi hizo."Tutatembelea nchi hizi kwa lengo la kujifunza na kuona wao wamefikiaje mafanikio waliyonayo na kuweza kuepukana na matatizo kama haya tuliyonayo sisi," alisema Jaji Bomani akirejea kauli ya Novemba 3, mwaka huu ya Rais Kikwete, aliyesema serikali itaiwezesha kifedha kamati hiyo kutembelea nchi mbalimbali duniani kujifunza namna zinavyosimamia sekta ya madini.

Pamoja na Bomani, Machunde na Tarimo, wajumbe wengine ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto (CHADEMA), Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige (CCM), Mbunge wa Kyela Dk. Harrison Mwakyembe (CCM), Mbunge wa Bariadi Mashariki na Mwenyekiti wa United Democratic Party (UDP), John Cheyo na mwanasiasa mkongwe, Iddi Simba.

Wapo pia Mwanasheria wa Wizara ya Nishati na Madini, Salome Makange, Kamishna wa Sera Wizara ya Fedha, Mugisha Kamugisha, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Makazi Wizara ya Ardhi, Edward Kihundwa na Mkurugenzi wa Madai na Sheria za Kimataifa kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Maria Kejo.

Hadidu za rejea za kamati hiyo zinaonyesha kuwa itapitia mikataba ya madini na nyaraka nyingine zinazohusu migodi mikubwa na kuchambua mfumo wa kodi unaotumika katika sekta hiyo.

Aidha, kamati itapitia mfumo wa usimamizi wa shughuli za uchimbaji mkubwa unaofanywa na serikali, itachambua na kuainisha haki na wajibu wa mwekezaji na serikali na pia itakutana na ‘Chamber of Minerals' na wadau wengine na kutoa mapendekezo kwa serikali.
 
Lakini huyu David Tarimo si Mtanzania, ni Muingereza....je ayasariti makampuni ya kwao au aangalie maslahi ya waswahili!
 
Lakini huyu David Tarimo si Mtanzania, ni Muingereza....je ayasariti makampuni ya kwao au aangalie maslahi ya waswahili!

Nego, pamoja na mapungufu yote ya David Tarimo, hakuna dalili za kuwa si Mtanzania, labda kama ana uraia wa nchi mbili ama uraia wa namna nyingine maana Tarimo ni kutoka mkoani Kilimanjaro na zaidi ni kutoka kabila la wachaga... Usishange mtu akasema wewe Nego kweli ni Mtanzania? Maana kama unasema Tarimo ni Muingereza basi kama wewe ni Mtanzania basi utakua ulikua unaishi "geti kali" na umesoma "academy" ama nje ya nchi kwa mwana hujachanyika na makabila ya Kitanzania, maana Wachaga wako kila mahali Tanzania. Vinginevyo SIJAKUELEWA ULIKUA NA MAANA GANI
 
Halisi,
Kwani Uraia wa nchi mbili unaruhusiwa Tanzania siku hizi? Mimi nijuavyo, hauruhusiwi!
Kama yeye Mtanzania kwa nini basi hajakana Uingereza wake, maana kaishi siku nyingi hapa akiwa nafanya kazi PricewaterhouseCoopers...Ukweli unabaki pale pale, David si Mtanzania kisheria! Labda hoja yako ikiwa kwamba, si lazima uwe Mtanzania ili kuchaguliwa kwenye kamati ya Rais.
Halisi, hilo jina la kichagga Tarimo, lisikupotoshe...Rais kateua mgeni kwenye kamati ya madini...huu ndio ukweli.
 
CHADEMA walishalisema hili kuwa baadhi ya wajumbe wa Tume ya Madini deals na Makampuni ya Madni lakini Gazeti la Uhuru,UV CCM na Mhariri wa Daily News na Baadhi ya watu wakawaona hawana akili. Bravo, Tundu Lissu!

Hata hivyo hili halishangazi hata kidogo, Tarimo ni mtu mwenye akili sana na ndiyo maana akatangaza mapema kuwa hawezi kutenda haki kwa maana kampuni yake ina mahusiano ya Kibiashara na Kampuni za Madini lakini kwa sababu inaonekana kuna sababu maalumu ya kuwaweka hawa wajumbe wanaolalamikiwa basi wanalzimisha tu kuwa wawemo na hii ni aibu.

Kama JK ana nia ya dhati kuhakiki na kurekebisha mikataba ya madini ni bora awatoe wote wanaolalamika na Wapinzani. Juzi jioni nilimsikiliza Dk. Slaa kwenye Darubini ya Siasa katika Star TV nikaona kuwa Wapinzania wana hoja za msingi na si za Kiasiasa kama vile CCM, UVCCM, Uhuru na Daily News wanavyojaribu kutushawishi bali ni Utaifa.
 
Inaelekea Kikwete anawateua watu kwa kutumia vyombo vya habari, what a colloquial goof!
 
HAya Tanzania Daima haooo..... Ama kweli vituko.....ama SIASA ama SII HASA za BONGOLAND... hii ndio Ze Comedy haswaaaa

Halisi
Hapa umenichanganya kidogo. Tanzania Daima wamepika habari au nini? Au kuna ka-vita kasikoonekana, isipokuwa kwa kutumia miwani special?
 
CHADEMA walishalisema hili kuwa baadhi ya wajumbe wa Tume ya Madini deals na Makampuni ya Madni lakini Gazeti la Uhuru,UV CCM na Mhariri wa Daily News na Baadhi ya watu wakawaona hawana akili. Bravo, Tundu Lissu!

Hata hivyo hili halishangazi hata kidogo, Tarimo ni mtu mwenye akili sana na ndiyo maana akatangaza mapema kuwa hawezi kutenda haki kwa maana kampuni yake ina mahusiano ya Kibiashara na Kampuni za Madini lakini kwa sababu inaonekana kuna sababu maalumu ya kuwaweka hawa wajumbe wanaolalamikiwa basi wanalzimisha tu kuwa wawemo na hii ni aibu.

Kama JK ana nia ya dhati kuhakiki na kurekebisha mikataba ya madini ni bora awatoe wote wanaolalamika na Wapinzani. Juzi jioni nilimsikiliza Dk. Slaa kwenye Darubini ya Siasa katika Star TV nikaona kuwa Wapinzania wana hoja za msingi na si za Kiasiasa kama vile CCM, UVCCM, Uhuru na Daily News wanavyojaribu kutushawishi bali ni Utaifa.
Kumbe Lissu alianza kitambo sana harakati za kupambana na mikataba mibovu ya madin???
 
Back
Top Bottom