David Tarimo naye amejitoa kamati ya Madini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

David Tarimo naye amejitoa kamati ya Madini?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Asha Abdala, Nov 28, 2007.

 1. A

  Asha Abdala JF-Expert Member

  #1
  Nov 28, 2007
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 1,134
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Yule David Tarimo wa PWC naye anaelekea kutaka kujitoa. Walau huyu anastahili heshima kwa kutambua mgongano wa kimaslahi kuliko Machunde aliyesingizia CHADEMA

  Kamati ya madini yageuka kama maigizo
  *Mwingine aandika barua ya kujitoa
  *Aliyejitoa wa kwanza, wa pili wahudhuria

  * Iddi Simba ahamaki waandishi kuwako ndani

  * Bomani awataka wajumbe kuweka maslahi ya taifa mbele


  Muhibu Said na Mwanaid Omary


  KAMATI ya Kuangalia Upya Mikataba ya Uchimbaji Madini nchini, imeanza rasmi kazi zake jana, huku wajumbe wake wawili walioomba kwa Rais Jakaya Kikwete kujitoa , wakishiriki.


  Wajumbe hao, ni Peter Machunde kutoka Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) na Mkaguzi wa Mahesabu kutoka Kampuni ya Kimataifa ya Ukaguzi wa Mahesabu ya PriceWaterhouse Coopers, David Tarimo.


  Hata hivyo, wakati hayo yakijiri, katika moja ya kazi zake, kamati hiyo imepanga kukutana na wenyeviti wa kamati zilizoteuliwa katika siku za nyuma kuchunguza kuhusu madini ili kupata uzoefu wao katika suala hilo, kuanzia Jumatatu na Jumanne wiki ijayo.


  Kamati hizo, ni ile ya Jenerali Robert Mboma iliyoundwa mwaka 2001, ya Brigedia Mang'enya ( 2003), ya Dk Kipokola (2004) na ya Masha (2006).


  Machunde alitangaza kujiuzulu wiki iliyopita kwa madai ya kukerwa na maneno ya baadhi ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ya kumtaka ajitoe katika kamati hiyo kwa madai ya kuwa na urafiki wa karibu na mmoja wa mawaziri wa serikali ya awamu ya nne.


  Taarifa za Tarimo kuomba kujitoa , zilitangazwa jana na Mwenyekiti wa Kamati hiyo , Jaji Mark Bomani wakati akifungua kikao chao cha kwanza katika Ofisi za Bunge, jijini Dar es Salaam.


  Akitoa taarifa hiyo, Jaji Bomani, alisema Tarimo aliwasilisha barua ya kujitoa katika kamati hiyo kama mjumbe kwa madai kwamba kampuni yake inatumiwa na baadhi ya makampuni ya madini, hivyo, ana wasiwasi ushiriki wake unaweza kuleta mgongano wa maslahi, lakini alisisitiza kuwa, atakuwa tayari kutoa ushauri utakapohitajika.


  Hata hivyo, Jaji Bomani alishindwa kusoma barua ya Tarimo, baada ya mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo, Iddi Simba kumzuia asifanye hivyo mbele ya waandishi wa habari kwa madai kwamba, iwapo jambo hilo litawafikia wananchi, linaweza kuibua malumbano mitaani.


  " Watupishe kwanza waandishi wa habari, tujadili sisi wenyewe, pengine baadhi yetu tunataka (Tarimo) asijitoe," alisema Iddi Simba na kuungwa mkono na Mbunge wa Msalala (CCM), Ezekiel Maige.


  Kutokana na ushauri huo, Jaji Bomani aliwataka waandishi wa habari wasitangaze habari hizo kwa muda huo na badala yake wasubiri hadi kamati imalize majadiliano kuhusiana na jambo hilo, kisha mchana watapewa taarifa.


  Maelekezo hayo ya Jaji Bomani, yalipingwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, aliyesema kuwa, haoni ni busara kuwaita waandishi wa habari kila baada ya kikao na kuishauri kamati iwaruhusu wakaripoti yale waliyokwishayapata kwa muda ule.


  Mapema, Tarimo alikataa kuzungumza chochote alipoulizwa na Jaji Bomani kama ana jambo la kuzungumza kuhusiana na hilo na kumuomba mwenyewe (Bomani) azungumze badala yake.


  Awali, akieleza sababu za kuendelea kushiriki kwenye kamati, Machunde alikiambia kikao cha kamati kuwa, amelazimika kufanya hivyo kwa kuwa hadi kufikia jana alikuwa hajapokea majibu kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete ya kuomba kujitoa katika kamati hiyo.


  " Mpaka sasa sijapata jibu la ombi langu kwa Rais. Hivyo, nitakuwa mkosefu wa heshima kama sitashiriki katika vikao vya kamati kabla sijapata jibu kutoka kwa Rais," alisema Machunde.


  Baadaye mchana, Jaji Bomani alikutana na waandishi wa habari na kuwaeleza kuwa, wajumbe walioomba kujitoa kwenye kamati hiyo, walishiriki kikao cha jana na kuongeza kuwa ana matumaini kuwa wataendelea kushiriki.


  Hata hivyo, tofauti na alivyosema awali, alikanusha Tarimo kuwasilisha barua ya kuomba kujitoa, bali barua hiyo inahusu wasiwasi wa kushiriki kwake kwenye kamati.


  " Tunatumai wasiwasi hautakuwapo, atafanya kazi vizuri na hakutakuwa na mgongano wa maslahi, " alisema.


  Kuhusu wajumbe wengine waliotakiwa na Chadema kujitoa kwenye kamati hiyo kutokana na kutuhumiwa kwa ufisadi au mgongano wa maslahi, alisema katika kikao cha jana, hakukuwapo na majadiliano kuhusu wajumbe wengine zaidi ya Mchunde na Tarimo.


  Jaji Bomani, alisema kikao cha jana ambacho kilihudhuriwa na wajumbe wake wote, isipokuwa wawili kutokana na kupatwa na udhuru, kili panga ratiba na kuafikiana namna kamati itakavyotekeleza majukumu yake.


  Alisema mbali na kukutana na wenyeviti au wawakilishi wa kamati zilizoteuliwa katika siku za nyuma kuchunguza kuhusu madini, pia watakutana na wadau mbalimbali pamoja na umoja wa wachimbaji madini na kutembelea kwenye maeneo yenye shughuli za machimbo.


  Jaji Bomani , alisema katika ratiba hiyo, pia watembelea nchi zenye sekta ya madini ili kujifunza namna wanavyoedesha shughuli za madini na kutoa nafasi kwa wananchi kutoa maoni kabla ya kamati kukaa na kutafakari waliyoyapata na kuandaa ripoti watakayoiwasilisha serikalini katika muda muafaka.


  Hata hivyo, alisema kutokana na muda na gharama kuwa finyu, watachagua nchi chache ambazo zimepata mafanikio katika shughuli za madini na kwamba, hadi kufikia jana walikuwa bado hawajakamilisha orodha ya nchi hizo na tarehe ya kuanza ziara hiyo.


  Awali, akifungua kikao hicho, Jaji Bomani aliwapongeza wajumbe kwa kuteuliwa kwenye kamati, lakini akawapa pole kwa maelezo kwamba, jukumu walilopewa ni nyeti na zito.


  Hata hivyo, alisema watafanya kazi kwa bidii, uaminifu wa hali ya juu ili mapendekezo yatakayotolewa na kamati yawe na maslahi mazito kwa taifa.


  Aliwataka wajumbe wawe huru kutoa maoni yao wenyewe, na siyo ya kutumwa na chombo au taasisi au chama, kwani wameteuliwa kwa sifa binafsi.


  " Tutoe fikra zetu na mependekezo yetu, tusiwe na ubinafsi, tutapelekea kupishana katika kutoa mapendekezo ya kamati. Tutoe mapendekezo ya kamati ili kazi yetu ifanyike kwa uwazi, siyo kwa siri siri. Pia katika ratiba yetu tutoe nafasi watu watoe mawazo yao hadharani na wakaribishwe wasomi watoe mawazo yao ili yafanyiwe kazi, " alisema Jaji Bomani.


  Alisema kabla ya kutangaza mapendekezo yao, watashauriana na Rais Kikwete kwamba, wayatangaze au wampe ayapitie kwanza.


  Akizungumza katika ufunguzi huo, Mbunge wa Bariadi Mashariki (UDP), John Cheyo, alisema kazi iliyo mbele yao ni nzito, hivyo, akawataka Watanzania wawaombee kwa Mwenyezi Mungu wapate hekima ya kutoa maamuzi mazuri kwa kuwa, nia yao ni moja ya kujaribu kusaidia taifa kupata maslahi kutokana na utajiri wa madini uliopo nchini.


  Wajumbe wengine wa kamati hiyo ni Mwanasheria wa Wizara ya Nishati na Madini, Salome Makange, Kamishina wa Sera Wizara ya Fedha, Mugisha Kamugisha, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Makazi Wizara ya Ardhi, Edward Kihundwa, Mbunge wa Kyela (CCM), Dk Harrison Mwakyembe na mtaalamu wa masuala ya kodi na Mkurugenzi wa Madai na Sheria za Kimataifa, Wizara ya Katiba na Sheria, Maria Kejo.


  Kamati hiyo iliundwa na Rais Kikwete Novemba 13, mwaka huu na itatekeleza kazi yake kwa kipindi cha miezi mitatu ambayo ni pamoja na kuchambua mfumo wa kodi unaotumika katika sekta ya madini na kupitia mfumo wa usimamizi wa shughuli za uchimbaji mkubwa unaofanywa na serikali.


  Mengine ni kukutana na taasisi zinazosimamia madini na wadau wengine na kutakiwa kutoa taarifa yenye mapendekezo na kupitia mikataba ya madini na nyaraka nyingine zitakazohusu migodi ya mikubwa nchini.
   
 2. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #2
  Nov 28, 2007
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Yaani sielewi elewi, naona giza tu
   
 3. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #3
  Nov 29, 2007
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  HAIWEZEKANI MTU ALIYEJITOA NA KUTANGAZWA KATIKA VYOMBO VYA HABARI KUHUDHURIA VIKAO AKIDAI KWAMBA HAJAPATA MAJIBU KUTOKA KWA RAIS, KWANI YEYE ALIMWANDIKIA RAIS BARUA KUKUBALI UTEUZI? KWANI ASIPOHUDHURIA ATASHITAKIWA? HIVI KUDAI KWAMBA KUTOSHIRIKI ANGEONEKANA ANAMDHARAU RAIS KUNA TOFAUTI GANI NA KUTANGAZA KUJIUZULU ALIKOFANYA NA KUPELEKA TAARIFA KATIKA MAGAZETI? AMA NDIO BAADA YA DK. RASHIDI KUOMBWA ARUDI NA WAO SASA WANATAKA WABEMBELEZWE NA RAIS? SASA ITAKUA KILA ANAYEBANWA KUJIUZULU ANAFANYA HIVYO HALAFU ANATEGEA KUOMBWA NA ARUDI AKIWA AMEVUNJA ZILE NGUVU ZA WANAOTAKA AJIUZULU? TANZANIA KUNA MBWEMBWE ZA AJABU SANA.


  Hapa dalili kubwa kwamba siasa zinaweza kutumika kuhakikisha wajumbe hao ambao walikwishakujitoa wabaki na hiyo inatokana zaidi na Chadema kutoa kauli ya "Kumtaka" rais atekeleze mambo fulani fulani, huku Ikulu na CCM wakitoa majibu ya kupinga kauli hizo. Kuanzia hapo suala hilo sasa limegeuka kuwa "mtaji" mpya wa kisiasa wa CCM baada ya Chadema kuonekana kuchezea "shilingi chooni", shilingi ambayo si CCM pekee bali hata vyama vingine viliitamani sana. Chadema pamoja na kuwa na sababu za msingi kabisa kutilia shaka Kamati hiyo, walidhihirisha uchanga wao katika mikakati ya kisiasa kwa kushindwa "kufanya siasa" na badala yake wakamwaga hadharani mambo ambayo wangeweza kutumia mbinu za kuyawasilisha kwa awamu na kwa maandalizi ya kutosha ili kuweza kuendelea na nguvu kubwa waliyoipata katika suala zima la kuonekana kutetea rasilimali za taifa na hasa madini amnbayo ni utajiri mkubwa ambao hauonekani kwa watu wa kawaida.

  Pamoja na hali hiyo, Chadema/wapinzani bado wana nafasi kubwa ya kuendelea kutumia hoja ya madini kwani bado wananchi hawajabadilika pamoja na propaganda kubwa ya CCM kuonyesha kwamba wao/serikali ndio yenye dhamira/nia/mkakati/lengo la kuhakikisha madini yanawanufaisha wananchi wote. Hata ikionekana kwamba Chadema/wapinzani hawana hoja/takwimu/taarifa sahihi, bado wananchi wataendelea kuamini kwamba "serikali/CCM" wametumia nguvu ya dola na uwezo wa kifedha katika kuficha taarifa hizo.

  Naamini kama Chadema/wapinzani wana nia ya kuendelea kupata kuungwa mkono, basi watumie gharama ili kushirikisha watu wa aina mbalimbali wanaoaminika katika kutoa ushauri ama kupanga mikakati ya kuhakikisha badala ya kurudi nyuma wanasonga mbele. Wakipoteza nafasi hii watajuta na CCM haitawapa tena nafasi ya kufurukuta nina hakika CCM itatumia kila aina ya mbinu walizo nazo ikiwamo fedha, vyombo vya habari, dola, wataalamu, vibaraka na hata mbinu nyingine chafu zaidi kuhakikisha wanadhibiti kasi ya Chadema/wapinzani kusonga mbele.

  Chadema/wapinzani wamtumie Zitto kwa uangalifu na kwa kumshauri ili kutengeneza hoja na kuendeleza hoja zilizopo badala ya kumkatisha tamaa na kumshambulia kwani, WASIJIDANGANYE Zitto pamoja na kuwa ni kijana, amepata umaarufu mkubwa kwa sasa kuliko mwanasiasa yeyote wa upinzani na nafasi hiyo itumike kujenga nguvu ya upinzani kwa uangalifu na malengo ya muda wa awali, wa kati na muda mrefu. KAMA KUNA NIA YA DHATI YA KUWATUMIKIA WATANZANIA, Hakuna kinachoshindikana.
   
 4. Dua

  Dua JF-Expert Member

  #4
  Nov 29, 2007
  Joined: Nov 14, 2006
  Messages: 2,481
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Tulikwisha sema tangu mwanzo, hii ilikuwa kazi ya bunge lakini kwa ajili ya umbumbumbu wanachaguliwa wajumbe kwa kura za turufu. Umefika wakati wabunge wasimame kidete ili wahesabiwe, kama kazi imewashinda wawaachie wenye machungu na nchi yetu.
   
 5. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #5
  Nov 29, 2007
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Kabla hata page ya pili ya thread haijaingia yametokea soma mwananchi hapa...

  http://www.mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=3191

   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  Nov 30, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  hivi huu ndio mtindo wa kisasa "tishia kujiuzulu, halafu usijiuzulu"...
   
 7. The Invincible

  The Invincible JF-Expert Member

  #7
  Nov 30, 2007
  Joined: May 6, 2006
  Messages: 4,723
  Likes Received: 1,213
  Trophy Points: 280
  hii kali. kwamba ukijiuzulu unatekeleza madai wapinzani. tishia kukubaliana na wapinzani, halafu rudi kundini.
   
 8. Kinyau

  Kinyau JF-Expert Member

  #8
  Nov 30, 2007
  Joined: Nov 24, 2006
  Messages: 793
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 60
  its the simplest way to catch peoples attention and make u feel so important
   
 9. M

  Mwakilishi JF-Expert Member

  #9
  Nov 30, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 484
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Naona Ze comedy wamepata washindani sasa, kazi kwa wananchi!
   
 10. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #10
  Nov 30, 2007
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  HAya Tanzania Daima haooo..... Ama kweli vituko.....ama SIASA ama SII HASA za BONGOLAND... hii ndio Ze Comedy haswaaaa


   
 11. N

  Nego Member

  #11
  Nov 30, 2007
  Joined: Oct 25, 2006
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Lakini huyu David Tarimo si Mtanzania, ni Muingereza....je ayasariti makampuni ya kwao au aangalie maslahi ya waswahili!
   
 12. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #12
  Nov 30, 2007
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Nego, pamoja na mapungufu yote ya David Tarimo, hakuna dalili za kuwa si Mtanzania, labda kama ana uraia wa nchi mbili ama uraia wa namna nyingine maana Tarimo ni kutoka mkoani Kilimanjaro na zaidi ni kutoka kabila la wachaga... Usishange mtu akasema wewe Nego kweli ni Mtanzania? Maana kama unasema Tarimo ni Muingereza basi kama wewe ni Mtanzania basi utakua ulikua unaishi "geti kali" na umesoma "academy" ama nje ya nchi kwa mwana hujachanyika na makabila ya Kitanzania, maana Wachaga wako kila mahali Tanzania. Vinginevyo SIJAKUELEWA ULIKUA NA MAANA GANI
   
 13. N

  Nego Member

  #13
  Nov 30, 2007
  Joined: Oct 25, 2006
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Halisi,
  Kwani Uraia wa nchi mbili unaruhusiwa Tanzania siku hizi? Mimi nijuavyo, hauruhusiwi!
  Kama yeye Mtanzania kwa nini basi hajakana Uingereza wake, maana kaishi siku nyingi hapa akiwa nafanya kazi PricewaterhouseCoopers...Ukweli unabaki pale pale, David si Mtanzania kisheria! Labda hoja yako ikiwa kwamba, si lazima uwe Mtanzania ili kuchaguliwa kwenye kamati ya Rais.
  Halisi, hilo jina la kichagga Tarimo, lisikupotoshe...Rais kateua mgeni kwenye kamati ya madini...huu ndio ukweli.
   
 14. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #14
  Nov 30, 2007
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  CHADEMA walishalisema hili kuwa baadhi ya wajumbe wa Tume ya Madini deals na Makampuni ya Madni lakini Gazeti la Uhuru,UV CCM na Mhariri wa Daily News na Baadhi ya watu wakawaona hawana akili. Bravo, Tundu Lissu!

  Hata hivyo hili halishangazi hata kidogo, Tarimo ni mtu mwenye akili sana na ndiyo maana akatangaza mapema kuwa hawezi kutenda haki kwa maana kampuni yake ina mahusiano ya Kibiashara na Kampuni za Madini lakini kwa sababu inaonekana kuna sababu maalumu ya kuwaweka hawa wajumbe wanaolalamikiwa basi wanalzimisha tu kuwa wawemo na hii ni aibu.

  Kama JK ana nia ya dhati kuhakiki na kurekebisha mikataba ya madini ni bora awatoe wote wanaolalamika na Wapinzani. Juzi jioni nilimsikiliza Dk. Slaa kwenye Darubini ya Siasa katika Star TV nikaona kuwa Wapinzania wana hoja za msingi na si za Kiasiasa kama vile CCM, UVCCM, Uhuru na Daily News wanavyojaribu kutushawishi bali ni Utaifa.
   
 15. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #15
  Nov 30, 2007
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Inaelekea Kikwete anawateua watu kwa kutumia vyombo vya habari, what a colloquial goof!
   
 16. The Invincible

  The Invincible JF-Expert Member

  #16
  Nov 30, 2007
  Joined: May 6, 2006
  Messages: 4,723
  Likes Received: 1,213
  Trophy Points: 280
  Halisi
  Hapa umenichanganya kidogo. Tanzania Daima wamepika habari au nini? Au kuna ka-vita kasikoonekana, isipokuwa kwa kutumia miwani special?
   
 17. Jambazi

  Jambazi JF-Expert Member

  #17
  Aug 21, 2017
  Joined: Jan 18, 2014
  Messages: 14,438
  Likes Received: 12,607
  Trophy Points: 280
  Kumbe Lissu alianza kitambo sana harakati za kupambana na mikataba mibovu ya madin???
   
Loading...